Wabunge wanaopinga ofisi za serikali kuhamishiwa UDOM watambue haya...

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Wabunge wamekomalia Serikali isiweke ofisi zake kwa muda Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ati utaratibu huo ni hatari kwa maendeleo ya wanafunzi - kutafanya wanafunzi wasijikite katika masomo!

Najiuliza kama hao Wabunge wenye mawazo hayo ni kwa sababu gani na kwa faida ya nani!

Hivi hawajui kama shule nyingi tangu za awali, msingi na sekondari zimejengwa au zimezungukwa na makazi ya watu hadi mahoteli, nyumba za wageni, mabaa, masoko au makusanyiko ya watu wenye shughuli nyingi na mbalimbali!

Hivi hawajui, wanafunzi wa vyuo vikuu ni watu wazima ambao baada ya masomo ni viongozi, au baadhi yao ni viongozi tayari! Wana uwezo wa kumudu changamoto za kimaisha na masomo.

Wanafunzi wa kutetea ni wale watoto wanaosoma kwenye shule ambazo zimejengwa kwenye sehemu zisizo rafiki.

TAFAKARINI CHUKUENI HATUA.
 
Back
Top Bottom