Wabunge mnakwama wapi??

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
663
195
Ndugu zetu Wabunge na Spika akiwemo,mbona mnaonekana kupatwa na kigugumizi kutoa maamuzi ya mjadala wa ESCROW? Hembu angalie facts hizi tatu hapa chini;

1. Nyote mmekubali kuwa Kamati ya PAC ni wawakilishi wa Bunge Zima,

2. Nyote mmekubali kuwa yaliyoletwa na PAC ni mapendekezo yanayowakilisha Bunge,

3. Nyote mmekubali kuwa kuna tatizo la ubadhirifu, wizi na ufisadi wa mali ya Umma,

Sasa vipi mnashindwa kufikia maamuzi? Kutoa mapendekezo au kushauri kuwa viongozi Fulani (Hata kama ni Executives)kuwajibika au kuachia ngazi SI KUINGILIA MAMLAKA NYINGINE ZA UTEUZI. KWASABABU MAMLAKA HIZO ZINA UWEZO WA KUPOKEA NA KUUFANYIA KAZI USHAURI HUO AU LA.


Mwisho, Nanyie Mawaziri (Wabunge), fanyeni kazi za BUNGE mnapokuwa Bungeni, acheni kabisa kuleta tafsiri za mikataba yenu ya AJIRA ndani ya BUNGE - Ni upuuzi na umangimeza.

Wabunge..toeni pendekezo lolote lile kwa Serikali kwa kadiri mtakavyo jiridhisha. PENDEKEZO AU USHAURI SI KUINGILIA KAZI ZA MAMLAKA NYINGINE.

WANANCHI TUNAWANGALIA TU NA OLE WENU!
 

fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,700
2,000
Kinana na nape wakija kijijini kwetu lazi Tuwafukuze na mawe wanatudanganya hawakumbatiyi wezi kumbe wana tudanganya wanajidai kushiriki kazi za kijamii kumbe wanatuona mafala me ninawatahadharisha wasije kijijini kwetu tushachoka usani wao ole wao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom