Wabunge wachafua hali ya hewa Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wachafua hali ya hewa Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 18, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,679
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Wabunge wachafua hali ya hewa bungeni
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 17 June 2011 22:27
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Waandishi Wetu
  Mwananchi

  BAADHI ya wabunge wameendelea kuwa mwiba mkali kwa Serikali katika Mkutano wa Nne unaoendelea mjini Dodoma wakijadili hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/12 iliyowasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

  Miongoni mwa wabunge hao ni Nimrod Mkono wa Musoma Vijinini (CCM), ambaye jana alieleza kusudio lake la kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, huku Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa akiiweka Serikali katika mazingira magumu baada ya kueleza kuwa imekuwa ikiwaua watu bila utaratibu.

  Mchungaji Msigwa jana alisababisha mvutano mkubwa bungeni baada ya kudai kuwa Serikali ya CCM inaua na kupiga watu, kauli ambayo aliombwa aithibitishe na Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama.Mchungaji Msigwa alisema Serikali imekuwa ikiwapiga na kuwaua watu wanaodai haki zao kwa kuamini kwamba inatunza amani, huku akitolea mfano wa mauaji ya raia Mjini Arusha na Nyamogo, wilayani Tarime mkoani Mara.

  Kutokana na kauli hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), ambaye pia ni Mbunge wa Isimani (CCM), William Lukuvi aliomba mwongozo huku akitumia Kanuni ya Bunge ya 64 kifungu (a) na (b).“Kwa mujibu wa kanuni hii, mtu yeyote haruhusiwi kuzungumzia jambo ambalo haliko kwenye mjadala lakini Msigwa anasema Serikali ya CCM inapiga watu na kuwaua,” alisema Lukuvi na kuongeza:

  “Ningependa kiti chako (Mwenyekiti wa Bunge), pia na mimi kama sehemu ya Serikali, mzungumzaji (Msigwa) alithibitishie Bunge ni mahali gani Serikali ya CCM imefanya mambo haya, atoe uthibitisho."Akitolea ufafanuzi wa kanuni hiyo, Mhagama alisema kauli iliyotolewa na Mbunge huyo wa Iringa Mjini haipo katika mjadala wa ajenda ya fedha huku akimtaka kuthibitisha kama ina ukweli ama laa.

  “Umeombwa uthibitishe kama kazi ya Serikali ya CCM ni kupiga na kuua watu… Sasa unaweza kufanya mawili, ama ukubali kuthibitisha kauli yako ili nichukue uamuzi wa kikanuni wa kukufanya uthibitishe hilo au uondoe kauli hiyo,” alisema Mhagama.

  Msigwa ambaye wakati akizungumza baadhi ya wabunge walikuwa wakimtaka akae chini alisema: “Serikali imeua watu Arusha, Nyamongo na kuna wanafunzi wamepigwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) na wamelazwa hospitali, siongei mambo ambayo hayana kina… ni Serikali imewaua.”Huku akizungumza kwa umakini Mhagama alisema: “Msigwa naomba ukae chini… kwa hiyo unathibitisha Serikali imeua watu.”

  Akijibu swali hilo Msigwa alisema: “Ndiyo… nakubali Serikali imewaua.”Jibu hilo liliamsha minong’ono kwa baadhi ya wabunge na Mhagama alimtaka mbunge huyo kuwasilisha uthibitisho maalumu huku akimtahadharisha kwamba kama hautajitosheleza, kanuni zitachukua mkondo wake katika kushughulikia suala hilo.Mhagama alizima mvutano huo na kumtaka Msigwa kuendelea kuchangia mjadala wa Bajeti.

  Hata hivyo, badala ya kuendelea kuchangia bajeti hiyo Msigwa aliibua mvutano mwingine baada ya kudai kuwa kuna wabunge ambao hutoa kauli kuhusu maandamano wakiwa bungeni lakini hawachukuliwi hatua yoyote.Kufuatia kauli hiyo, Mwenyekiti wa Bunge alisema kuwa yeye ndiye anayeoa uamuzi wa mwisho huku akimtaka mbunge huyo kukaa chini kama hakuwa na hoja yoyote ya msingi.

  “Kaa chini Mchungaji Msigwa… Nikishafanya uamuzi nimefanya, kama hauna hoja nimwite mchangiaji mwingine aendelee kuzungumza,” alisema Mhagama.Akichangia Bajeti hiyo Msigwa alisema: “Tunapozungumza kuhusu maendeleo ya taifa letu na kwamba nchi yetu imekuwa huru kwa kipindi cha miaka 50, hakuna anayesema nchi hii haijafanya lolote.
  Tunachozungumza ni sawa na kuwa na mtoto wa miaka 10 mwenye tabia ya mtoto wa miaka miwili, taifa letu lina umri wa miaka 50 lakini tunachokizungumza kama kambi ya upinzani ni kwamba tabia za Serikali yetu hazilingani na umri wa mtu aliyekomaa, hapo ndiyo ugomvi unapoanzia.

  ”Alisema mtoto mchanga ana tabia za kulialia lakini mtu mzima anawajibika kulingana na umri wake na kusisitiza kuwa hoja inayozungumzwa na kambi ya upinzani ni umri wa Tanzania na maendeleo ambayo hayalingani na umri huo.“Tunazungumza vitu basic tu (vya msingi), watu wamezungumzia kuhusu kubana matumizi na wabunge wengi wamemsifia Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) kwa kuacha kutumia magari ya bei mbaya VX na kutumia GX, ila mimi naomba nikuseme kidogo Waziri Mkuu,” alisema Msigwa.

  Kauli hiyo ya Msigwa iliibua mvutano mwingine. Safari hii Mhagama alilazimika kutoa ufafanuzi kuhusu kanuni za Bunge kwamba mbunge yeyote akizungumza hatakiwi kumtaja mtu kwa jina.

  “Hapa unaongea na kiti siyo mtu, kwa mujibu wa kanuni mbunge hatakiwi kumshutumu mbunge mwenzake bungeni…, tufuate utaratibu, kama una mambo yako niambie mimi, kanuni zimewekwa ili tufuate utaratibu, Bunge hili ni Mwenyekiti, Naibu Spika, Spika na mzungumzaji,” alisema Mhagama.

  Alipotakiwa kuendelea kuchangia Msigwa alisema Waziri Mkuu aliwahi kwenda mkoani Iringa kwa kutumia ndege mbili na msafara wa magari takribani 50 na kwamba barabara zote zinazoingia mkoani humo kutokea Iringa, Mbeya na Dar es Salaam zilifungwa kwa muda wa saa tano.

  “Hii si dalili nzuri ya kubana matumizi, tunapozungumza kubana matumizi inatakiwa tumaanishe kwa vitendo ili watoto wanaodai haki zao waone watendaji wa Serikali tunafanya kazi vizuri,” alisema Msigwa.

  Kufuatia kauli hiyo iliyomlenga Waziri Mkuu na kukashifu umri wa miaka 50 wa Tanzania, Lukuvi pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka waliomba Bunge kutoa maelekezo ya kina kuhusu kauli zinazotolewa na wabunge kwa kutumia maneno makali na lugha za kuudhi.

  Alipotakiwa kuthibitisha kauli yake kwamba Waziri Mkuu alikwenda mkoani Iringa kwa ndege mbili na msafara wa magari 50 Msigwa alisema;“Mimi nimesema alikuja na ndege mbili, sasa kikawaida sidhani kama kuna mtu anaweza kupanda ndege mbili, pia katika suala la msafara wa magari kulikuwa na magari mengi hata mimi gari yangu ilikuwa katika msafara huo.”Mkono kukwamisha bajeti ya Nishati na Madini

  Mkono alieleza kusudio lake la kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, kutokana na Mgodi wa Buhemba kunuka rushwa kwani hakuna kiongozi wa Serikali wala wapinzani wanaofika eneo hilo lililokuwa machimbo ya dhahabu ya Kampuni ya Meremeta.

  Mbunge huyo alisema haamini kama wamiliki wa eneo hilo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)."Jambo la tatu ninalotaka kuzungumzia ni jambo sugu la Mgodi wa Buhemba, ni suala linalonisumbua kwa miaka kumi na moja hivi sasa, Serikali kila wakati inaniahidi kwamba itafanya kitu kuhusu Buhemba lakini hakuna kitu," alisema Mkono na kuongeza:

  "Mgodi umebaki pale unaachama tu, watu wa Kenya ndiyo wanaofaidi na sisi tunabaki tunashangaa, Waziri Mkuu ameniahidi kwamba atakuja lakini hajawahi kutekeleza ahadi hiyo, sasa nasema wakati Waziri wa Nishati na Madini atakapowasilisha bajeti yake nakusudia, nasema nakusudia kutoa shilingi ili nijue hatima ya jambo hili." Mkono alisema haiingii akilini kwamba eneo hilo limeachwa pori tangu ilipokuwa Meremeta hadi leo na kwamba kuna kila dalili kwamba kutelekezwa kwa mgodi huo kunawanufaisha baadhi ya watumishi wa Serikali na viongozi wa kisiasa wakiwamo wapinzani.

  Umiliki wa mgodi wa dhahabu wa Buhemba mkoani Mara, ni tete kutokana na Serikali kwa maelezo ya Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonekana kuwa si mmiliki.Mgodi huo ulikuwa chini ya Kampuni ya Meremeta, kampuni ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wapinzani katika kwamba iilijihusisha na ufisadi kutokana na ofisi ya CAG kusema hajui taarifa zozote za mgodi huo wala hajawahi kupitia hesabu zake na wala hajui kama ni mgodi wa Serikali.

  Utata wa umiliki wa mgodi huo wa Buhemba, umeendelea kuwapo huku taarifa za awali zikionyesha kuwa ulikuwa unamilikiwa na Kampuni ya Meremeta, ambayo inamilikiwa na Serikali.Mkono aliwahi kunukuliwa akisema mabilioni ya fedha yalitumika katika kuimarisha mgodi huo, hata baada ya kuanza uzalishaji wa dhahabu si Serikali wala wananchi ambao walifaidika na uchimbaji huo wa madini.

  Imeandikwa na Neville Meena, Habel Chidawali, Dodoma na Fidelis Butahe, Dar  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [h=4][/h]
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Yaaani bunge la safari hiii.....ni kijiwe cha KAHAWA tuuu.....
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Bravo Msigwa! Ni kweli sijawahi kuona mtu mmoja akipanda ndege 2 kwa wakati mmoja
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Bye bye Bunge la kuburuzwa la CCM. Karibu Bunge makini lenye kujua haki za wananchi. Inachoshangaza ni kwamba bado CCM ina Wabunge kibao wanaoshabikikia mauaji yanayofanywa na serikali yao -- yaani wao wanaona sawa. Shame on you all CCM MPs -- badfo mnaishi karne ile ya utumwa ya kuburuzwa tu!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Wabunge wa CCM na Spika wao ni vilaza wa kupindukia. Chukua mauaji ya Tarime kwa mfano. Mgazeti, vyombo vya habari viliripoti kwa kina mauaji ya raia wasikokuwa na silaha, hivi Mbunge anatakiwa athibitishe nini? Hata majaeneza yaliyotupwa na polisi wa CCM yalionyershwa kwenye magazeti. Uthibitisho wa nini? Wale martehemu walijipiga risasi wenyewe?CCM mnakera sasa -- tena mnaudhi wananchi kweki kweli -- ne bila shaka kwa sababu mnaporomoka vibaya! Pambaff kabisa!!!!!!!!
   
Loading...