Wabunge wa Upinzani watoka bungeni wakiwa wameziba midomo yao

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
BUNGENI: Wabunge wa upinzani waziba midomo yao kwa karatasi na utepe na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakigomea kushiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika.

Hii staili ya leo ya wapinzani kutoka bungeni imenipa maswali mengi sana, imenitisha mpaka namehisi kitu flani hivi hapa nilipo. Hii ni staili mpya kabisa.

Sasa naona tunakoelekea sio kizuri, huu utaratibu wa kufanya maamuzi kwa ubabe mwisho wa siku hua hakuna mshindi. Hii ni aibu kubwa sana ambayo ameipata Naibu spika.Nimtake tu atafute suluhu na wabunge hawa zaidi atazidi kudhalilishwa pasina sababu


.

13495001_1043923152366010_5851559993147660337_n.jpg


ClYF7GIVYAEBMvl.jpg


ClYF7GGUYAQn8mV.jpg


 
Hivi hawa ukawa kweli wana akili sawa sawa leo naona wame-edit staili yao ya kutoka bungeni kwa kubandika makaratai kwenye midomo yao sasa sijui hasa walichokuwa wanamaanisha wakati tuliambiwa hakuna aliye wazuia kuingia bungeni ni utashi wao wenyewe

Sasa naanza kuliona kaburi la upinzani 2020 sijui kama watatoboa tena hawa dah kweli za kuambiwa changanya na zako tangu wameaambiwa hawataki kuchanganya zao
 
Hii staili ya leo ya wapinzani kutoka bungeni imenipa maswali mengi sana, imenitisha mpaka namehisi kitu flani hivi hapa nilipo. Hii ni staili mpya kabisa.

Sasa naona tunakoelekea sio kizuri, huu utaratibu wa kufanya maamuzi kwa ubabe mwisho wa siku hua hakuna mshindi. Hii ni aibu kubwa sana ambayo ameipata Naibu spika.Nimtake tu atafute suluhu na wabunge hawa zaidi atazidi kudhalilishwa pasina sababu.
Naibu Spika ameaibikaje sasa, yaani waache kuaibika waliofanya huo utoto aibike Naibu Spika, hebu tuache ushabiki wa kimbeya mbeya!
 
Mi naona ccm wakae watafakari kinachotokea sababu hapo sio huyo naibu anadhalilika serikali nzma na democrasia inapotea kabisa. Sasa kutakua na faida gani kua na bunge la ccm tu. HakutKua na mashiko ya bunge kwa namna biyo
 
Hakuna kuweka suluhu, Dk Tulia aendelea kukaza tu, kama wapinzani wanadhani wanamkomoa Dk Tulia ni wajinga, hasara ni kwa waTz waliowapigia kura, 2020 si mbali, tutasikia malalamiko mengi ya tulishindwa kufanya tuliyo ahidi kwa sababu tulibanwa.
Hivi kwa akili zako hao waliobaki ndani watatekeleza waliyoyaahidi kwa kuwa wanabaki bungeni? usijifanye kujivua akili hivi umeona au kusikia michango ya hao waliobaki ndani je ina tija kwa Taifa.
 
Naibu Spika ameaibikaje sasa, yaani waache kuaibika waliofanya huo utoto aibike Naibu Spika, hebu tuache ushabiki wa kimbeya mbeya!
Hapa sio ushabuki mkuu unatakiwa uache kutafuta majibu mepesi kwenye maswali magumu, sitaki kuelewa kwamba umeshindwa kabisa kuweza kuelewa tafsiri ya hizo mask? Au unataka kuniambia wewe unaakili kuliko kundi lote pale bungeni? Nadhan hata wewe pia una haja ya kuacha ushabiki wakimbeambea
 
Hivi kwa akili zako hao waliobaki ndani watatekeleza waliyoyaahidi kwa kuwa wanabaki bungeni? usijifanye kujivua akili hivi umeona au kusikia michango ya hao waliobaki ndani je ina tija kwa Taifa.
Kwa hiyo hao waliotoka nje wanawafaidisha nini waTz kwa kutoka nje, acha waendelee na maigizo, 2020 si mbali wananchi watatoa hukumu kama walichagua wawakilishi waende kususia bunge.
 
Aisee kumbe hili ni tatizo kubwa tofauti na ninavyolichukulia, Dr must step down to rescue this situation, sioni sababu ya kuonyesha ubabe katika hili, na bajeti hii ndio itadhihirisha umuhimu wa upinzani bungeni, kifupi huwezi kuendelea kama hukubali kukosolewa
 
Back
Top Bottom