Wabunge Hawasimamishwi Kazi Wakiwa na Kesi za Jinai kwanini?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,799
Sheria ya utumishi wa umma inataka mtumishi yeyote anapokuwa na kesi ya jinai mahakamani utumishi wake unasimama na analipwa mshahara wake nusu akisubiri hatima yake.
Lakini tumeona Bungeni hali ni tofauti kwani wao wanaendelea na kazi ikiwemo kuwajadili walewale waliowasababishia kuwa na kesi mahakamani. Mfano mbunge Badwel alipofikishwa mahakamani kwa kesi ya rushwa wakati ule aliendelea kuchapa kazi mpaka kufikia watumishi mashahidi wa kesi ile kuwa na hofu ya ajira zao.
Jee hawa wabunge sheria hiyo haiwahusu au ni uzembe tuu wa Katibu na Spika wa bunge katika kuchukua hatua? Na kama haiwahusu ni kwa nini?
 
Lete kifungu cha sheria husika acha mambo ya kusikia. Unarejea sheria iliyokufa wewe!
 
Hapa mimi sijui kitu ngoja nimwite katibu wa bunge, katibuuu hatua inayofuata..... hebu toa maelezo hapa kwanza
 
Sheria ya utumishi wa umma inataka mtumishi yeyote anapokuwa na kesi ya jinai mahakamani utumishi wake unasimama na analipwa mshahara wake nusu akisubiri hatima yake.
Lakini tumeona Bungeni hali ni tofauti kwani wao wanaendelea na kazi ikiwemo kuwajadili walewale waliowasababishia kuwa na kesi mahakamani. Mfano mbunge Badwel alipofikishwa mahakamani kwa kesi ya rushwa wakati ule aliendelea kuchapa kazi mpaka kufikia watumishi mashahidi wa kesi ile kuwa na hofu ya ajira zao.
Jee hawa wabunge sheria hiyo haiwahusu au ni uzembe tuu wa Katibu na Spika wa bunge katika kuchukua hatua? Na kama haiwahusu ni kwa nini?
Hata mtumishi wa umma sio lazima kusimamishwa na pia sio lazima kulipwa nusu mshahara (tunashauri alipwe full tu kuepusha madai ya mshahara wake pindi kesi itakapoisha)..Kusimamishwa kazi itategemea na jinsi mamlaka yako ya nidhamu itakavyoona inafaa ila sio lazima wakusimamishe kazi labda kama kazi hiyo unayofanya kwa namna moja au nyingine inaweza kuharibu upelelezi wa kesi au inaweza kufanya uharibu zaidi...mfano hao wabunge ilitakiwa wasimamishwe ujumbe kwenye kamati ili wasiendelee kutuhumiwa kuomba rushwa kwa vikao vingine au wasiweze kupanga namna ya kujiokoa na tuhuma ziliZowafikisha kortini (kwa kunyofoa nyaraka nk)
 
Kwa sheria ya sasa unalipwa full salary. Kama ulivyosema kusimamishwa si lazima kunategenea mamlaka ya nidhamu na jinsi itakavyoona kama kuendelea kuwepo kazini kunaweza kuharibu ushahidi.
 
mkuu wabunge wako bungeni kupitia kura za wananchi kwa hiyo ni wawakilishi wa wapiga kura wao,japo wanalipwa na serikali,ndio maana sio rahisi kuwasimamisha ubunge hata wakiwa na kesi.tunapodai katiba mpya hayo ndio tunataka yarekebishwe ili wananchi waweze kumkataa mbunge wao kama hawaridhiki na utendaji kazi wakethata kama miaka yake mitano bado.
 
Lete kifungu cha sheria husika acha mambo ya kusikia. Unarejea sheria iliyokufa wewe!
Rejea post ineishia na kwa nini? Ni mfumo wa swali hivyo mwaga uelewa wako badala ya napenzi ya itikadi kwa vile mpaka sasa wabunge waliohusishwa ni wa ccm pekee. Maana siri bado zinaanikwa na kesho au keshokutwa wabunge hata wa upinzani waweza kuhusishwa.
Sasa kama sheria ya kusimamishwa kazi imefutwa, kwa nini watu kama Masamaki na wenzao wasiendelee kazini na utumishi wao ukahamishwa tuu badala ya pale bandarini na kuwa vitengo vingine?
Na kama wabunge wao haiwahusu kwani haina athari jee likitokea jambo la kuijadili Halnashauri ya Gairo unawezaje kutompa nafasi mfano Lugola asichangie mchango utakao mmaliza DED wa Gairo?
 
Sheria ya utumishi wa umma inataka mtumishi yeyote anapokuwa na kesi ya jinai mahakamani utumishi wake unasimama na analipwa mshahara wake nusu akisubiri hatima yake.
Lakini tumeona Bungeni hali ni tofauti kwani wao wanaendelea na kazi ikiwemo kuwajadili walewale waliowasababishia kuwa na kesi mahakamani. Mfano mbunge Badwel alipofikishwa mahakamani kwa kesi ya rushwa wakati ule aliendelea kuchapa kazi mpaka kufikia watumishi mashahidi wa kesi ile kuwa na hofu ya ajira zao.
Jee hawa wabunge sheria hiyo haiwahusu au ni uzembe tuu wa Katibu na Spika wa bunge katika kuchukua hatua? Na kama haiwahusu ni kwa nini?
yaah,.. hawa watu wamekua miungu mtu hata wenyekuhusika wanaogopa kutekeleza sheria. kuwakamata ilikua taboo na huku wengi kwa asili ni vibaka tu wamenunua ubunge kwa pesa chafu. sasa ni wakati wa sheria kufuatwa kama ni kusimamishwa wakati kesi zao zinaemdelea wasimamishwe. sio tumuone mtu eti yuko kwenye vikao vya kamati au ziara kama mbunge huku anatuhumiwa kula rushwa. hakika ni mzaha.
 
Rejea post ineishia na kwa nini? Ni mfumo wa swali hivyo mwaga uelewa wako badala ya napenzi ya itikadi kwa vile mpaka sasa wabunge waliohusishwa ni wa ccm pekee. Maana siri bado zinaanikwa na kesho au keshokutwa wabunge hata wa upinzani waweza kuhusishwa.
Sasa kama sheria ya kusimamishwa kazi imefutwa, kwa nini watu kama Masamaki na wenzao wasiendelee kazini na utumishi wao ukahamishwa tuu badala ya pale bandarini na kuwa vitengo vingine?
Na kama wabunge wao haiwahusu kwani haina athari jee likitokea jambo la kuijadili Halnashauri ya Gairo unawezaje kutompa nafasi mfano Lugola asichangie mchango utakao mmaliza DED wa Gairo?
Angalia post No. 5 na 6. Sina mapenzi na watuhumiwa wa rushwa. Hapa ni suala la kisheria tu
 
mkuu wabunge wako bungeni kupitia kura za wananchi kwa hiyo ni wawakilishi wa wapiga kura wao,japo wanalipwa na serikali,ndio maana sio rahisi kuwasimamisha ubunge hata wakiwa na kesi.tunapodai katiba mpya hayo ndio tunataka yarekebishwe ili wananchi waweze kumkataa mbunge wao kama hawaridhiki na utendaji kazi wakethata kama miaka yake mitano bado.
Naam ndugu yangu. KATIBA MPYA itamayaliza haya mazingaombwe yote. Watu wata "kimbilia" Bungeni KUTUMIKA na siyo KUJITUNISHA kiuchumi!..
 
Angalia post No. 5 na 6. Sina mapenzi na watuhumiwa wa rushwa. Hapa ni suala la kisheria tu
Post namba 6 ingekuwa ndiyo imekaa pale namba 2 ungekuwa unefanya la maana sana. Ok , umeeleweka.
Lakini kama mchukia rushwa jee hii imekaa sawa kweli kwa mtumishi wa umma kuendelea na utumishi akiwa na tuhuma za rushwa? Mfano Hakimu naye awe anasikiliza kesi za rushwa huku naye anatuhumiwa?
 
Tatizo wabunge wapo kimaslahi hata sheria zinatungwa kwa maslahi. Sheria zinazowagusa hazitakiwi kabisa. Ni lazima sasa serikali iingilie kati hii ni tabia mbaya.
 
Sheria zetu ni dhaifu sana katika kushughulikia makosa yanayohusiana na ufisadi....ndio maana haishangazi mtu aliyeitumia ofisi yake vibaya na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni wanapewa adhabu za kufanya usafi mahospitalini.......

Ndio maana leo watuhumiwa wa ufisadi huwa wanatabasamu wanapopelekwa mahakamani.....
 
Sheria ya utumishi wa umma inataka mtumishi yeyote anapokuwa na kesi ya jinai mahakamani utumishi wake unasimama na analipwa mshahara wake nusu akisubiri hatima yake.
Lakini tumeona Bungeni hali ni tofauti kwani wao wanaendelea na kazi ikiwemo kuwajadili walewale waliowasababishia kuwa na kesi mahakamani. Mfano mbunge Badwel alipofikishwa mahakamani kwa kesi ya rushwa wakati ule aliendelea kuchapa kazi mpaka kufikia watumishi mashahidi wa kesi ile kuwa na hofu ya ajira zao.
Jee hawa wabunge sheria hiyo haiwahusu au ni uzembe tuu wa Katibu na Spika wa bunge katika kuchukua hatua? Na kama haiwahusu ni kwa nini?
Kwani mbunge ni mtumishi wa umma??
Yeye ni mwakilishi tu , hajawahi kuajiriwa mahali popote na hana mshahara, anaishi kwa posho ambazo inabidi asaini ili apewe, akijisahau kuasini hapewi, labda zile za lazima kama mafuta na mengineyo.

Hana mkataba na serikali kwa hiyo serikali haiwezi kumwajibisha kwa kutumia sheria ya utumishi wa umma
 
Sheria zetu ni dhaifu sana katika kushughulikia makosa yanayohusiana na ufisadi....ndio maana haishangazi mtu aliyeitumia ofisi yake vibaya na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni wanapewa adhabu za kufanya usafi mahospitalini.......

Ndio maana leo watuhumiwa wa ufisadi huwa wanatabasamu wanapopelekwa mahakamani.....
Ninakubaliana na angalizo lako. Tuna sheria dhaifu sana katika makosa ya ufisadi na rushwa.

Mimi nina hamu sana ya kufahamu adhabu zitakazotolewa kwenye sheria itakayoletwa kuhusu mahakama za mafisadi.
 
Back
Top Bottom