Wabunge wamepuuza mjadala kuhusu mgomo wa madaktari, Kwa hili madaktari mgomo uendelee

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Mh Mnyika CHADEMA na Mh Ndugulile CCM walikuwa na hoja ya dharura leo katika kikao cha bunge, tena hoja ya msingi kwa mustakabari wa afya na uhai wa Watanzania kutokana na mgomo wa madaktari. Kwa vyovyote vile huu ndiyo ulikuwa wakati mwafaka wa bunge kujadili na kutafuta njia ya kutatua utata huu. Hata hivyo wabunge wetu wameonyesha kuwa suala hili halijawagusa kiasi cha kuona hakuna haja ya kuwaunga mkono wenzao. Kwa hili wabunge wetu hawajaonyesha uzalendo. Inaonyesha wanajali maslahi yao zaidi kuliko matatizo ya wananchi walio wengi. Kwa hili madaktari kuna haja ya kuendelea kukaza uzi na kuendelea na mgomo wenu mpaka pale watakapoamua kuwasikiliza.
 
Najua kuwa mgmo unatuathiri walalahoi moja kwa moja, lakini nauunga mkono, kwani ni njia mojawapo ya kuieleza seriikali kuwa kuna mahali mambo hayako sawa. Hawa wabunge hatuwashangai - si wao posho zao mpya wanalipwa!
 
Kwanini Wasipuuze???

419756_223593481065940_100002458688809_480537_1503040120_n.jpg
 
Mnajua kwanini hawakuunga mkono? Wabunge wanaogopa contradiction! Wakiwaponda madaktari kibao kitawageukia kuwa mbona wao wanalipana mapesa mengi kama posho. Wakiwatetea madaktari wanaogopa posho zao serikali itazifuta! wanaogopa kujichanganya. Lakini dhambi hiyo iwe juu yao wao na vizazi vyao!
 
ni zamu ya wauguzi kuwaunga mkono! Wanaamini muda unavyokwenda madaktari watapoa!
 
Akili zao zinawatuma waamini vazi la Taifa ni muhimu kuliko maisha ya watu wanaoteketea bila msaada
 
kuna presha flani kwa Makinda asiruhusu hoja hiyo Bungeni.
Ndo raha ya kuweka mtu wako mahali, waweza tumia rimoti tu
 
Kwa jinsi nilivyoona taharifa ya habari ITV leo usiku hakika inatia majonzi,maskini watanzania wamekufa na wengine wanasubiri kesho ifike wafe kwani hawana tiba yoyote ile

Na hii serikali inaliona na inalifumbia macho kwakuwa wao hawana ndugu wala wao wenyewe hawatibiwi kwenye hizi hospitali za kimaskini,nimejikuta najiuliza hivi tumefikaje hapa,hivi Tanzania kuna serikali kweli,hivi kuna rais hapa Tanzania kweli,hivi kwa watu kufa hivi rais anamkomoa nani madaktari ama wananchi maskini,na kwa hawa wanaokufa serikali itakuwa tayari kuwajibika?

Pamoja na maumivu haya kwetu sisi walalahoi,naunga mkono mgomo huu uendelee mpaka hapo serikali itakapokuwa tayari kuwatimizia matakwa yao,kama ni kufa acha sisi tuendelee kutangulia mbele za haki kwani hata wao siku itafika watakufa kama sisi tena kwa uchungu mkubwa
 
Back
Top Bottom