Wazo zuri sana,lakini kwa nini unapendekeza walau wawe wamehitimu kidato cha sita?uelewo na elimu ya mtu nadhani havina uhusiano wa moja kwa moja ,ndio maana watu kama kina zuma ambaye ni rais wa afrika ya kusini wameweza kufikia ngazi hizo.mifano ni mingi...............labda tutafute njia nyingine ya kupima uelewa wa mtu,na sio elimu ya darasani............hebu fikiria wanasheria wetu kwa mfano,wanaoingia mikataba ambayo hata mtu wa kawaida asiye na elimu ya sheria anaweza kuikosoa,angalia madarasa yanayojengwa chini ya kiwango;tatizo sio ueledi ila ni ubinafsi wa kutaka kujinufaisha binafsi,kutokomeza mishahara hewa kwa mfano, tunahitaji mshauri muelekezi? Nadhani tatizo ni kuwa watanzania wengi tumepoteza uzalendo..........unamchagua kiongozi bila kuzingatia uwezo wake,bali masilahi binafsi.