Wabunge wawe na elimu ya kidato cha sita na kuendelea

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
4,916
2,452
Nimekuwa nikifuatilia mijadala wakati wa vikao vya bunge letu tukufu,nilichogundua ni kwamba uwezo wa baadhi wabunge wetu ni duni mno kiasi ya kuwa wanashindwa kuchangia mijadala muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu.Rai yangu ni kwamba uchaguzi wa 2015 ni lazima vyama vyote vya siasa kuhakikisha ya kuwa wabunge wao wanakuwa na elimu ambayo itamsaidia si tu kuchangia mijadala ndani ya bunge pamoja na kuelewa miswada ambo huwa inakuwa imeandikwa kwa lugha ya kingereza
 
Wazo zuri sana,lakini kwa nini unapendekeza walau wawe wamehitimu kidato cha sita?uelewo na elimu ya mtu nadhani havina uhusiano wa moja kwa moja ,ndio maana watu kama kina zuma ambaye ni rais wa afrika ya kusini wameweza kufikia ngazi hizo.mifano ni mingi...............labda tutafute njia nyingine ya kupima uelewa wa mtu,na sio elimu ya darasani............hebu fikiria wanasheria wetu kwa mfano,wanaoingia mikataba ambayo hata mtu wa kawaida asiye na elimu ya sheria anaweza kuikosoa,angalia madarasa yanayojengwa chini ya kiwango;tatizo sio ueledi ila ni ubinafsi wa kutaka kujinufaisha binafsi,kutokomeza mishahara hewa kwa mfano, tunahitaji mshauri muelekezi? Nadhani tatizo ni kuwa watanzania wengi tumepoteza uzalendo..........unamchagua kiongozi bila kuzingatia uwezo wake,bali masilahi binafsi.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala wakati wa vikao vya bunge letu tukufu,nilichogundua ni kwamba uwezo wa baadhi wabunge wetu ni duni mno kiasi ya kuwa wanashindwa kuchangia mijadala muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu.Rai yangu ni kwamba uchaguzi wa 2015 ni lazima vyama vyote vya siasa kuhakikisha ya kuwa wabunge wao wanakuwa na elimu ambayo itamsaidia si tu kuchangia mijadala ndani ya bunge pamoja na kuelewa miswada ambo huwa inakuwa imeandikwa kwa lugha ya kingereza

Unafikiri itasaidia hiyo?! Mbona wengi wao (haswa wa CCM) wana hadi degrees za kutoka Harvard lakini ni bure tu?!? Kuna usemi kwamba ukishakua mbunge kupitia CCM, akili na utashi vinaachwa pale Lumumba Street au HQ pale Dodoma.
 
Mr. Makupa, is this the end of your tether? Sorry it does'nt work that way!!!!!!!!!!!:photo:
 
Mi napendekeza Wabunge wawe wanalipwa mshahara wa KIMA cha CHINI.

Hawa ingewezekana wakalipwa toka katika makusanyo ya Halmashauri husika za Majimbo yao naamini ingewafanya wawajibike zaidi. Fikiria matumizi ya Halmashauri yanapobandikwa kwenye ofisi zake na wananchi wakaona kodi yao iliyotumika kumlipa Mh na wakati hajafanya aliyoahidi unadhani mwezi unaofuata watakubali alipwe?

Yaweza kusaidia kuwatia akili ya uwajibikaji na kupunguza fix zao!
 
Mi napendekeza Wabunge wawe wanalipwa mshahara wa KIMA cha CHINI.

Naunga mkono, ubunge ndiyo iwe kazi ya wito...mtu asigombee kimaslahi zaidi.Tumechoka kusikia ualimu na udaktari kuwa ndiyo kazi za wito
 
Mi napendekeza Wabunge wawe wanalipwa mshahara wa KIMA cha CHINI.

Mkuu tatizo sio mshahara per se, ni miposho ya kila aina na msururu wa marupurupu. Labda ungekazia kwa kusema unapendekeza
pamoja na mshahara wa kima cha chini, na kukomesha posho na marupurupu mengine.

Hata sasa hivi wanakwambia mshahara ni kama 2m, lakini kila mwezi wanaondoka na 12m wakiwa kwenye vikao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom