Wabunge wahoji fedha za Rambirambi Arusha kutumika kwenye matumizi ya serikali

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Rambirambi za wafiwa zalalamikiwa bungeni, wabunge wataka maelezo kwa nini fedha hiyo imeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
=========
Sakata la matumizi ya rambirambi iliyochangwa kwa lengo la kufariji wafiwa wa wanafunzi 32 na wafanyakazi watatu wa Shule Lucy Vicent Jijini Arusha limetinga bungeni baada ya watunga sheria kutaka maelezo kwanini fedha hizo zimeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.

Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) ndiye aliyefikisha suala hilo bungeni mjini hapo jana aliposimama na kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuhusu matumizi ya Fedha hizo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Rambirambi za wafiwa zalalamikiwa bungeni
 
Hata Nduli Iddi Amin Dada pamoja na udikteta wake wote sidhani kama alifikia kula rambirambi!!!

Yaani hadi napata hofu kwamba huenda hivi sasa serikali ikawa inafurahia majanga!!!

Limekuja tetemeko la ardhi; michango kwa ajili wahanga wakapiga!!!

Bila kujali waliofariki ni watoto wadogo ambao tumezoea kuita Malaika wa Mungu; bado rambirambi zilizotokana na umauti wao zimepigwa!!!!

Yaani serikali inaleta wanajeshi, migari mikubwa mikubwa... tukio kubwa kweli kweli la kuaga miili ya watoto wetu!!

Watu tunadhani, kwa kuona uchungu kutokana na tukio husika serikali imeamua kugharamia shughuli za mazishi!!

From nowhere, tunakuja kujuzwa pesa zingine za rambirambi zimetumika kugharamia shughuli za kuaga marehemu... aaaaaaargh!

Kwani wazazi wa watoto waliwatuma muandae shughuli ya kitaifa?!! Mnaandaa shughuli kuuuuuubwa kumbe lengo lenu mpate nafasi ya kula rambirambi!!!

Hii ni haramu ambayo hata wale Mateja wa Daudi Albert Bashite wanaweza kuogopa kuitenda!!

Hapa majanga yakizidi kutuandama watokee wengine waseme eti Freemason wakati ni laana ya kula rambirambi!!!
 
Rambirambi za wafiwa zalalamikiwa bungeni, wabunge wataka maelezo kwa nini fedha hiyo imeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
=========
Sakata la matumizi ya rambirambi iliyochangwa kwa lengo la kufariji wafiwa wa wanafunzi 32 na wafanyakazi watatu wa Shule Lucy Vicent Jijini Arusha limetinga bungeni baada ya watunga sheria kutaka maelezo kwa nini fedha hizo zimeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) ndiye aliyefikisha swala hilo bungeni mjini hapo jana aliposimama na kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuhusu matumizi ya Fedha hizo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

Naona waatazidai na za kwao pia wakija kusikia zimepangiwa kujenga hospitali
 
Awamu hii tutaona mengi. Mlifikiri kuongoza nchi ni kazi ya mdomoni tu? Ila hili la rambirambi serikali ione aibu ya bukoba hatujasahau bado mnaongeza mengine kama serikali imewashinda kuongoza acheni waje wengini hiyo 2020 ni mbali mno msije mkavamia hadi sadaka za makanisani sababu awamu hii inaonekana mna allergy na hela. Katapila aliwezi kuwa usafiri wa abiria.
 
Rambirambi za wafiwa zalalamikiwa bungeni, wabunge wataka maelezo kwa nini fedha hiyo imeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
=========
Sakata la matumizi ya rambirambi iliyochangwa kwa lengo la kufariji wafiwa wa wanafunzi 32 na wafanyakazi watatu wa Shule Lucy Vicent Jijini Arusha limetinga bungeni baada ya watunga sheria kutaka maelezo kwa nini fedha hizo zimeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) ndiye aliyefikisha swala hilo bungeni mjini hapo jana aliposimama na kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuhusu matumizi ya Fedha hizo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Makosa yalifanyika 2015!wabunge wengine hawakupaswa kuchaguliwa/kuteuliwa kuingia bungeni!siamini kama wananchi jimboni kwake walimtuma kutoa hoja za kitoto kama hizi! !
 
Hata Nduli Iddi Amin Dada pamoja na udikteta wake wote sidhani kama alifikia kula rambirambi!!!

Yaani hadi napata hofu kwamba huenda hivi sasa serikali ikawa inafurahia majanga!!!

Limekuja tetemeko la ardhi; michango kwa ajili wahanga wakalamba!!!

Bila kujali waliofariki ni watoto wadogo ambao tumezoea kuita Malaika wa Mungu; bado rambirambi zilizotokana na umauti wao zimerambwa!!!!

Yaani serikali inaleta wanajeshi, migari mikubwa mikubwa... tukio kubwa kweli kweli la kuaga miili ya watoto wetu!!

Watu tunadhani serikali, kwa kuona uchungu kutokana na tukio husika na hivyo imeamua kugharamia shughuli za mazishi; from nowhere wanaibuka eti michango mingine ya rambirambi imetumika kushughulikia shughuli za kuaga... aaaaaaargh! Kwani wazazi wa watoto waliwatuma muandae shughuli za kitaifa?!! Mnaandaa shughuli kuuuuuubwa kumbe lengo lenu mpate nafasi ya kula rambirambi!!!

Hii ni haramu ambayo hata wale Mateja wa Daudi Albert Bashite wanaweza kuogopa kuitenda!!
Inshort ile migari na jeshi na wageni wote pale tulikodishiwa, ilibidi tulipie huduma Mkuu.
 
Rambirambi za wafiwa zalalamikiwa bungeni, wabunge wataka maelezo kwa nini fedha hiyo imeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
=========
Sakata la matumizi ya rambirambi iliyochangwa kwa lengo la kufariji wafiwa wa wanafunzi 32 na wafanyakazi watatu wa Shule Lucy Vicent Jijini Arusha limetinga bungeni baada ya watunga sheria kutaka maelezo kwa nini fedha hizo zimeelekezwa kwenye matumizi ya Serikali.
Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) ndiye aliyefikisha swala hilo bungeni mjini hapo jana aliposimama na kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuhusu matumizi ya Fedha hizo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Sio bure, hazina kuna jambo
 
Back
Top Bottom