figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Katika hali ya kushangaza, Wabunge wa CCM wamempongeza naibu spika kwa kitendo chake cha kuwakomoa na kuwabagua wapinzani. Kitendo cha kuwapa adhabu wapinzani na kuwanyima Uhuru wa kuchangia bungeni hasa kupangiwa waseme nini, Kimeibua vifijo na nderemo kwa wabunge wa CCM. Hata wale Wabunge waliokuwa hawaongei, Sasa wanaongea kumpongeza Naibu Spika.
Baadhi wamekiri kwamba, Wabunge wa Upinzani wana akili sana, wanajua mambo mengi ambayo walikuwa wakiongea na kuwafanya CCM yote ionekane si chochote. Hotuba ya upinzani ya mambo ya ndani, ilihaririwa na Uongozi wa Bunge kwa Shinikizo la CCM ili isiumbue Uongozi wa awamu ya tano, jambo lilifanya Godbless Lema kuisusia kuisoma.
Wabunge wa CCM wanasema wamekuwa na amani Bungeni, Wanasema sasa wanafanya watakalo hata wakikiuka kanuni hakuna anayeomba Muongozo wala kuhoji.
Wamemshauri Naibu Spika kuendelea hivo hivo, Mheshimiwa naibu Spika, natamani kuona hawa wapinzani ikiwezekana Tuwafukuze kabisa wasirudi Bungeni. Fanya uwezavyo kuwanyosha.
Na mbunge anayetuhumiwa kwa Ufisadi na aliyekaliwa Kooni na Upinzani Andrew Chenge, Kasema "Kwa mujibu wa katiba sheria na kanuni za bunge akidi ya Maamuzi tunayo. Meshimiwa naibu SpikaMimi sipo nyuma yako, nipo Bega kwa bega na wewe". Hii ina maanisha hata wakivuruga hakuna wa kuwauliza kwani Wabaya wanao waharibia Madili hawapo na Bunge halipo live hivo wataruhusu kurushwa kile wanachotaka ilimradi kuilinda CCM.
Kuthibitisha haya nliyosema, Nitaweka video hapa, nmeitoa Youtube ya JamiiForums kama Ushahidi tosha wa haya.
Tanzania bado tuna safari ndefu.
R.I.P Alfonce Mawazo, R.I.P Mwalimu Kidole, R.I.P Msafiri Mbwambo, R.I.P Dennis Kasanga . Hawa ni Wahanga waliopoteza Maisha wakitetea mabadiliko ya kweli ndani ya Nchi yetu.
Sasa ni wakati Naibu Spika awe Mbunge wa Kuchaguliwa sio wa kuteuliwa sababu Rais anapojiteulia Kiongozi wa Bunge anayemtaka, mjue Bunge linafanywa kibogoyo