YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,995
Katika watu wanaoongoza kwa utoro kazini ni wabunge. Huingia ofisini kwao muda wapendao na hutoka muda wanaojitakia. Kila mtu ukienda ofisi ya mbunge humkuti yuko kwenye mishe mishe zake wakati mshahara analamba kama kawaida.
Naomba kule kwenye ofisi zao majimboni mbunge naye awe anasaini kaingia ofisini saa ngapi na kutoka saa ngapi ili atulie ofisini. Daftari hili ikiwezekana lilwe lile lile wanalosaini wafanyakazi ofisi ya mkuu wa wilaya kama ofisi yake iko eneo la ofisi ya mkuu wa wilaya.
Wabunge hawana udhibiti wa kuwepo ofisini. Hii tabia lazima ikome. Mtu kama anaona muda mwingi anakuwa kwenye biashara zake haoni ulazima wa kukaa ofisini ahudumie wananchi kwa nini aombe ubunge?
Ofisi ya bunge na serikali ihakikishe wabunge wanakuwemo maofisini mwao toka asubuhi hadi muda wa kazi kumalizika.

Last edited by a moderator: