Wabunge wajadili UDA kwa dharura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wajadili UDA kwa dharura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  John Mnyika


  Kamati ya Wabunge wa Dar es Salaam jana ilikutana kwa dharura baada ya kupokea taarifa na nyaraka mpya za tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi unaodaiwa kuendelea katika Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

  Ukiukwaji huo wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi, unadaiwa kufanyika kinyume cha maagizo ya mamlaka zinazohusika, likiwamo Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu wa Wabunge hao, John Mnyika, alisema nyaraka ambazo kamati yake imezipokea ni pamoja na barua ya UDA ya Januari 26, mwaka huu.

  Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CBA/Reg/01/UDA, inataka dola za Marekani 133,125 zitolewe kutoka kwenye akaunti ya UDA, ambayo ilishaagizwa awali fedha zisitoke kinyemela. Nyaraka nyingine ni Muhtasari wa kikao kinachodaiwa kuwa cha wanahisa wa UDA cha Februari 13, mwaka huu.

  Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo alidai kuwa ikao hicho kilifanywa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, akiwa ni mwenyekiti pamoja na Robert Kisena aliyetambulishwa kwenye muhtasari huo kama Mwenyekiti Mtendaji wa UDA na Katibu wa Bodi ya Shirika hilo.

  Alidai kikao hicho pamoja na mambo mengine, kilifanya maamuzi haramu ya kubadili waweka saini katika akaunti ya UDA iliyozuiwa kwa lengo la kuwezesha fedha kutolewa kinyemela na Simon Group.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. K

  Kidumbasi Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Mtemvu,Mnyika, Zungu,Iddi Azzan,Dr Faustin, Mdee,Mwaiposa kasoro Mahanga.
  Tumechoka na vikao vyenu. Kama mna ukweli SI MUMSIMAMISHE Masaburi ?
  Tata 30 teyari, menejimenti ya Simon Group Nyinyi kazi yenu Vikao tu,,,
  Au mnataka mkatiwe (RUSHWA) ndio mnyamaze ?
  Corcodio
   
Loading...