Wabunge Uingereza washinikiza Tanzania inyimwe Sh212 milioni

Mugo"The Great"

JF-Expert Member
Oct 7, 2007
262
25
Na Jonas Songora

Source: http://www.mwananchi.co.tz

SERIKALI ya Uingereza inaweza kusitisha kutoa dola za Marekani 212 milioni ilizoahidi katika bajeti ya mwaka 2007/2008 kufuatia kuwepo kwa tuhuma za kunyanyaswa wawekezaji wa nchi hiyo walioko nchini.

Hatua hiyo imekuja baaada ya mbunge kutoka chama cha Conservative, Roger Gale kuwakilisha hoja katika bunge la nchi hiyo, akidai kuwa wawekezaji wawili wa Uingereza wanafanyiwa hila kunyang?anywa mashamba yao na mfanyabiashara wa Kitanzania, Benjamin Mengi ambaye ni mdogo wa mmiliki wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi.


Wawekezaji hao Stewart Middleton na Sarah Hermitage wamekuwa katika mzozo wa kisheria dhidi ya Mengi tangu mwaka 2004 walipotiliana saini kukodisha mashamba ya Silverdale na Mbono, mkataba ambao hadi sasa haujasajiliwa huku wawekezaji hao wakikamatwa na polisi mara kwa mara hali ambayo imetafsiriwa kama ni unyanyasaji kwa wawekezaji wa kigeni.


Alidai pia kuwa wawekezaji hao waliwahi kushitakiwa kufuatia habari zilizoandikwa magazetini kuhusu mashamba hayo, ambapo iliamriwa kuwa Mengi ambaye ni mmiliki wa mahoteli alipwe dola za Marekani 100,000. Habari hiyo iliripotiwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa.


Akizungumza na gazeti la EastAfrican kwa njia ya simu,jumatano wiki iliyopita, Gale alidai kuwa kushindwa kwa serikali kusuluhisha tatizo hilo lilidumu kwa muda mrefu, kumepunguza imani ya wawekezaji wa kigeni.


Mbunge huyo alitoa pendekezo kuwa Uingereza isitishe kutoa kiasi hicho cha fedha, kutokana na alichodai kuwa ni vitendo visivyoridhisha dhidi ya wawekezaji hao wanaofanya biashara zao mjini Moshi.


Katika hatua nyingine, mbunge huyo alidai kuwa pamoja na nchi yake kusifia Tanzania kama moja ya nchi inayopiga hatua kubwa kiuchumi, bado hajaridhishwa na namna serikali inavyopambana na rushwa na kuongeza kuwa serikali ya Uingereza imeshindwa kuibana Tanzania hasa katika kuwathamini wawekezaji wa kigeni.


Hata hivyo msimamo huo wa Gale bado haujajadiliwa katika vikao vya ndani na kuwa hadi sasa hakuna mpango wowote uliopitishwa kuhusu kusitisha kutoa fedha hizo zilizoaidiwa na Uingereza.


Akizungumzia kuhusu sakata hilo, John Bradshaw ambaye ni Afisa anayeshughulikia Siasa na Mawasiliano katika ubalozi wa Uingereza nchini, alidai kuwa ingawa kuna msukumo mkubwa kutoka kwa wanasiasa wa nchi hiyo kutaka kusitishwa kutolewa kwa fedha hizo, bado serikali haijaamua kuchukua hatua yoyote.


Aliongeza kuwa ofisi yao imekuwa karibu na serikali ya Tanzania katika kusuluhisha migogoro inayohusu sekta ya uwekezaji na kuwa wanaamini kuwa serikali ya Tanzania itashughulikia suala hilo na kutoa uamuzi sahihi.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Patrick Mombo, alipohojiwa na gazeti hilo alieleza kuwa Tanzania inaamini katika utawala bora, na kuwa serikali inaamini kuwa suala hilo litashughulikiwa na mahakama bila kuingiliwa.


Makampuni ya Kiingereza yamewekeza kiasi cha Dola za Marekani 322 milioni katika sekta ya kilimo na utalii katika miaka 11 ilityopita, ambapo inakadiriwa kuwa Waingereza 6,000 wanaishi nchini Tanzania.
 
Ndiyo maana vongozi wetu wanashinikizwa na kukubali mikataba kama wa City water, Rada. Miradi ambayo inapelekea Tanzania kulipa maradufu ya kile walichotukopa au kutoa misaada.
 
Back
Top Bottom