Wabunge hawa wametuangusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge hawa wametuangusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by clemence, Nov 15, 2011.

 1. clemence

  clemence JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 595
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwanza nianze kwa kusema kuwa Watanzania wa leo sio wale wa miaka hiyo ambao walikuwa wanaitikia kila kitu kinachosemwa na viongozi wao, wakiamini kuwa kila neno litokalo kwa kiongozi ni sahihi na ni mwiko kupinga.

  Leo hii kiongozi unapoamua kuongea ili uma wa Watanzania wakusikie wakuelewe na hatimaye wakuamini inabidi ujipange sawasawa, kwani watu wa leo wanapenda kuzitafakari kauri za viongozi wao.

  Jana sikuamini kama ni Mh ANNA KILANGO huyu ninae mfahamu ambaye alikuwa aliishikia bango issue ya Richmond au ni mwingine? Kwamba Mh KILANGO hajui tume ya kusimamia mchakato wa kukusanya maoni juu ya katiba mpya pamoja na bunge la katiba vitachaguliwaje kama raisi asipopewa hayo mamlaka.

  Je Kilango nafasi aliyo nayo aliteuliwa na raisi au alichaguliwa na wananchi? Nadhani hakumsikia prf Shivji, vinginevyo asinge hoji hao wajumbe wanaweza kupatikana vipi kama raisi atapunguziwa mamlaka katika uundwaji wa katiba mpya.

  Kweli ANNA KILANGO umeniangusha kuwa hauna dhamira ya kweli ya kumsaidia Mtanzania bali kuisaidia CCM. Na huyu naye mbunge wa cCUF KHALIFA kama sijakosea jina lake, anawataka wabunge waaendelee na mjadala kwa madai kuwa hizo kasoro zitahojiwa na Wananchi na hivyo kuja kurekebishwa kwa kuondoa ama kuongeza wanachokitaka Wananchi.

  Jamani wana JF kweli huyu na ubunge wake hajui ni nini ambacho upinzani unataka? Utakuja kubadiri nini wakati tayari umeshapitisha bungeni mswada unaompa mamlaka makubwa raisi ya kuteua kila kitu.

  Je kwa fikra zake kutakuwa na uhuru wa kweli katika kuifikia katiba tunayoitaka, nani atakuwa kinyume na raisi wakati wote ni wateule wake?

  Leo hii wabunge wa CCM hawako huru japo wamechaguliwa na Wananchi na japo wao wenyewe wanasema wana wawakilisha Wananchi, lakini ukweli ni kuwa kutokana na mfumo tulionao wabunge hawa wanajikuta wanawakilisha serikali ya CCM hata kama nafsini mwao hawapendi.

  Watafanyaje ili hali wakiwa kinyume na serikali wanafukuzwa uanachama na ubunge unakoma. Inashangaza sana kwa wabunge wa ccm pamoja na kupata nafasi hii ya kuweza kubadilisha mifumo mibovu kandamizi.

  Inasikitsha sana tena sana kwa usaliti huu wa wabunge wa ccm na hawa baadhi wa upinzani.

   
 2. J

  Juma. W Senior Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mh. Kilango hajui hata alama za nyakati, Tanzania anayoijua yeye ni ile ya "Zidumu Fikra Sahihi". Tunahitaji umakini zaidi hapa, la sivyo tutaiweka Tanzania pabaya.

  Baadhi wanadhani katiba ijayo ikiwa "on their favor" itawasaidia miaka yote. Huu ni mtazamo duni sana, katiba ni zaidi ya uchaguzi, ni zaidi ya maisha ya watanzania wa leo, ni kwaajili ya Tanzania ya leo na hata ijayo. Tumezoea hata ukija muswada ambao hata mtu wa kawaida anaone upoupo, mradi umetoka serikalini basi kundi fulani la watu hulazimisha upite. Hawa watu walichaguliwa na serikali kuiwakilisha bungeni??? kama wamechaguliwa na wananchi nadhani wangejua ni nini wanatakiwa kufanya.
   
 3. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ....tuna wabunge wachache sana Tanzania (kwa maana ya wawakilishi wa wananchi). Wengi ni wawakilishi wa serikali, nadhani asilimia kubwa ya wabunge wa CCM wapo si kwa ajili ya wananchi bali serikali.

  Inasikitisha sana, kuchaguliwa na wananchi na kisha kuwageuka waliokuchagua.

  Siwalaumu wabunge wa viti 'maalum' kwa kuwa wao wapo kwa kazi 'maalum', ila hawa waliochaguliwa kwa kura!!

  Mama Kilango kazibwa masikio labda na ubongo, haamini kuwa wananchi wana maamuzi na akili kuliko hata rais. Anahisi rais ni jamii ya 'mungu' ambae maamuzi yake ni ya msingi mara zote.

  Khalifan nae anahisi wanaonewa, hawajali watanganyika tena. Kupewa nafasi kubwa kwake imekuwa faida. Anashangaa wasomi na kujisifu kwa kutosoma 'sana'. Nadhani hilo ni tatizo kwake. Hawaamini wengine nadhani hata utashi wake hauamini zaidi ya serikali.

  Tunapanda mbegu, tusipochagua vizuri aina ya mbegu kulingana na mazingira yetu tutavuna haba ama hatutavuna kabisa.
  Tusiangalie Kenya, Uganda, Zambia wamefanya nini. Ila tuangalie watanzania wanahitaji nini.
  Kwanini wao wawe mifano kwetu tu, na sisi tisiwe mfano kwao!?

  Kupanga ni kuchagua, tukipanga hovyo na matunda yatakuwa hovyo. Tuamue leo kwa kesho njema.

  Mungu atupe hekima na tuitumie ipasavyo.
   
 4. b

  bubukapoka Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kwamba wametuangusha tu,lakini nilichofurahi tumewajua kama ni mamruki waliokua wamejificha kichakani.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wakoloni weusi someni alama za nyakati watu mitaani wamechoka sana sasa hivi wanaelewa nani ni mkombozi wao na nani anakwamisha maendeleo yao na nani ananufaika kwa kupitia migongo ya walalahoi someni alama za nyakati mapema kabla hamjaanza kusoteshwa magerezani kutesa kwa zamu
   
 6. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu, kwa kifupi, HAIJAWAHI KUTOKEA enzi hizi mtu mzuri akawa ndani ya CCM. Ni lazima ujue kuwa viongozi walioshikiria madara Africa ni Genge na linatakiwa kuondolewa lote bila kuwa na FIKRA kuwa ndani ya genge hilo kuna MKOMBOZI na MTETEZI wa wanyonge.

  Ni kundi la watu waliojisahau na ndo maana umeona wanashirikiana na kina CUF na "DKT" Mlema. Wote hao wasanii na wanasitahili kuhadhibiwa siku moja ambayo haiko mbali
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  2015 itakuwa zamu yetu kuwaangusha kwenye masanduku ya kupigia kura
   
 8. D

  Deo JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kilango si tu alijiaibisha bali pia aliwaaibisha wapiga kura wake kwa vile alitoa msimamo wake binafsi kana kwamba ni wa wapiga kura wake.

  Kilango anaangalia alama ya nyakati za maslahi ya muda mfupi, akitegemea ateuliwe na rahisi kwenye nafasi yeyeyote.

  Kilango amefuta na kuchafua sifa alizochota wakati wa richmond kitaifa na kimataifa, sinashaka hata jimboni kwake ni hivyo hivyo tu.

  Aibu yako ni kubwa mama
   
 9. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tuna safari ndefu sana wa-Tz kisiasa, wabunge kujitapa kuwa wanawakilisha mawazo ya wananchi wakati hawakuwahi kufanya mchakato wowote wa kukusanya maoni yetu si unafiki na uongo mkubwa? Nilimsikia Kilango akijitapa kuwa anazungunza kwa niaba ya wananchi wa Same Mashariki wakati yale yalikuwa mawazo yake binafsi. Ninaamini hivyo kwani mchango aliotoa wa kuwakandia wapinzani waliotoka nje hakutumwa na wananchi wa Same Mashariki, wangemtuma kwani walikuwa wabashiri kujua wapinzani watatoka nje?. Zile dakika alizokuwa anaomba Speaker azilinde alikuwa amepanga kuzungunza nini alichotumwa na wananchi wake? Kwa jinsi mchakato wa kuandika katiba mpya ulivyo muhimu nilitegemea aje na hoja yakinifu zikiainisha vipengele ambavyo vina dhaifu katika mswada huu. Lakini kwa mshangao alianza kuzungunza mambo ambayo hakupanga kabla. Wa-Tz tuamke hawa wapiga kelele wasio wakilisha mawazo yetu tuwapige chini ghafla, hatuhitaji bla bla kwenye maswala nyeti kama haya.
   
 10. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hatutakiwi kufika 2015 kwakuwa wanajua rais wao ataunda tume ya uchaguzi ya kuwapitisha majimboni. Hawa napendekeza ata ikibidi tuwaloge.
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ndoto za mchana hizo mkuu!!! Unamfahamu Lewis Makame na Abdalah Kiravu? Au tutakodi tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zambia???
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ahh wananchi nao wabadilike
   
 13. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  hii imenikumbusha sikuile ya kongamano la katiba pale UDSM Dr.Lwaitama alivyokuwa anamshawishi mh.Mnyika akubali huu muswada upelekwe bungen kwa kuwa tutapata fursa ya kuwaona hao wanafki na kuwasikia hao wasiopenda mabadiliko haya,,,,,is the matter of time mengi yanakuja.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo CCM na huyu Anna Kilango bado wanaamini kuwa yeye (Anna Kilango) ni maarafu mbele ya watanzania wengi. Jambo ambalo hawataki kuelewa ni kuwa huyu Kilango alipata umaarufu kutokana na kupinga ufisadi, lakini pale aliageuka ghafla na kuanza kula na mafisadi umaarufu wake uliisgha. Sasa hivi tunaelewa hata ile hoja ya ufisadi haikuwa inatoka moyoni, alikodishwa huyu mama kwa sababu walimjua ni msemahovyo asiye na aibu. She is just a loose canon.
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,583
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Mimi wamenifurahisha sana kwani wamejivua nguo wenyewe, tusubiri hukumu ya wananchi 2015.
   
 16. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hawa watu wanatuchezea akili zetu kweli,kama waganga wa Tanzania wangeamua kutengeneza nyuklia na kuwalipua vichwa vyao,ingekaa vizuri sana tena wangewatumia wakiwa mjengoni.
   
 17. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,746
  Trophy Points: 280
  Gamba ni gamba tu liwe la kike
  ama la kiume ni gamba
  huyu mama aliniaibisha
  na labda alivyokuwa
  anang'aka alikuwa anasaka umaarufu tu
  ili ----------- ampe angalao
  ukuu wa wilaya
  shame on those two women
  supika na huyo kill" ango


   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Problem with most ccm legislators they either dont read the bills due to laziness or they dont understand technical terms in the bill, so the best thing for them is to accept everything because if you oppose you have to understand what you are opposing and you must give reasons to convince the mass at large, but saying I accept 100% is easy any Bloody idiot can do that!!
   
Loading...