Wabunge CCM Wataka Rais Ahojiwe Bungeni

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
Hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatazamiwa kukumbwa na mtikisiko kutokana na kuwepo nia ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete, ahojiwe bungeni.

Taarifa za ndani zilizolifikia NIPASHE Jumamosi zinaeleza kuwa, hatua hiyo inatarajiwa kufanikishwa kupitia mabadiliko ya kanuni yatakayoamuru Rais wa nchi kuhojiwa na Bunge kupitia maswali ya papo kwa hapo, badala ya Waziri Mkuu kama ilivyo sasa.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaielezea hali hiyo kuwa huenda ikakumbwa na mtikisiko na malumbano ya kisheria kati ya makundi yanayounga mkono mfumo uliopo sasa na wale wanaomtaka Rais aulizwe maswali.

Hadi kufikia sasa, imebainika kuwa hoja hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ritta Enespher Kabati.

Kabati amethibitisha azma hiyo lakini akapinga kwamba inatokana na shinikizo la kundi moja kati ya yanayopingana ndani ya CCM.
"Mimi sina haja ya kupata shinikizo lolote, nina akili na uwezo wangu, ninatambua kwamba ninawatumikia wananchi wa Iringa hasa wanawake," alisema katika mahojiano yake na NIPASHE Jumamosi.

Kabati alisema nia ya kuwasilisha hoja hiyo inatokana na uchunguzi aliowahi kuufanya kwa nyakati tofauti na kubaini kwamba asili ya kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu ni Bunge la Uingereza ambapo Waziri Mkuu ana mamlaka ya kuwa Mtendaji Mkuu wa serikali, tofauti na ilivyo hapa nchini.

"Ninavyouona mfumo huu, tunahitaji kufanya marekebisho ili badala ya Waziri Mkuu kuulizwa maswali ya papo kwa hapo, awe anakuja Rais wa nchi," alisema.

Kabati alisema mfumo uliopo sasa ambapo Waziri Mkuu anashindwa kutoa majawabu ya baadhi ya hoja za wabunge anazoulizwa, isipokuwa kuelekeza kwenye mamlaka ya Rais, kunatoa fursa ya kufanya mabadiliko hayo.

"Kama unavyolifuatilia Bunge kuna wakati Waziri Mkuu anatoa majawabu yasiyowaridhisha wabunge, inafikia wakati anaonekana anadanganya na hata kufikia hatua ya kudhalilishwa kama ilivyowahi kutokea wakati Godless Lema alipokuwa Mbunge wa Arusha Mjini.

Lema aliwahi kuliambia Bunge kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilidanganya Bunge wakati akitoa majibu kuhusu mgogoro uliosababisha mauaji ya raia mjini Arusha, hali iliyosababisha kiti cha Spika kumpa siku saba kuthibitisha kabla ya kutolewa mwongozo.

Hadi kufikia sasa, gazeti hili halijapata kumbukumbu zinazoonyesha kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda ama wasaidizi wake walishatoa bungeni utetezi wa Lema kuhusu hoja hiyo.

"Kwa hiyo ninaona kwamba kama Rais atakuwa anakuja kujibu maswali kila Alhamis, itasaidia kupunguza mkanganyiko na wakati mwingine kumfanya aonekane anadanganya," Kabati alisema.

Source: Nipashe

My Take:- Iwapo huu utaratibu utaafikiwa, "DHAIFU" atakuwa na majibu ya kuwaridhisha wabunge kuliko "LIWALO NA LIWE"? Naona kama hawa wabunge wana hamu ya kupewa majibu ya uongo na ahadi hewa zisizotekelezeka.
 
Itakuwa na tofauti gani hotuba zake za kawaida Mkuu, si ni kama siku zote tu anapohutubia bunge tu??

Ninachoaamini ni kuwa kila swali litapata blah blah zake...... "tumejipanga, tuko mbioni, pia tumeliona hilo, mchakato naendelea kwenye ofisi yangu, nimeongea na waziri juzi.... blah blah blah"
 
Katiba ya sasa ya Tanzania waziri mkuu ndio kiongozi wa serikali bungeni na sio rais. Labda katiba mpya na usisahau mfumo wetu ni tofauti na UK kama unavyotaka kuufanisha, hapa kwetu rais ni mkuu wa nchi (head of state) na ni mtendaji (executive), wakati huko UK malkia ni mkuu wa nchi (head of state) lakini si mtendaji maana wao mfumo wao ni wa ufalme wa kikatiba yaani constitutional monarchy.

Kuna matabaka makuu matatu ya utawala katika nchi yetu na yote kinadharia yana uhuru na kujitegemea yaani Serikali, bunge na mahakama na hayaingiliani katika utendaji wake, at least in theory...
 
hapa nadhani kila alhamis jamaa anaweza akawa anajitafutia safari za nje.....
 
hiyo itaharibu hata zaidi, majibu hapa tanzania hayafungi mtu
 
kUMHOJI RAISI HAKUNA MANTIKI KWA MFUMO WETU W UONGOZI

KWA MUJIBU WA KATIBA WAZIRI MKUU NDIO MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI

HIVYO CHA KUFANYA NI KUTAMBUA RAISI NI KIONGOZI WA KUCHAGULIWA, TUMUACHE AFANYE KAZI ZA KUHAMASISHA, KUJENGA UHUSIANO KUTOA MAAMUZI YA MWISHO YASIYO YA KUKURUPUKA

LAKINI KWA KUJUA KWANINI TUSAIDIWE NA WATENGENEZA MAGARI KUJENGA BARABARA ILI TUNUNUE ZAIDI "KAMA COCA COLA ANAVYOMPATIA MWENYE DUKA FRIJI" HUKU FEDHA YOTE IMAYOTOKANA NA MADINI, SAMAKI, MAZAO KWA WINGI INAKWENDA NJE KUPITIA MAGARI, SIMU, KOMPUTA, NA MENGINE.

TUNALALAMIKA UCHUMI UNAKUA LAKINI UMASIKINI HAUPUNGUI KUMBE MIPAKA YA NCHI INAVUJA TUZIBE MIPAKA FEDHA IKIINGIA IZUNGUKE KUONGEZA UWEZO WA KUNUNUA NA KUTENGENEZA AJILA NA KUTOKA ITOKE KWA SHIDA.

HAYA TUMUACHIE WAZIRI MKUU KWANI ALIYESEMA WAZIRI MKUU AWE MTENDAJI MKUU KIKATIBA ALIJUA KUWA URAISI UNAHITAJI KUWA MAARUFU KUCHAGULIWA.

ILA TUNAKOSEA KWA WAZIRI MKUU HUYU NDIYE ANATAKIWA KUBALANSI UONGOZI KUWEKA SIFA ZA KIUTENDAJI NA KUFUATILIA KILA KITU.

KWA MUJIBU WA KATIBA BUNGE NDICHO CHOMBO KIKUU CHA MAAMUZI KATIKA JAMHURI HIVYO BASI

BUNGE LILITAKIWA KUWA KAMA BODI YA KUSIMAMIA SERIKALI LIKISHAURI NA KUWAJIBISHA

KAMA WAO HAWAJAJITAMBUA KWA MAMLAKA HAYA BADO TUNA KAZI YA KUFANYA ILI TUFIKIE SERIKALI KUTUMIKIA WANANCHI NA BUNGE KUSIMAMIA SERIKALI
 
sijawahi ona JK akirusu maswali ya papo kwa hapo kama vile kukutana na waandishi wa habari!yeye uhutubia tuu
 
Huyo mama katumwa na nani? Amweche Jk coz ana mihangaiko ya kutalii na kuijua dunia zaidi. Kama hataki waziri mkuu amjibu, na agome kwenda bunge liwalo na liwe.
 
Hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatazamiwa kukumbwa na mtikisiko kutokana na kuwepo nia ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete, ahojiwe bungeni.

Taarifa za ndani zilizolifikia NIPASHE Jumamosi zinaeleza kuwa, hatua hiyo inatarajiwa kufanikishwa kupitia mabadiliko ya kanuni yatakayoamuru Rais wa nchi kuhojiwa na Bunge kupitia maswali ya papo kwa hapo, badala ya Waziri Mkuu kama ilivyo sasa.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaielezea hali hiyo kuwa huenda ikakumbwa na mtikisiko na malumbano ya kisheria kati ya makundi yanayounga mkono mfumo uliopo sasa na wale wanaomtaka Rais aulizwe maswali.

Hadi kufikia sasa, imebainika kuwa hoja hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ritta Enespher Kabati.

Kabati amethibitisha azma hiyo lakini akapinga kwamba inatokana na shinikizo la kundi moja kati ya yanayopingana ndani ya CCM.
“Mimi sina haja ya kupata shinikizo lolote, nina akili na uwezo wangu, ninatambua kwamba ninawatumikia wananchi wa Iringa hasa wanawake,” alisema katika mahojiano yake na NIPASHE Jumamosi.

Kabati alisema nia ya kuwasilisha hoja hiyo inatokana na uchunguzi aliowahi kuufanya kwa nyakati tofauti na kubaini kwamba asili ya kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu ni Bunge la Uingereza ambapo Waziri Mkuu ana mamlaka ya kuwa Mtendaji Mkuu wa serikali, tofauti na ilivyo hapa nchini.

“Ninavyouona mfumo huu, tunahitaji kufanya marekebisho ili badala ya Waziri Mkuu kuulizwa maswali ya papo kwa hapo, awe anakuja Rais wa nchi,” alisema.

Kabati alisema mfumo uliopo sasa ambapo Waziri Mkuu anashindwa kutoa majawabu ya baadhi ya hoja za wabunge anazoulizwa, isipokuwa kuelekeza kwenye mamlaka ya Rais, kunatoa fursa ya kufanya mabadiliko hayo.

“Kama unavyolifuatilia Bunge kuna wakati Waziri Mkuu anatoa majawabu yasiyowaridhisha wabunge, inafikia wakati anaonekana anadanganya na hata kufikia hatua ya kudhalilishwa kama ilivyowahi kutokea wakati Godless Lema alipokuwa Mbunge wa Arusha Mjini.

Lema aliwahi kuliambia Bunge kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilidanganya Bunge wakati akitoa majibu kuhusu mgogoro uliosababisha mauaji ya raia mjini Arusha, hali iliyosababisha kiti cha Spika kumpa siku saba kuthibitisha kabla ya kutolewa mwongozo.

Hadi kufikia sasa, gazeti hili halijapata kumbukumbu zinazoonyesha kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda ama wasaidizi wake walishatoa bungeni utetezi wa Lema kuhusu hoja hiyo.

“Kwa hiyo ninaona kwamba kama Rais atakuwa anakuja kujibu maswali kila Alhamis, itasaidia kupunguza mkanganyiko na wakati mwingine kumfanya aonekane anadanganya,” Kabati alisema.

Source: Nipashe

My Take:- Iwapo huu utaratibu utaafikiwa, "DHAIFU" atakuwa na majibu ya kuwaridhisha wabunge kuliko "LIWALO NA LIWE"? Naona kama hawa wabunge wana hamu ya kupewa majibu ya uongo na ahadi hewa zisizotekelezeka.

Yetu macho
 
Raisi hana mda wa kusikiliza hoja wala maswali ya wabunge na wananchi. Amebanwa na safari za nje ambazo zinaiweka nchi kwenye madeni yasiyolipika. Labda huyu mama ajaribu anaweza akasikilizwa ila sidhani
 
Dhaifu sidhani kama ataweza kuyajibu hayo maswali kwa alivyomvivu wa kufikiri!
 
wameanzisha hiyo hoja wenyewe halafu wataipinga wenyewe
 
mpaka miaka mitano iishe tutakuwa tumeona mengi na kusikia mengi,Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom