Wabunge wamkaanga Waziri Ngeleja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wamkaanga Waziri Ngeleja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 16, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,494
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wabunge wamkaanga Waziri Ngeleja [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 15 July 2011 20:33 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Leon Bahati, Dodoma
  Mwananchi

  WABUNGE jana walimweka kitimoto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja baadhi yao wakimtuhumu kwa kudanganya kwenye bajeti yake na kurundika miradi ya umeme jimboni kwake (Sengerema) na kwa maswahiba wake ambao pia ni mawaziri.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti Bungeni jana, wabunge hao walisema bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2011/12, ni mbaya na mbovu isiyofaa hata kupitishwa.

  Wakichangia makadirio ya matumizi ya wizara yaliyowasilishwa Bungeni jana asubuhi na Waziri Ngeleja, wengi wao walieleza kutoridhishwa na mipango iliyomo katika hotuba ile.

  Mbunge wa Same Mashariki (CCM) Anne Kilango Malecela na mwnezake wa Nkasi, Ally Mohamed pia wa CCM ndio walioanza kumwashia moto Ngeleja na kisha kufuatiwa na wabunge wengine.

  Kilango, ambaye amekuwa mpambanaji dhidi ya ufisadi alilalamika kuwa utekelezaji wa miradi ya umeme umependelea zaidi mawaziri wakati kwenye jimbo lake wamelaghaiwa.

  Alitaja baadhi ya mawaziri alidai wamependelewa ni Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) wa Jimbo la Same Mashariki, Aggrey Mwanri (Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- Tammisemi) kutoka Jimbo la Siha na Profesa Jumanne Magembe (Kilimo, Chakula na Ushirika) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga.

  Kilango alilalamika kwamba kwenye hotuba ya Ngeleja alitaja vijiji ambavyo vimesambaziwa umeme kwenye jimbo la Same Mashariki, lakini ukweli vyote vipo Same Magharibi, kwa waziri mwenzake, Dk Mathayo.Kilango hakuvitaja vijiji hivyo, lakini kwa mujibu wa hotuba ya Ngeleja ni Mhezi, Ijinyu, Kijom, Msindo, Mbakweni, Kizungo na Digo.

  Alimtaka waziri huyo kuacha kudanganya Watanzania na huku akionyesha upendeleo wa wazi kwa kupeleka miradi mingi ya umeme kwenye majimbo ya maswahiba wake.Mbunge huyo alilalama, "Sisi (wabunge) wote tuko hapa kwa kazi moja tu nayo ni (kujadili) namna ya kuondoa matatizo ya Watanzania. Lakini, mengine tunayoyafanya ni ya kitoto."

  Akionyesha kukasirishwa na kuzungumza kwa jazba, Kilango alisema tatizo la umeme linawatesa sana Watanzania.

  Akaitaka Serikali iachane na mpango wa kufikiria yenyewe namna ya kutatua tatizo la umeme nchini badala yake iwashirikishe na wengine.

  Katika hatua nyingine, Kilango alisema serikali haitaweza kutatua tatizo la umeme nchini iwapo itaendelea na tabia yake ya kubeba miradi mingi kwa wakati mmoja.

  Alisema kitendo hicho husababisha miradi hiyo kushindikana kutekelezwa ama maendeleo yake kwenda kidogo kidogo na kutofikia malengo yake kwa wakati uliokusudiwa.Alisema tatizo la umeme nchini ni la muda mrefu, lakini utatuzi wake umekuwa ni mgumu kwa sababu katika mikakati yake, upo utitiri wa miradi.

  Tatizo hilo, alisema linatokana na Serikali kutohusisha mawazo ya watu wengine katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme.Naye Mbunge wa Nkasi (Ally Mohamed) katika mchango wake alimlaumu Ngeleja kwa kile alichosema ni kudanganya kwenye hotuba yake kuwa katika wilaya yake tayari mradi wa kusambaza umeme umetekelezwa kwa asilimia 62.

  Mohamed alisimama baada ya Ngeleja kumaliza hotuba yake na kuomba kutoa taarifa kuwa waziri huyo alikuwa amelidanganya Bunge.

  "Alisema (Waziri Ngeleja) kuwa njia ya umeme wa msongo mkubwa umekamilika na usimikaji wa nguzo umetekelezwa kwa asilimia 62. Huu ni uongo. Hakuna hata nguzo iliyochimbiwa ardhini," alilalamika Mohamed.

  Alisisitiza kwamba hataunga hoja ya waziri huyo kwa sababu kuna udanganyifu mwingi na kuonya kwamba kama ni maofisa wake, basi walimpelekea taarifa potofu.

  Kauli ya Ngeleja
  Awali, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake jana, Waziri Ngeleja aliorodhesha utitiri wa miradi ya umeme ambayo inalenga kumaliza tatizo la umeme nchini.

  Alisema kuwa mpango wa bajeti hiyo umezingatia mikakati mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa kama vile, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano, Malengo ya Maendeleo ya Milenia na sera za CCM."Lengo la Serikali ni kuimarisha na kuboresha sekta ya nishati na kuongeza fungamanisho la sekta ya madini na sekta nyingine," alisema Ngeleja.

  Alitaja miradi 16 akisema ni miongoni mwa ile itakayotekelezwa na Serikali ili kuongeza uzalishaji wa umeme, kupanua na kuboresha njia za umeme, kuendeleza na kupanua miundombinu ya gesi asilia.

  Miongoni mwa miradi aliyoitaja Ngeleja ni ule wa mitambo ya kufua umeme ya megawati 100 jijini Dar es Salaam ambao alisema utakamilika Desemba mwaka huu na megawati 60 jijini Mwanza ambao utakamilika Juni mwakani.

  Miradi mingine pamoja na muda wa kukamilika kwenye mabano ni Kinyerezi (Dar es Salaam) wa megawati 240 (2013/14), Mnazi Bay (Mtwara) wa megawati 300 (2013/14), Somanga Fungu (Kilwa), megawati 230 (2013/14)Ruhudji, megawati 358 (2015/16).

  Mingine ni mgodi wa makaa ya mawe Kiwira (Mbeya) megawati 200 (2013/14), Ngaka wa megawati 400 (2014/15), Mchuchuma megawati 600 (2014/15), Murongo/Kikagati (Kagerea) wa megawati 16 ambao utategemea kukamilika kwa makubaliano kati ya Serikali ya Uganda na Tanzania.
  Aliitaja miradi mingine kuwa ni Rusumo (Kagera) wa megawati 63 ambao upo kwenye taratibu za kutafutiwa fedha, Stiegler's Gorge (Pwani) wa megawati 2,100 na Mpanga wa megawati 165 (2015/16).

  Pia, aliitaja mingine kuwa ni Rumakali wa megawati 222 (2018), Dar es Salaam-Tanga ambayo ni ya dharura ikijumuiasha Symbion (megawati 112.5), Aggreko (megawati 100), ununuzi wa mitambo itakayofungwa Majani Mapana, Tanga wa megawati 70 na ule wa gesi wa IPTL, Tegeta jijini Dar es Salaam.

  Waziri huyo aliitaja miakakati mingine ya kuboresha sekta ya nishati ni kuunganisha makao makuu zote za wilaya, kuendelea kusambaza umeme vijijini, utekelezaji wa miradi iliyopo chini ya MCC pamoja na miradi mingine midogo ya umeme ukiwepo unaotokana na nishati ya jua.

  Akizungumzia kuhusu sekta ya madini, Ngeleja alisema Sheria ya Madini ya mwaka 2010 imefanyiwa marekebisho mbalimbali ili kuboresha usimamizi wa sekta hiyo."Marekebisho hayo ni pamoja na mfumo wa ukokotoaji wa mrahaba na viwango vipya na ada mbalimbali za leseni za madini," alisema Ngeleja.

  Alifafanua kuwa, "Kisheria marekebisho hayo yatawagusa wawekezaji wapya na kampuni ambazo hazina miakataba na serikali."Alisema kuwa Serikali ipo katika mikakati ya kuwasiliana na kampuni ambazo tayari zina mikataba ili sheria hiyo mpya waitekeleze.Migodi hiyo aliitaja kuwa ni Bulyanhulu, Resolute Tanzania Limited, Geita Gold Mine na Buzwagi Gold Mine.Ili kutekeleza miradi hiyo, Ngeleja aliliomba Bunge liidhinishe Sh402.4 bilioni ikiwa ni pamoja na matumikzi ya kawaida.


  Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameliambia Bunge kuwa uhaba wa umeme unaolikumba Taifa kwa sasa unatokana na tatizo la uongozi.

  "Hakuna 'seriousness' (umakini) katika kutatua tatizo la umeme," alisema Mbowe wakati akichangia hotuba hiyo ya waziri Ngeleja. Alisema tatizo la umeme limekuwa likilikumba taifa kutokana na mipango yake ya utekelezaji kufanywa kisiasa.Alionya kuwa tatizo hili limekuwa likionekana ni dogo lakini linawaathiri watu wengi hasa kampuni na viwanda vilivyowekezwa nchini na linavitishia kuviangamiza kabisa.

  Hali inavyonekana kwa sasa, alisema inaashiria kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amezidiwa kutokana na kurundikiwa mambo mengi ayafanya kwa wakati mmoja.Kwa sababu hiyo akapendekeza wizara hiyo igawanywe mara mbili kutokana na unyeti wa mambo iliyo nayo juu ya sekta ya madini na nishati.

  Alitoa mfano kuwa suala la madini na nishati limekuwa na wawekezaji wajanja sana kiasi kwamba mtu anapokuwa ameelemewa na mambo mengi, anaweza kujikuta akiingia kwenye mikataba mibovu.

  Hata hivyo, baada ya kumaliza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alitoa taarifa kuwa kamati ya Makamba ina wajibu wa kuikosoa serikali.Alisema kamati ile inajumuisha wabunge wa pande zote hivyo si ya CCM na ina wajibu wa kuikosoa na kuishauri serikali.

  Mbunge wa Kibakwe George Simbachawene, aliwataka wachimbaji wodogo kufuata sheria ili kuepuka matatizo yasiiyokuwa ya lazima."Mtu ukianza kuchimba madini huwezi kufanya shughuli nyingine atachimba madini tu, serikali iwasaidie hawa wachimbaji wadogo siyo kuwasaidia wakubwa tu,"alisema Simbachawene.

  Mbunge wa Kasulu Vijijini kwa tiketi ya NCCR Mageuzi Agripina Buyogera, alisema kukosa umeme wa uhakika katika Mkoa wa Kigoma, ni matokeo ya kukosa viongozi wazuri wa kuhakikisha Mkoa huo unapata umeme wa uhakika.

  Alieleza kwamba, mkoa huo unarasilimali za kutosha ambazo zinauwezo mkubwa wa kuhakikisha Mkoa huo unakuwa na Nishati kubwa ya umeme."Kila Mwezi Kigoma umeme unaozalishwa na majenereta unakatika kwa zaidi ya wiki moja, hii ni kutokana na kukosekana kwa mafatuta, kwanini isitumike maporomoko ya mito Iliyopo ili kuondoa kero hii,"alisema Buyogera.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Maneno matupu,miradi mingi sana yote ni usanii.mimi haya yote hayanisaidii ni bora waziri akakaa kimya then nchi ikawa na umeme kuliko kula kodi yetu huku utekelezaji ni sifuri.
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwenye soft copy ya bajet ya ngeleja atupe plz!
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  tatizo wanaongea ku-win mioyo ya wapiga kura wao na kupamba vichwa vya habari vya medias but at the end wanaunga mkono na kupitisha bajeti then hali inaendelea kuwa ileile... yaaani hiyo wizara ilitakiwa itoe majibu ya vitendo na si maneno!
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hili ndiyo tatizo la viongozi wetu kuweka siasa kila sehemu, harafu hata akisema uongo hawezi kung'atuka sababu hakuna wa kumwajibisha wala sheria za nchi zinamegwa megwa na mtu anavyotaka anafanya. We need an independent institution itakayokuwa inawashtaki hawa viongozi wahuni wanaosababisha vifo vingo sababu ya ukosefu wa maadili ya uongozi.

  System nzima ikiwa corrupted, hakuna la maana!! hata sisi wananchi hatuwezi kusema sana kwani karibu 80% tunakula milungula kila kukicha. So complicated.
   
 6. p

  plawala JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kila mbunge angechangia kama alivyofanya A Kilango pengine serikali ingeacha tabia ya business as usual

  Na ni tabia hii hii ianyofanywa kila mwaka kutuhadaa watanzania huku wabunge wengi wakichangia chini ya kiwango hasa mda huu ambao umeme umekuwa janga la kitaifa

  Na hii bajeti itapita maana wabunge wanaojiwakilisha wataiunga mkono.
   
 7. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hiyo bajeti ya ngeleja ni usanii mtupu kwani mipango ijayo ni ya uongo mtupu maaan itawezekanaje upange ya kesho wakati ya leo yanakushinda???
   
 8. dkims

  dkims Senior Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hiyi bajeti hata mtambo wa mg 100 hautoshi, hapo ni usanii mtupuu!
   
 9. B

  Baikoko Senior Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi kukaa kimya kwa mtu kama Ngeleja ni gharama kubwa kuliko ahadi hewa?
   
 10. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Megawati kwa porojo anaongoza.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,494
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa bajeti ya Nishati imejaa uongo mwingi na usanii wa hali ya juu lakini itapitishwa tu ili kulinda maslahi ya akina magamba badala ya ya yale ya nchi na hivyo kuendelea kuwa na umeme wa kunahatisha siku hasi siku, mwezi hadi mwezi na pia mwaka hadi mwaka.
   
 12. MWAGONA

  MWAGONA Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumechoka kudanganywa na huyu Ngeleja 2na kumbukumbu kuwa tatizo hili kufikia mwaka huu linnge kuwa historia kumbe imekuwa Historia katika machungu miradi mingi utekelezaji F . Kinachotakiwa kwa katiba mpya tuweke kifungu cha kuwajibishana iwapo waziri or raisi ana danganya wananchi nazaini hii itapunguza kudanganywa kama watoto kila siku
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hii miradi naona daily inatajwa ila sion ikitekelezwa!
   
Loading...