Wabunge wa CCM wajadili bajeti ya upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM wajadili bajeti ya upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Listener, Jul 4, 2012.

 1. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Natazama Bunge live lakini cha ajabu naona kama wabunge wa CCM wanaijadili tena kwa kina bajeti ya upinzani. Kimsingi nadhani walitakiwa kuiboresha bajeti ya serikali yao huku wakiuchukua ushauri (hasa ule wanaouona kwao unafaa) toka katika bajeti ya upinzani.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Wapinzani wanatoa maoni, lakini hoja bajeti ya serikali. Wabunge wote wanatakiwa wajadili hiyo hoja yaani bajeti ya serikali, sasa kama wanajadili maoni ya upinzani hili ni janga lingine la kitaifa. Kwa bahati mbaya anayeongoza kikao cha bunge ama kwa makusudi au kutojua ameamua kuacha kuacha watu wajadili maoni na sio 'hoja'.

  Na kwa msingi huo hakuna haja ya serikali kupeleka hoja bungeni maana wabunge hawachangii/hawachambui hoja. Waachwe wapinzani wapeleke maoni since wabunge wa CCM wako bungeni kujadili maoni ya wapinzani!
   
 3. cooper

  cooper JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 394
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Siyo bajeti tu hata sera na ilani yao hawaizingatii tena wanasubiri waone CDM wanafanya nini au wanasema nini, halafu wao wafuate au wajadili. CCM ni chama tawal kinadharia ila CDM ni chama tawala in action maana ilani yao, bajeti na hotuba zao ndo zinaongoza kujadiliwa na CCM na vyama vingine badala zile za CCM, sasa nani anatawala hapo??
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hili ndio tatizo la kuweka maslahi ya chama mbele, CCM ni janga la kitaifa na wabunge wake ni virus wanaitafuta Tanzania, mimi nimeacha hata kutazama bunge maana linaendeshwa kitoto sana na wenyeviti na spika dahifu toka chama cha kipuuzi kinachoongozwa na mwenyekiti dhaifu!
   
 5. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  typical defensive mechanism which is wrong
   
Loading...