Wabunge, Masaburi yaibuka tena upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge, Masaburi yaibuka tena upya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Feb 29, 2012.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MSUGUANO kati ya wabunge wa Dar es Salaam na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, umeibuka upya baada ya wabunge hao kusema wamepata nyaraka mpya za tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria katika suala la ubinafsishaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

  Kamati ya Wabunge hao waliokutana jana kwa dharura kujadili nyaraka hizo, imepanga kutoa taarifa kuhusu uamuzi na maazimio ya kikao na hatua ambazo watachukua leo.

  Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Kamati hiyo, John Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo, ilisema walikutana kwa dharura chini ya uenyekiti wa Abbas Mtemvu, Mbunge wa Temeke.

  “Wabunge wa Dar es Salaam wanaendelea na kikao cha kupitia nyaraka zote na kufanya uamuzi wa hatua za kuchukua na taarifa juu ya hatua hizo itatolewa kwa umma baada ya kumalizika kwa mkutano unaoendelea,” Mnyika alisema jana.

  Wabunge walioshiriki mkutano huo ni Mtemvu (Mwenyekiti), Mnyika (Katibu), Halima Mdee, Mussa Zungu, Idd Azzan, Neema Mgaya Hamid, Suzan Lyimo, Zarina Madabida, Faustine Ndugulile, Phillipa Mturano na Eugene Mwaiposa.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyaraka ambazo Kamati hiyo imepokea ni pamoja na barua ya UDA ya Januari 26 yenye kumbukumbu namba CBA/Reg/01/UDA ambayo inataka dola za Marekani 133,125 zitolewe kutoka akaunti ya UDA ambayo ilishaagizwa awali fedha zisitoke kinyemela.

  Waraka mwingine uliojadiliwa ni wa kikao kinachodaiwa kuwa cha wanahisa wa UDA cha Februari 13 ambacho inadaiwa kilifanywa na Meya Masaburi akiwa Mwenyekiti pamoja na Robert Kisena ambaye anatambulishwa kwenye muhtasari huo kama Mwenyekiti Mtendaji wa UDA na Katibu wa Bodi ya UDA.

  Wabunge hao wanakishutumu kikao hicho pamoja na mambo mengine, kuwa kimefanya uamuzi haramu wa kubadili waweka saini katika akaunti ya UDA iliyozuiwa kwa lengo la kuwezesha fedha kutolewa kinyemela na Simon Group.

  Wanadai kwamba Meya Masaburi kwa kushirikiana na Simon Group wameshirikiana kwa mara nyingine kukiuka uamuzi wa mamlaka mbalimbali na sheria na kanuni.

  Kwa mujibu wa wabunge hao, Januari 9, Baraza la Madiwani wa Jiji lilipitisha maazimio kuhusu mgogoro unaoendelea katika UDA mojawapo ikiwa ni pamoja na kufanyika uchunguzi wa kughushiwa kwa barua iliyomwelekeza Simon Group Limited kulipa awamu ya pili ya malipo kwa kutumia akaunti ya Mwenyekiti wa Bodi ya UDA na kwamba suala lipelekwe kwenye vyombo husika kwa ajili ya kubaini ukweli na hatua kali zichukuliwe dhidi ya aliyeghushi.

  Taarifa hiyo iliongeza, kwamba Baraza la Madiwani liliazimia kuwa uthamini wa hisa uliotumiwa katika kumwuzia hisa Simon Group, haukuwa halisi hivyo hisa zote zifanyiwe uthamini upya ili ziuzwe kwa bei inayostahili.

  Ilielezwa pia kuwa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, liliazimia kuwa Simon Group asitambuliwe kama mwanahisa mkuu katika UDA na hivyo kuazimia kuwa iteuliwe Bodi ya muda itakayosimamia utekelezaji wa mkataba kati ya UDA na Simon Group.

  Taarifa iliendelea kueleza, kwamba Baraza lilimteua Mwaiposa kuwa mjumbe wa Bodi hiyo akiwakilisha Halmashauri ya Jiji na Meya Masaburi kinyume na maazimio ya mkutano wa Januari 9, akashiriki kikao cha Bodi ya UDA Februari 13 na kudaiwa kufanya uamuzi wa kubadili waweka saini wa akaunti ili fedha zihamishwe.

  Agosti 4 mwaka jana, wabunge wa Dar es Salaam walikutana Dodoma na kutoa tamko la kueleza kile walichosema ni kusikitishwa na tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi katika mchakato wa ubinafsishaji wa UDA.

  Tuhuma za wabunge hao kwa Masaburi ziliibuka mwaka jana ambapo Meya huyo alilazimika kutumia kauli kali baada ya wabunge hao kumtaka ajiuzulu kupisha uchunguzi akisema wabunge hao baadhi yao wanashindwa kufikiri kwa kutumia vichwa na badala yake wanatumia makalio.

 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Nilipoona masaburi nikafikiri masaburi kweli.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini hawa wabunge wasitoe msimamo wa kupinga UDA isibinafsishwe?
   
 4. J

  John W. Mlacha Verified User

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  kwani huyo masaburi ni feki?
   
 5. K

  Kidumbasi Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2][​IMG] Wabunge, Masaburi yaibuka tena upya[/h]
  MSUGUANO kati ya wabunge wa Dar es Salaam na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, umeibuka upya baada ya wabunge hao kusema wamepata nyaraka mpya za tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria katika suala la ubinafsishaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

  Kamati ya Wabunge hao waliokutana jana kwa dharura kujadili nyaraka hizo, imepanga kutoa taarifa kuhusu uamuzi na maazimio ya kikao na hatua ambazo watachukua leo.

  Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Kamati hiyo, John Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo, ilisema walikutana kwa dharura chini ya uenyekiti wa Abbas Mtemvu, Mbunge wa Temeke.

  “Wabunge wa Dar es Salaam wanaendelea na kikao cha kupitia nyaraka zote na kufanya uamuzi wa hatua za kuchukua na taarifa juu ya hatua hizo itatolewa kwa umma baada ya kumalizika kwa mkutano unaoendelea,” Mnyika alisema jana.

  Wabunge walioshiriki mkutano huo ni Mtemvu (Mwenyekiti), Mnyika (Katibu), Halima Mdee, Mussa Zungu, Idd Azzan, Neema Mgaya Hamid, Suzan Lyimo, Zarina Madabida, Faustine Ndugulile, Phillipa Mturano na Eugene Mwaiposa.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nyaraka ambazo Kamati hiyo imepokea ni pamoja na barua ya UDA ya Januari 26 yenye kumbukumbu namba CBA/Reg/01/UDA ambayo inataka dola za Marekani 133,125 zitolewe kutoka akaunti ya UDA ambayo ilishaagizwa awali fedha zisitoke kinyemela.

  Waraka mwingine uliojadiliwa ni wa kikao kinachodaiwa kuwa cha wanahisa wa UDA cha Februari 13 ambacho inadaiwa kilifanywa na Meya Masaburi akiwa Mwenyekiti pamoja na Robert Kisena ambaye anatambulishwa kwenye muhtasari huo kama Mwenyekiti Mtendaji wa UDA na Katibu wa Bodi ya UDA.

  Wabunge hao wanakishutumu kikao hicho pamoja na mambo mengine, kuwa kimefanya uamuzi haramu wa kubadili waweka saini katika akaunti ya UDA iliyozuiwa kwa lengo la kuwezesha fedha kutolewa kinyemela na Simon Group.

  Wanadai kwamba Meya Masaburi kwa kushirikiana na Simon Group wameshirikiana kwa mara nyingine kukiuka uamuzi wa mamlaka mbalimbali na sheria na kanuni.

  Kwa mujibu wa wabunge hao, Januari 9, Baraza la Madiwani wa Jiji lilipitisha maazimio kuhusu mgogoro unaoendelea katika UDA mojawapo ikiwa ni pamoja na kufanyika uchunguzi wa kughushiwa kwa barua iliyomwelekeza Simon Group Limited kulipa awamu ya pili ya malipo kwa kutumia akaunti ya Mwenyekiti wa Bodi ya UDA na kwamba suala lipelekwe kwenye vyombo husika kwa ajili ya kubaini ukweli na hatua kali zichukuliwe dhidi ya aliyeghushi.

  Taarifa hiyo iliongeza, kwamba Baraza la Madiwani liliazimia kuwa uthamini wa hisa uliotumiwa katika kumwuzia hisa Simon Group, haukuwa halisi hivyo hisa zote zifanyiwe uthamini upya ili ziuzwe kwa bei inayostahili.

  Ilielezwa pia kuwa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, liliazimia kuwa Simon Group asitambuliwe kama mwanahisa mkuu katika UDA na hivyo kuazimia kuwa iteuliwe Bodi ya muda itakayosimamia utekelezaji wa mkataba kati ya UDA na Simon Group.

  Taarifa iliendelea kueleza, kwamba Baraza lilimteua Mwaiposa kuwa mjumbe wa Bodi hiyo akiwakilisha Halmashauri ya Jiji na Meya Masaburi kinyume na maazimio ya mkutano wa Januari 9, akashiriki kikao cha Bodi ya UDA Februari 13 na kudaiwa kufanya uamuzi wa kubadili waweka saini wa akaunti ili fedha zihamishwe.

  Agosti 4 mwaka jana, wabunge wa Dar es Salaam walikutana Dodoma na kutoa tamko la kueleza kile walichosema ni kusikitishwa na tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi katika mchakato wa ubinafsishaji wa UDA.

  Tuhuma za wabunge hao kwa Masaburi ziliibuka mwaka jana ambapo Meya huyo alilazimika kutumia kauli kali baada ya wabunge hao kumtaka ajiuzulu kupisha uchunguzi akisema wabunge hao baadhi yao wanashindwa kufikiri kwa kutumia vichwa na badala yake wanatumia makalio.

  Nashangazwa sana na hao Wabunge, kila siku vikao na kushutumu Masaburi.
  kiseni wembe mdundo, tata 30 kishaongeza, yard kishaikodsha,menejimenti ni ya kwake, madereva na watumishi wapo chini ya mamlaka yake.
  Wao wanaendelea na vikao, mpaka lini ?
  Waache siasa za magazetini, wafanye kweli.​
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu meya Masaburu ni fisadi siku nyingi lakini alikuwa anabebwa sana na Makamba; na hivi sasa juu ya kushindwa kuliendeleza jiji na matatizo yake lukuki inasemekana anataka tena ubunge wa Afrika Mashariki alioupata hapo awali kwa kuhonga fedha nyingi sana!! Nitashangaa kama ccm inayosisitiza wanachama wake kutokujilimbikizia madaraka watampitisha na wabunge aliowatukana kuwa wanafikiri kwa kutulia MAKALIO watakuwa wamesahau na kumchagua tena!!
   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ulidhani kuna Mtu kachojoa nini!
   
 8. K

  Kidumbasi Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heee....!!!!! Anautaka Ubunge wa Afrika Mashariki ?
  Atakubali kupokea kura zinazotoka kwa Watu wanaofikiria kwa kutumia MAKALIO (mkunduni) ?
   
Loading...