Wabunge UKAWA watoka bungeni wakiwa na mabango yenye ujumbe kwa Rais Magufuli na Dr. Tulia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Wabunge wa UKAWA watoka nje ya bunge wakiwa wametinga mavazi meusi na wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbali mbali.

Baadhi ya Mabango yalikuwa yanasomeka...
  • Magufuli, acha kutawala Zanzibar kijeshi
  • Magufuli, nchi hii siyo mali yako binafsi
  • JPM & Tulia liacheni bunge lifanye kazi
  • Hatuwezi kuongozwa kwa kauli za mtu mmoja
  • Bunge ni chombo cha wananchi, kiachwe kifanye kazi yake
  • Tulia, Bunge siyo kampuni binafsi
  • Magufuli: Siasa ni maisha, huwezi kuyasimamisha
  • Kama mko sahihi, woga wa nini?

VIDEO


13557873_10154338848014345_8967128156740305770_n.jpg

Screenshot from 2016-06-30 10:41:32.png
 
tuna muhitaji sana Mungu aingilie kati,maana nchi hii nusu ya wakuu wa wilaya ni wanajeshi,hapo demokrasia inapitia wapi,dada Tulia muheshimiwa hata ile hekima kidogo tu ya uongozi hana na yeye,kwa kuwa alibebwa na yeye anaibeba serikalo
 
tatizo siasa za Afrika zimejaa sana chuki na visasi na kulindana watu wanamtaja Mungu kwenye midomo ila mioyo yao iko mbali sana ndio maana wapo tayari kuua ili wao watawale
naibu katibu mkuu wa vijana ccm UVCCM ndugu SHAKA SHAKA anafanya mikutano anazunguka tu alianzia Tanga,ARUSHA sasa yupo Iringa azuiliwi tunaitaji sana hekima ya uongozi wala usifanye haya kwa kuwa wewe ni bunge na serikali
 
Mbaya zaidi na wakawa CCM hawatumii akili kufikiria, maadam wanaona wanaonyanyaswa ni wapinzani wao furaha tele hawafikirii mustakabali wa taifa letu pendwa
 
Back
Top Bottom