Wabunge EALA wabaini vikwazo vya maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge EALA wabaini vikwazo vya maendeleo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Sep 3, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2]Wabunge EALA wabaini vikwazo vya maendeleo[/h][h=2][/h] Jumatatu, Septemba 03, 2012 05:15 Otilia Paulinus na Aziza Hassan, Dar es Salaam

  WABUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wamesema wamebaini vikwazo vinavyozuia maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki ambavyo vingi vinasababishwa na mifumo dume katika nchi husika.

  Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bunge hilo Tawi la Tanzania, Adam Kimbisa.

  Alisema ingawa nchi hizo ni tajiri, lakini wananchi wake ni masikini, huku uchumi ukiwa bado ni tegemezi.

  “Nchi zote tano zina rasilimali watu tena ni wachapakazi hasa, lakini wanakabiliwa na umasikini na tumegundua tukishirikiana kwa kutumia rasilimali zetu kama ardhi tutafanikiwa.

  “Nchi za Afrika Mashariki zina ardhi ambayo ina manufaa juu na chini, pia tunaweza kutumia bandari zetu hizi mbili ya Dar es Salaam na Mombasa kwa kuziridhisha nchi zote tano.

  “Kwa miezi hii miwili toka tuchaguliwe tumeweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo tukienda katika bunge hili ambalo linaanza leo, tutaweza kujadili na kuyatafutia ufumbuzi,” alisema Kimbisa.

  Alisema kutokana na idadi ya watu milioni 133 iliyopo ni rahisi mwekezaji yeyote kuvutiwa kuja kwa kuwa anaweza kupata faida kubwa kutokana na wateja waliopo.

  Naye, Katibu wa Wabunge hao, Shyrose Bhaji, alisema ni muhimu wanawake wakapiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.

  “Tatizo kubwa lililopo ni kwamba, wananchi wengi hawaelewi ujasiriamali ni nini, sasa ni muhimu wananchi wajikite katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  “Soko ni kubwa, tuitangaze Jumuiya ya Afrika na hatimaye wananchi waweze kufaidika, tusizoee kuona akina Bakhresa tu kwa kuwa wako wengi, sisi tumejiandaa kufanya kila tunaloweza kuwainua kwa kuwapigania,” alisema Bhanji

  Wabunge hao wanaoiwakilisha Tanzania wamechaguliwa katika kamati mbalimbali za maendeleo katika Bunge la kwanza lililofanyika miezi mitatu iliyopita.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
Loading...