Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Leo Bungeni Dodoma wabunge wa pande zote bila ya kujali itikadi za vyama vyao wameungana na kutoka nje ya Bunge mara baada ya Naibu Spika Dr. Tulia AKson Mwansasu kukataa bunge lisijadili hoja ya dharura kuhusu kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi wa program maalumu ya wanafunzi wa stashahada ya uwalimu katika masomo ya sayansi. Muungano huu ni jambo jema ana la kupongezwa.
Lakini kuungana huku kwa ghafla kumechochewa na ukweli kwamba kuna wabunge, mawaziri na watumishi wa umma wengi wenye 'VYETI FEKI' na wameiona hatari ya mkakati wa kukagua vyeti feki. Na mtu ambaye ameonekana ni mwiba kwao ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ambaye amelishikia bango suala la vyeti feki, sasa kuna mkakati umesukwa ili kumkwamisha waziri huyu kwa kumuonyesha ni mtu asiye makini hatimaye aondolewe serikalini na wale wenye vyeti feki waendelee kudunda tu Bungeni na kwenye Sekta Nyeti za Serikali. Wabunge wanataka hoja ijadiliwe na waziri aonekane ni mzembe, hivyo aondoe dhamira yake juu ya Vyeti Feki.
Pia juzi waziri huyu alikuwa mtegoni kuingia kwenye kashfa ya kutenga bilioni 8 kwaajili ya kujenga na kukarabati ofisi za Wizara, lakini hoja ilikuwa inajengwa ili aonekane anataka kujenga ofisi yake binafsi.
Ikumbukwe jana moja ya stori kubwa ni kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Sakata la vyeti feki lawa gumzo kwa wabunge’. Gazeti hilo limeripoti kuwa siku moja baada ya serikali kutangaza kuwa itachunguza uhalali wa vyeti vya watumishi wa umma wakiwamo wabunge, uongozi wa Bunge umesema hauna kipingamizi kuhusu uamuzi huo.
Katika mahojiano na Nipashe Naibu Spika wa Bunge, Tulia Akson alisema uongozi wa Bunge hauna kipingamizi juu ya kukagua vyeti vya elimu vya wabunge ingawa bado haujapewa barua rasmi kuhusu uamuuzi huo.
Rejea thread hii iliyowahi kuletwa hapa JF:
Vyeti Feki vitampa Magufuli maadui wengi kuliko hata "Ufisadi''
Kumbuka wabunge wanatumika kwa mambo mengi kila jambo linalobana maslahi yao basi huwa na kawaida ya kuwa na ummoja mfano hakuna siku wabunge wamekuwa tofauti juu ya mishahara na posho zao. Vyeti feki vinawaumiza kwa namna moja.