Wabunge wa CHADEMA wawasha moto Dodoma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CHADEMA wawasha moto Dodoma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Nov 7, 2011.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa CHADEMA leo wamewasha moto katika mkutano wa hadhara mkoani Dodoma katika uwanja wa Barafu kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge.

  Christowaja kaishukia bodi ya mikopo, asema mabilioni yamefujwa wakati inadai haina fedha za wanafunzi. Kaeleza ufisadi kwenye masharika ya umma.

  Akoonay akaeleza kesi ya baraza la ardhi iliyosababisha wananchi kuvunjiwa Dodoma imetokana na justice fraud kwa kesi kufunguliwa 2011 na kuhukumiwa baada ya siku chache huku kuna kesi ya wananchi mahakama kuu kwenye suala hilo hilo toka 2007. Kasema muswada wa katiba ni mbovu kwa kutoa mamlaka makubwa kwa rais, ataka wananchi kuunga mkono CHADEMA kufanya mambadiliko.

  Nyerere amewaambia Dodoma wanaoikumbatia CCM kuwa chama hicho kina wenyewe, asema yeye amenufaika na CCM kuliko wao lakini ameachana nayo baada ya kutekwa na mafisadi. Awataka wabadilike na kuunga mkono CHADEMA.

  Kiwanga kasema halmashauri zimeoza chini ya CCM, fedha zafujwa na mikataba mibovu yaingiwa. Atoa mifano ya halmashauri zinazoongoza kwa ufisadi.

  Msigwa kasema tatizo la nchi hii ni baba wa nyumba mzembe ndio amefanya nchi iwe ovyo ovyo kila mahali. Amtaka Kikwete kuwajibika ili viongozi wa chini yake nao wawajibike. Amesema haiwezekani tukawa na chama kile kile na viongozi wanaofanya yale yale halafu tukategemea tofauti. Amesema tofauti ya Kikwete na matonya ni kuwa mmoja ni local beggar wakati mwingine ni international begger.

  Wenje kataka wananchi waunge mkono mabadiliko, wote tunakubaliana kupiga ushoga kulinda maadili lakini ameshangaa Waziri Membe kutumia nguvu kubwa kupinga masharti juu ya ushoga badala ya kuongeza Tanzania iweze kujitegemea. Asema mbunge wa Dodoma ni kama hayupo hivyo wananchi wajipange kuziba pengo lake.

  Regia katangaza serikali imefilisika kiuchumi na kiutendaji kwa kiwango cha kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa. Amesema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu ambalo hatua zisipochukuliwa ni hatari kwa taifa.

  Kasulumbayi kasema CCM ni kama kiatu kinachobana, huwezi kusema uendelee kukivaa kwa sababu tu ni chako huku kinakuumiza. Awataka Wananchi wa Dodoma walioumizwa na CCM waachane nayo na kuunga mkono mabadiliko kwa kushirikiana na wasomi wa vyuo vikuu katika mkoa huo.

  Mnyika akasema udhaifu wa Kikwete na serikali yake kwenye kushughulikia migogoro ya ardhi na kupanda kwa gharama za maisha ni tishio kwa amani ya nchi. Amesema CCM imeweka mtego wa muswada mbovu wa katiba ili ukikataliwa wapate kisingizio cha kuchelewesha katiba, ukikubaliwa wapitishe katiba mbovu zaidi na umma ukinikiza katiba bora wameleta muswada unaokinzana na ibara ya 98 ya katiba ili baadaye mchakato mzima upingwe mahakamani.

  Mnyika kataka wananchi wasisubiri 2015 bali waiwajibishe serikali hivi sasa kwa nguvu ya umma; asema wananchi wakianza sasa CCM itaondoka madarakani hata kama katiba itaendelea kuwa mbovu na hatimaye CHADEMA italeta katiba mpya. Kaeleza uhusiano baina ya haki za kikatiba na haki za wananchi kuhusu elimu, ardhi nk na vita dhidi ya ufisadi. Amesema Kikwete alitamka bungeni ukitaka ule lazima uliwe na anaowaita wakumbwa wamempa masharti ya ushoga, hivyo anapaswa atoe kauli ya kuungana na watanzania wengine kumpinga Cameroon.

  Arfi katangaza vita na Pinda kuhusu kuuza au kukodisha ardhi ya watanzania ya kutupa kwa wageni. Kaeleza kusuidio lake la kuwasilisha hoja binafsi kudhibiti uporaji wa ardhi unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Kasisitiza ardhi ndio urithi peke wa watanzania. Ameeleza kwa kina mikataba mibovu ya uuzaji ardhi nchini. Kasema miaka 50 ya Uhuru hakuna cha kujivunia iwapo nchi inazidi kuuzwa wa wageni na kurejea katika ukoloni. Amesema kauli mbiu ya uhuru inapaswa iwe ¬Ďtumethubutu, tumeharibu, tutafakari¬í. Amesema nchi itaendelea iwapo rasilimali za nchi zitatumiwa vizuri kwa manufaa ya umma, asisitiza yuko tayari kufa kutetea ardhi kwa mujibu wa ibara ya 27 ya katiba. Kaahidi CHADEMA imejipanga kujijenga Dodoma kijiji kwa kijiji.

  NB:
  Mkutano ulikuwa na hamasa kubwa, wananchi wamechangishana kwa ajili ya kugharamia kesi ya wananchi wenzao waliovunjiwa nyumba 27. Umati umevutana kugombea nyaraka za katiba na muswada wa katiba kutoka kwa mbunge wa Ubungo. Kamanda Benson Kigaila ameeleza hatua zaidi zitakazochukuliwa na wananchi wa Dodoma kwa nguvu ya umma pamoja na kesi walizobambikiwa mpaka hivi sasa.
   
 2. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Werawera. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Viva chadema!
   
 3. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Muda umewadia... Waanze kutafuta Exile mapema
   
 4. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  vipi mbona hawa wabunge wako dodoma angali wenzao wako nmc arusha/
   
 5. V

  Vitalino mlelwa Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanks ngoma inogile lazma kieleweke wataondoka au wataondolewa wasijali.
   
 6. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Safi sana!

  Saa ya ukombozi imefika...wabongo jiandaeni hakuna awezaye kuzuia upepo huu mkali
   
 7. tama

  tama JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 604
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kumekuuuuuchaaaaa....
   
 8. m

  makaptula Senior Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Safi Saaaaaaaaaaaaaanaaaaa
   
 9. j

  jigoku JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Jamani tunashukuru kwa hili la Dodoma,vipi kuhusu Arusha?hali inaendeleaje huko?bado wako viwanja vya NMC? binafsi sioni sababu ya kuendelea na vikao vya bunge kama serikali haitaki kurusu haki itendeke,ila nawaza tena wasipokuwepo hapo mjengoni hawa mafisadi watapitisha haraka mswaada wa Katiba haraka kwa kura yao ya ndio bila kuwa na pingamizi lolote,wana JF naomba hapa tuchange mawazo,maana ilitakiwa pia kuanza safari ya ukombozi sasa,mimi naamini inawezwkana kwani nchi ilipo sasa iko hatarini sana.kila kukicha ni upuuzi mtupu,,angalia leo tatizo la mafuta limejirudia tena,angalia kuporomoka kwa shilingi dhidi ya dola,angalia jinsi ufisadi ulivyoibuliwa na kamati za bunge lakini mwisho wa siku itaishia hivyo hivyo.mfano wa karibu ni sakata la UDA.sasa hivi kimya kana kwamba hakukuwa na kitu,ndo maana napendekeza ukombozi uanzie ARusha,tuunge mkono.
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  watatoka tu watake wasitake! pambaaaaaf hawa
   
 11. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  wanatwanga kote kote,from north to south,west to east.unataka waende wote arusha magamba wawalipue wasingizie al shabaab.
   
 12. ZALEOLEO

  ZALEOLEO Senior Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wapi picha?
   
 13. JOASH MUSSA

  JOASH MUSSA JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Yaani mwanzo mwisho, wanaoiombea chadema mabaya wazidi kuomba sababu wanaomba kwa shetani na shetani akijaribu anakutana na nguvu ya MUNGU anashindwa na zaidi ya kushindwa,. Viva CHADEMA huku Arusha kule Dodoma pale Mwanza na Nchi nzima waitambue CHADEMA waitambue haki yao kama Watanzania
   
Loading...