figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,717
- 55,819
Hali ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge, baada ya wabunge wote wa Upinzani kutoka ndani ya bunge, mara baada ya Wabunge kuanza kuchangia hotuba ya Rais.
Baada ya Maswali na Majibu, yalifuata matangazo, baada ya Matangazo, wabunge wakaanza kuomba muongozo lakini Naibu Spika Mhe. Tulia, hakuweza kuwapa nafasi ya Kuongea. Mtu akiomba Muongozo anasimama na kusema Mimi nikisimama mbunge inabidi ukae, Mbunge akikaa anamuita mchangiaji. Mbunge akiomba muongozo, naibu Spika anasimama tena na kusema nikisimama inabidi ukae.
Mwisho wa yote wabunge wa Upinzani wakaamua kutoka nje kwa kile wanachodai wamenyimwa nafasi ya kusikilizwa walipoomba muongozo ndani ya bunge.
Wabunge wa CCM, wanaendelea na kujadili Hotuba ya Rais.