Wabunge wa CCM na upitishaji mikataba kuwakomoa wapinzani ni janga la taifa

Robinhomtoto

JF-Expert Member
May 17, 2017
238
244
Watanzania wenzangu mtakubaliana nami mateso anayoyapasa Mh. Rais Magufuli ni tabia ya Viongozi wa CCM Kwa kushikiana na Wabunge wa CCM kukubali kupitisha Mikataba iliyoandaliwa Kimkakata ili kuwanufaisha wachache ambao Leo Rais anahangaika nao. Wapinzani wamekuwa wakipinga sana lakini viongozi wa CCM Na Serikali wamekuwa wanawaagiza Wabunge wake wapitishishe mikataba. Mh. Rais kuna mikataba mingi ambayo Wabunge wa CCM walitumia uwingi wao kuipitisha. Baadhi ya mikataba ni kama ya;
1.Gesi
2. Madini
3.Mlimani city
4.Uwekezaji Oysterbay Polisi
5.Lugumi
6.Loliondo kitalu cha mfalme

N.k.
Tunakuomba itisha mikataba hiyo ni michafu.
 
Mkuu USIMTENGE Rais na uvundo uliofanyika kwenye Mikataba ya Madini..

Amekuwa Mbunge kwa karibu Miaka 20 na Waziri kwa karibu Miaka 15..

Haya madudu ya kwenye mikataba yalivyokuwa yanapitishwa kwenye cabinet alikuwepo..

Mle bungeni amegonga meza sana tu hii mikataba ilivyokuwa inapitishwa na wakina Lissu walivyokuwa wanapiga kelele.

He is part and parcel kwa madudu yote yaliyofanyika.

Don't sympathise na sura anayokuonyesha hivi sasa.
 
Ungesema walipitisha mikataba awamu zilizopita kujipatie mafedha...ungegusa haswa.

Na wa upinzani wengine walihusika, ingawa walipiga kelele kujisafisha. Ila hakuna linalojificha chini ya jua...

Mkulu kagusia jana pia hayo
 
Wana kazi ya kupiga meza kama mbweha pale bungeni ila matokeo ndio Haya wa nakuja kuwaambia wananchi tuungane. Mi CCM ni mijitu ya hovyo sana. Nikikumbuka ile sheria ya uchimbaji wa gesi ilivyopitishwa kwa hati ya dharura sina hamu.watu tulipiga kelele wakatuona wapuuzi. Tusubiri hata haya ya gesi yatalipuka tu.
 
Hata sheria ya HESLB kukata asilimia 15 kwenye mishahara ya wakopaji wamepitisha hao hao wazee wa ndiyooooo. They are the disaster of this nation.
 
Ungesema walipitisha mikataba awamu zilizopita kujipatie mafedha...ungegusa haswa.

Na wa upinzani wengine walihusika, ingawa walipiga kelele kujisafisha. Ila hakuna linalojificha chini ya jua...

Mkulu kagusia jana pia hayo
Si kweli kwamba wapinzani walipitisha huo ni uongo mtupu
 
Wana kazi ya kupiga meza kama mbweha pale bungeni ila matokeo ndio Haya wa nakuja kuwaambia wananchi tuungane. Mi CCM ni mijitu ya hovyo sana. Nikikumbuka ile sheria ya uchimbaji wa gesi ilivyopitishwa kwa hati ya dharura sina hamu.watu tulipiga kelele wakatuona wapuuzi. Tusubiri hata haya ya gesi yatalipuka tu.
Huko ndiko kwenye hatari zaidi
 
Mkuu USIMTENGE Rais na uvundo uliofanyika kwenye Mikataba ya Madini..

Amekuwa Mbunge kwa karibu Miaka 20 na Waziri kwa karibu Miaka 15..

Haya madudu ya kwenye mikataba yalivyokuwa yanapitishwa kwenye cabinet alikuwepo..

Mle bungeni amegonga meza sana tu hii mikataba ilivyokuwa inapitishwa na wakina Lissu walivyokuwa wanapiga kelele.

He is part and parcel kwa madudu yote yaliyofanyika.

Don't sympathise na sura anayokuonyesha hivi sasa.

Kuna crip moja inatembea ikimuonyesha mkulu akijadili mikataba ya madini, akiwa nahisi na waheshimiwa wenzake kipindi hichooooo, aliliona na lilikuwa linamkera, ''chukua form'' quoted
 
Huwa inapitishwa wapi Mkuu? Tusaidie.

Sheria mbovu ambazo ndiyo zinazaa hii mikataba ya kifisadi ndiyo zinapitishwa bungeni na wabunge wa CCM ndiyo vinara wa kupitisha sheria hizi kwa makusudi kabisa ili kuwakomoa wapinzani. CCM ni adui wa ustawi wa taifa letu.
 
Wana kazi ya kupiga meza kama mbweha pale bungeni ila matokeo ndio Haya wa nakuja kuwaambia wananchi tuungane. Mi CCM ni mijitu ya hovyo sana. Nikikumbuka ile sheria ya uchimbaji wa gesi ilivyopitishwa kwa hati ya dharura sina hamu.watu tulipiga kelele wakatuona wapuuzi. Tusubiri hata haya ya gesi yatalipuka tu.
Na waziri alikuwa Muhongo!! Sijawahi kumwamini profesa huyu mwenye dharau kuliko wasomi wote Tanzania.
 
Mikataba yote baraza la mawazi wote chini ya mwenyekiti wao rais huipitia mikataba na kuridhia lkn bungeni wapinzani wakitaka mikataba ili waipitie lkn wabunge wa ccm hupinga kwa shinikizo la rais ambaye ni mwenyekiti wa chama chao ,huyu jamaa alikuwepo kama waziri utasemaje kuwa hayumo?
Huyu jamaa wala asituzuge mkuu, YUMO!
 
Ungesema walipitisha mikataba awamu zilizopita kujipatie mafedha...ungegusa haswa.

Na wa upinzani wengine walihusika, ingawa walipiga kelele kujisafisha. Ila hakuna linalojificha chini ya jua...

Mkulu kagusia jana pia hayo

Rais kapitisha hiyo mikataba akiwa waziri na mbunge. Yeye kachangia Tanzania kuibiwa.
 
Back
Top Bottom