Wabunge walipwe kutokana na profession yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge walipwe kutokana na profession yao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SirBonge, Apr 2, 2011.

 1. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  'Wabunge walipwe mishahara kutokana na profession zao, kama ni mwalimu, alipwe mshahara wa mwalimu.n.k ili atetee vema masilahi ya wananchi'...Dr. Lwaitama. HII IMETULIA SANA
   
 2. Onambali

  Onambali Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ushauri mzuri, ila tatizo nionalo mimi ni kwamba watakaokuwa wanapata mishahara mikubwa sana (kwa professional zao) wanaweza kutumia nguvu kwa pesa kuwa na influence katika eneo hili la maamuzi. Nionalo mimi ni mishara ya wabunge iwe fixed (sawa kwa wote) ila mwenye taaluma ya kitu zaidi (mfano injinia, mkemia, mchumi n.k) kama anatenda professional yake kupitia sekta au kamati ya bunge apewe mshahara zaidi kulingana na matumizi ya hiyo profession na qualification yake. Kama hana anachochangia basi apate tu huo mshahara wa ubunge. Kwa njia hiyo wabunge hawataua career zao kama ilivyo sasa ambapo magwiji wa professions wanajimaliza kitaaluma kupitia siasa za kitumwa tulizorithi kutoka kwa waliotutawala.
   
 3. E

  Egyptian Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli hiyo imetulia kuliko maji mtungini.Kwani ikiwa hivyo itapunguza wimbi la wataalam kuacha taaluma zao na kukimbilia kwenye siasa.Wengi wamekimbilia huko na bado wengi wanatamani,kutokana na hilo utendaji wa kitaaluma umeporomoka na kuishia kufanya kazi kwa madili na hivyo kuendeleza wimbi la ufisadi.
   
 4. s

  seniorita JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni hoja nzuri ya kutilia maana na kufanya utafiti zaidi...je impact yake kwa constituency ya mheshimiwa ambaye profession yake ni shs malaki tu????? Je, impact ya such a decision kwa utendaji wao....je impact ya such a decision for their ego (those who are paid minimal salary) before those with big mshiko...je impact yake kwa kodi za mlalahi...inaweza kuwa na ka unafuu kwetu walala hoi au ndio tutafinywa zaidi na wale wenye profession kubwa kubwa....ni mengi ya kuzingatia for me at least....
   
 5. N

  Ndinimbya Senior Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mi nadhani ubunge ungekuwa kama heshima tu na wasiwe na mishahara bali posho peke yake, ili tupate wawakilishi wenye nia ya kweli sio wasaka pesa nono zisizo na jasho. Na hii nadhani itapunguza wimbi la wataalam kukimbilia ubunge
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nafikiri wangeendelea kuhold post zao za zamani kama walikuwa civil servant, kwa maana wakinaliza kipindi cha bunge warudi vibaruani mwao, just like others who apply for secondment when going for contractual work. In so doing mishahara yao ya zamani itumike.

  Kwa others kuwe na fixed scale kutokana na majukumu lkn being in various commitees
   
 7. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kuna kitu hatukiangalii vizuri kama taifa.
  Tunalalamika sana tunapo train wataalamu wetu wa fani mbalimbali kama taifa kisha baada ya kufuzu hukimbia nchi na kwenda kufanya kazi nchi zingine. Na wale waliobahatika kupata scholarship za serikali kwenda nje kuongeza maarifa uamua kubaki huko kwasababu ya maslahi mazuri wanayopata.They always look for green pasture. Thats good. Lakini tunasahahu kuwa hata wale waliobaki nchini kisha wakakimbilia kwenye siasa na kuacha kupractice proffesional zao hawana tofauti na wale waliokimbilia nje maana hatufaidi matunda ya kile walicho kisomea. Maana kazi za siasa zinaweza kufanywa na mtu yoyote na ndio maana tunaona kuna watu wenye elimu tangu la saba hadi maprofesa. Suala la malipo kwa nafasi za siasa liangaliwe sana na tujali pia proffesional za watu hili wasikimbie maana tukiendelea hivi tutaanza kuimport wataalamu huku wa kwetu wakiwa wamejazana mjengoni na kwenye positions zingine za kisiasa kwasababu zinalipa zaidi ya proffesional walizozisomea ingawa zina umuhimu mkubwa kwa mstakabali na ukuaji wa taifa letu. Haipendezi kuona mshahara wa Mbunge unazidi mfano mshahara wa Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa au Engineer wa wilaya, au Maprofesa walioko vyuoni kunoa bongo za vijana wetu. Naproffesionals zingine nyingi zinazoweza kifit hapo. Lakini kumbuka mtu yoyote anaweza kuwa mbunge na akawawakilisha watu wake lakini si kila mtu anaweza kufanya kazi yenye kuitaji proffesional ya mtu mwingine. Lazima tuheshimu hilo. Huwa nashangaa ninapoona wabunge wanalalamika waongezewe posho au mishahara. Ninajiuliza ya kazi gani? Kama anaona haitoshi si aache ili wengine wanaodhani kwa pato hilo wanaweza kuwatumikia watu wao wachukue nafasi. Ingawa pia si lazima liendane na mapato ya kada zingine. Lakini suala hili haliwezi kutumika kwa mambo yanayohitaji proffesion. Mfano kama hakimu akigoma kuendesha kesi si kila mtu anaweza kufanya hiyo kazi, lazima uwe umesomea sheria ndo unaweza kufanya kazi yake. Kwa vyovyote vile lazima tujenge utaratibu wa kuheshimu na kujali proffesion za watu kwa matendo na hata kwa mafao pia.
   
 8. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Naungana na Dr. Lwaitama, Mishahara ya wabunge ipunguzwe hata kama si kwa kuangalia professions zao kama kigezo.
  Pia ningependa idadi yao pia ipunguzwe walau kufikia mbunge mmoja kwa watanzania laki tano (1:500,000) ili ukijumlisha wawakilishi wa makundi maalumu na mawaziri (ambao ni vizuri wasiwe wabunge) basi tuwe na bunge la watu kama 200 tu.
  Unajua, inawezekana baadhi yao wanasinzia na kuzomea hovyo bungeni kwa kuwa hakuna nafasi ya wao wote kuwa active kwa wakati husika.
  Ukiunda na baraza lenye namba maalum kikatiba kama ishirini na mbili (22) tu inatosha kabisa kuendesha serikali makini.
   
 9. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nionavyo mimi wabunge walipwe kwa kazi wanayoifanya yaani UBUNGE. Ikiwa bado unaipenda profession yako usikimbilie mjengoni, tulia fanya kazi yako. Mkikimbilia mjengoni kubali yaliyoko huko profession yake umeshaiacha- "You can't eat a cake and have it":drum:
   
 10. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #10
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Kwa hili sikuungi mkono kwa kuwa tutakua na watunga sheria wasiokuwa na elimu na matokeo yake miswaada mibovu kabisa inaweza pitishwa bungeni.
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  sasa prof maji marefu ambaye nasikia alikuwa mganga wa kienyeji atalipwaje? na atakuwa anatetea jamii gani?
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Umenikuna. Hili litakuwa suluhisho la kupata wawakilishi wa kweli na wenye moyo wa kuwatumikia wananchi. Utakuta mtu ansema hadi kufuka mate kinywani kwamba yeye anataka Ubunge ili akawatumikie wananchi ilihali kumbe nia yake ni mshahara mnono na marupurupu ya Ubunge na wala hana hata chembe ya kuwatumikia wananchi. Na hao professionals wakiingia Bungeni wengi wao hukengeuka na kunena ama kutenda tofauti kabisa na matakwa ya professionals zao. Sijui ma professionals wakiingia kwenye jengo la bunge/siasa huwa akili zinawaruka? Sijui huwa wanalogwa hadi kusahau kabisa wajibu wao katika professionals zao. Niliwahi kusikia kuwa bunge lililopita kuna mtu alinaswa akifanya Ulozi/akiloga bungeni!! Huenda kuna matambiko ambayo huwarusha akili ma professionals tunaowaheshimu.
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Umenikuna. Hili litakuwa suluhisho la kupata wawakilishi wa kweli na wenye moyo wa kuwatumikia wananchi. Utakuta mtu ansema hadi kufuka mate kinywani kwamba yeye anataka Ubunge ili akawatumikie wananchi ilihali kumbe nia yake ni mshahara mnono na marupurupu ya Ubunge na wala hana hata chembe ya kuwatumikia wananchi. Na hao professionals wakiingia Bungeni wengi wao hukengeuka na kunena ama kutenda tofauti kabisa na matakwa ya professionals zao. Sijui ma professionals wakiingia kwenye jengo la bunge/siasa huwa akili zinawaruka? Sijui huwa wanalogwa hadi kusahau kabisa wajibu wao katika professionals zao. Niliwahi kusikia kuwa bunge lililopita kuna mtu alinaswa akifanya Ulozi/akiloga bungeni!! Huenda kuna matambiko ambayo huwarusha akili ma professionals tunaowaheshimu.
   
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Qualification yake ni kujua kusoma na kuandika!
  Mshahara wake na posho ni mara kumi ya daktari,mwalimu,mhandisi,mhasibu askari nk!
   
 15. Dadii

  Dadii Senior Member

  #15
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yule mbunge Maji Marefu wa CCM sijui mngemlipa kiasi gani,,, maana by professional yeye ni Mganga wa kienyeji. inanipa tabu hapa kidogo. Tena ni professor eneo lake, kazi kwelikweli.
   
Loading...