Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Rais wa awamu ya tatu Mzee Benjamini Mkapa akiwa katika mkutano wa urathi (legacy) wa Mwalimu Nyerere aliwaongelea wabunge ambao wameingia bungeni katika miaka ya karibuni.
Aliwazungumzia akiongelea namna ambavyo wanashindwa kujenga hoja za maana na wanabakia wakiongelea mambo yasiyofanana na umuhimu wao kwenye taifa linalotaka kuelekea katika mapambano ya uzalishaji wa viwanda.
Rais mstaafu alionyesha mshangao kwa jinsi ambavyo uwepo wa uhuru wa habari unavyoshindwa kutumiwa katika uanzishwaji wa mijadala mipana na yenye tija kwa taifa.
Ninapovitazama vipande vya video za baadhi ya wabunge (clips), naona kabisa kwamba Mheshimiwa Mkapa yupo sahihi, na ukizingatia ukweli kwamba hata baada ya kustaafu urais na uenyekiti wa CCM bado anayo ile tabia ya kusoma vitabu na kutafuta maarifa mengi.
Nimekumbuka enzi zila za awamu ya kwanza kuelekea ya pili, wakati ule bunge likifanyia shughuli zake pale katika ukumbi wa Karimjee, napowatazama hawa wabunge wa DOT.COM sidhani kama wangekuwa na ubavu wa kukaa katika ukumbi mmoja na wanasiasa wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja kama Marehemu Sebastian Kinyondo na Marehemu Tuntemeke Sanga.
Kizazi cha wabunge walioutumia ukumbi wa Karimjee naweza kusema kwa masikitiko kwamba kinaweza kuwa ni cha mwisho katika umahiri wa ujengaji hoja nzito na uwezo wa ushawishi.
Sio wabunge wa CCM wala sio wale wa upinzani, kwa ujumla taifa linakosa wabunge wengi ambao wanapoongelea leo kitu fulani basi wiki nzima kinakuwa na uzito wa kustahili kuteka mijadala yote ya wanazuoni na wananchi wa kawaida kwenye sehemu za maongezi.
Tunaelekea kubaya ingawa nadhani kwamba hatujatambua. Na ni afadhali kwamba awamu ya tano inapambana kuiokoa thamani ya elimu ili isizidi kushuka, vinginevyo huko mbeleni vituko vitakuwa vingi sana ndani ya ukumbi wa bunge.