Wabunge na Watu wenye Ulemavu wapiga Kambi Serengeti Kutalii

Jun 4, 2019
14
23
Chama cha wabunge wenye ulemavu wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakiongizwa na mwenyekiti wake mheshimiwa Riziki Lulida na katibu kamati Mbunge mh Amina mollely Leo wanaendelea na Utalii wa kuzungukia vivutio vya utalii vilivyopo nchini katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiamabatana na viongozi wa vyama vya walemavu na baadhi ya watu wenye ulemavu kutoka Tanzanania bara na visiwani.

Mbunge Mh,Riziki Lulida ameeleza kufurahishwa sana kwa mapokezi mazuri na uhifadhi mzuri wa hifadhi ya Serengeti. Kupiti kundi la watu wenye ulemavu ambalo limefanya utalii katika hifadhi ya Serengeti anaamini kuwa itakua chachu ya kuongeza idadi ya watalii wandani na kuyataka makundi mengine pia kuanzakufanya utalii wandani hasa wakuu wa mikoa wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es alaam Poul Makonda .

Nae Mbunge Amina Mollel ameeleza kuwa huo ni mwanzo tu kwa watu wenye ulemavu kuanza kufanya utalii na wao watakua mabalozi wazuri wa kuwahamasisha Watanzania kutembelea vivutio vyetu vya ndani na Kushukuru Bunge pamoja na Wiraza ya Mali asili na utalii kuwezesha safari ya watu wenye ulemavu kutembelea vivutio vya utalii.

Lengo likiwa ni kuhamasisha watu wenye ulemavu kupewa nafasi na haki ya kufanya utalii wa ndani ikiwa ni moja kati ya haki za binadamu.

Msimamizi wa Hifadhi ya Serengeti amewapongeza wabunge wenye ulemavu wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha wabunge wenye ulemavu Mheshimiwa Riziki Lulida na Katibu wake Mheshimiwa Amina Mollel kwa jinsi wanavyo hamasisha utalii nchini.

Wabunge hao na Watu wengine walioambatana nao wazunguka ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa muda was Siku tatu kabla ya kwenda kwenye hifadhi nyingine.
 
Back
Top Bottom