Wabunge Kununuliwa na vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Kununuliwa na vyama vya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Jan 11, 2012.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Katika mabadiliko anayokusudia Tendwa kuyafanya kwa kushirikiana na serikali itapelekea biashara ya kuuza na kununua Wabunge na kama biashara hii ikiaanza basi CCM ndio wataonufaika kwa kiwango kikubwa.

  Kwa sheria wanayoandaa sasa na kutaka kuipeleka bungeni Kama CCM wakitaka Kumnunua Mbunge mfano Mnyika wao watampelekea watu wa kumshawishi kwa fedha nae atataja kiasi anachotaka kwa kunuliwa au kusajiliwa na CCM na wakikubaliana inakuwa tayari zoezi limekamilika kwani baada ya malipo kufanyika yeye atatupa kadi ya Chadema na kuchukua kadi ya CCM na hapo CCM watakuwa wameongeza(wamasajili ) mbunge na Chadema watakuwa wamepoteza mbunge.

  Kwa mazingira kama haya biashara ya Wabunge kunuliwa na kuuzwa itakuwa na madhara makubwa siku za mbeleni katika kukuza demokrasia
   
 2. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wapi ishafanyika hii,mkuu? Maana wakubwa hupenda kutoa mifano nje ya nchi yetu.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  malawi imeshafanyika rais Bingwa mutharika alijiondoa kutoka katika chama tawala na kuunda chama kipya kisha kusajili wabunge katika chama kipya na kuendelea kuwa rais wa malawi na chama kipya alichokisajili kikanunua wabunge na kikawa ndio chama kipya tawala pasipo na uchaguzi
   
 4. k

  king11 JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ccm wanaweza kumnunua Dr slaa na Mboe
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Bingu aliweza kuhama chama kwa sababu Katiba ya Malawi hailazimishi mgombea wa nafasi ya urais kuwa sponsored na chama. Alivyoona hiyo loophole na baada ya kuona hakubalini na sera za chama chake akajitoa na kuanzisha chama, bila kuathiri nafasi yake ya uraisi.
   
 6. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mabadiliko nchini Kenya yaliwzekana baada ya wabunge waliokuwa wa KANU (chama tawala) kuhama na kuingia upinzania na bado wakaendeleakuwa wabunge, kwa maana ingine walihama mabenchi tuu. Kumbuka hii sheria ya mbunge kupoteza ubunge akifukuzwa na chama iliungwa mhsusi na CCM enzi za Nyerer ilikuwadhibiti wabunge wakitumikia chama badla ya kutumika wananchi, japokuwa sasa hivi inatumiwa sana na uoinzani. Ndio maana ni vyema kufuta shria zote kandamizi hata kabla ya walio wapinzani loe hawajainia mafarakani kwani uzoefu unaonyesha mtu akiingia madarakani na kurithi sheria kandamizi huwa hodari san kuziumia kuliko hata yule aliyezitunga. Ndio maana CCM leo ni hodari sana kutumia sheria nyingi kandamizi zilizotungwa na wakoloni kwa ajili ya kuidhibiti TANU
   
 7. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ccm tu ndio inaweza kununua wabunge na madiwani; hapo ni kuwapunguzia mbano na wale ccm wanaaoona haifai wanaweza kuhama wasidhurike kitu ambacho kinategemewa maana wapinzani already wako ktk suffering bench hatuwategemei sana kuathirika na sheria
   
Loading...