Wabunge wa NCCR Kutoka Mkoa wa Kigoma kuunguna na wanaukombozi leo - Bungeni kuwaka Moto

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Leo Asubuhi Wabunge wa NCCR Mageuzi kutoka Mkoa wa Kigoma watasema neno fupi bungeni kuhusiana na udhalimu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa ccm na Police juu ya wananchi na kisha watatoa tamko kali bungeni kwa serkali ya ccm na police wake.

Baada ya Matamko hayo Wabunge hao kwa pamoja watatoka Bungeni na kuelekea Arusha kuungana na watanzania wote katika maombolezo ya Taifa kuelekea uhuru wa kweli.

Lakini kwasasa juhudi kubwa zinafanywa na viongozi wa CCM na Baadhi ya Mawaziri kuwanyamazisha vijana hawa wasiseme kitu Bungeni leo juu ya kile ambacho wamekipanga kwani kitaivua nguo serikali na kuwafanya baadhi ya wabunge wa CCM wenye itikadi za upinzani kuanza kupingana rasmi na kina Mwigulu na serikali ya CCM. Mh Mbatia kwasasa anasemekana kutumiwa kuwashinikiza lakina vijana kutoka Kigoma wanasema liwalo na liwe lazima Serikali iwajibike na wao lazima watie Timu Arusha kwa mapambano ya haki. Vijana wanasema hawezi kusali ummaa kwa pesa za mafisadi

my take Wabunge wa Chama changu CCM ambao hamko mlengo wa Mafisadi na mitandao yao hebu ishinikizeni Serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani iwajibike kwa hili swala la Arusha msiendeshwe kama gari bovu na kina lukuvi, nape na mwigulu wakati nguvu ya umma ndani ya CCM ya Nyerere na hata Chadema itawaunga mkono kwa lolote litakalotokea.

Nawatakia kila la kheri Wabunge wa NCCR kutoka kigoma kwa maamuzi yao magumu ya kuleta mshikamano wa kitaifa kwa kuwakacha wana CCM Bungeni leo nakuungana na Watanzania wote katika kupaza sauti ya haki juu ya Damu isiyo na hatia inayomwaga na Police na CCM Mafisadi.
 
safi saana wabunge kwa kujitambua mungu awatie nguvu katika hili.
 
Bunge letu la bajeti limedoda baada makamanda wa CHADEMA kutokuwepo. Nimeamini CHADEMA ndo wanaotoa changamoto kwenye maswala ya kitaifa.Vyombo vyote vya habari vinaripoti ya Arusha,wanakouawa na kuumizwa raia na polisi.Kenya na Uganda wanajadili uchumi wao,sisi tunapigwa risasi na mabomu.
 
Ifanyikaje sasa kwa kuandamana bungeni au? any way tusubiri tuone! Mbatia wee Kafulila umemsahau!!!!
 
Cuf vip?
Wapinzani wa bongo bure kabisa.,badala ya kuungana katika mambo ya msingi kama haya wao wanatengana,.
Hovyo sana
CUF haiwezi kushirikiana na CHADEMA, wameshaona faida ya Jino kwa jino ilipo wafikisha, CHADEMA bado wanasafari refu sana.
 
Wanaakili wale nyinyi si muanawaita CCM B na mukakataa kuunda KAMBI MOJA BUNGENI
kambi rasmi ya upinzani ipo kwa mujibu wa kanuni na si nani anataka nini... Kama wameamua kuungana ni wao wameona wafanye hivyo na busara ya kawaida inamtaka anayechagua jambo jema asikatishwe tamaa na aungwe mkono.
 
NCCR watakuwa wanafiki wakubwa kama watajihusisha na hawa wahuni wakati juzi baadhi ya wabunge wake walishauri hiki chama kifutwe
 
Back
Top Bottom