Wabunge CCM wafanya siasa za kibaguzi kwenye bajeti UCHUKUZI

Dec 11, 2010
3,322
0
Wabunge wa CCM kutoka kanda ya ziwa wamefanya siasa za kibaguzi bungeni kwa kutoa michango yao huku wakionyesha kuwa wanabaguliwa kwa kuwa wao ni wasukuma na ndio maana mradi wa ujenzi wa uwanjwa wa ndege wa Mwanza umesimama na si sawa na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sogwe mkoani Mbeya.

Ki mantiki wao (wa kanda ya ziwa) wanaona kuwa wao hawapelekewi maendeleo kwa kuwa waziri ni si mtu kutoka kanda yao (Ziwa) na yeye niwa kanda ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya), Nimemsikia Mh Chenge akisema "...Hatujengewi uwanja wa ndege wa Mwanza kwa kuwa sisi.... kwa kuwa sisi....." Na baadae akapata nafasi mbunge mwingine wa CCM, naye akaja na hoja vilevile za ukanda.

Kwa aina hizi za siasa za kibaguzi, CCM wanazidi kuipeleka nchi yetu pabaya,kama vipaumbele vya maendeleo vinapangwa kwa namna wabunge wa CCM walivyo kuwa wanaotoa hoja za ukabila/ukanda na si kwa nguvu ya hoja basi kazi tunayo kwa siasa za namna hii.

Mwenyezi Mungu atuepushe na hili balaa
 
Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
Cheo ndio alimalizia kwa kuwa sisi ni Wasukuma, mambo ya Kakobe yako mbioni kutokea na hata ndoto ya mama Maria Nyerere Inaelekea kutimia .....
 
The Name

JF-Expert Member
Jan 30, 2014
812
225
Maccm yatakufa kifo kibaya sana haiwezekani watanzania wanataka maendeleo,wanataka mambo ya msingi yapewe kipaumbele,wabunge magamba wao kupiga meza tu na kupitisha mambo yasiyokua na msingi,hosptali hakuna,madawa hakuna,barabara hakuna!mwakembe anaahidi ndege tu,raisi amekaa kimya anakula bata tu nje ya nchi,kinana na nape wanawadanganya wananchi huko mikoani,ccm mungu awalani na ukoo wenu wote!
 
Matawana

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
730
250
Ukweli lazima usemwe, uwanja wa Mwanza ni muhimu kiuchumi kuliko songwe. Sisemi songwe usingejengwa lakini priority ingekuwa mwanza
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
Nimemsikia KOMBA akiwazodoa CHADEMA kuwa hawana hata ofisi, kwahiyo akamuasa Mwakyembe kuwa asiwasikilize sana hawa wahuni, yeye achape kazi. Maendeleo yanaonekana.
 
isotope

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
2,392

Chenge naye chadema? Sema kwa sauti akusikie!
 
Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,794
1,500
Ukweli lazima usemwe, uwanja wa Mwanza ni muhimu kiuchumi kuliko songwe. Sisemi songwe usingejengwa lakini priority ingekuwa mwanza
Kwani uwanja wa Songwe umeanza kujengwa wakati Mwakyembe akiwa waziri wa uchukuzi? Ila Mwakyembe amesema kuwa mpango uliopo ni kuufanya uwanja wa Mwanza kuwa ni mkubwa kuliko viwanja vyote Afrika ya Mashariki
 
isotope

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
2,392
0
Wabunge wa CCM kutoka kanda ya ziwa wamefanya siasa za kibaguzi bungeni kwa kutoa michango yao huku wakionyesha kuwa wanabaguliwa kwa kuwa wao ni wasukuma na ndio maana mradi wa ujenzi wa uwanjwa wa ndege wa Mwanza umesimama na si sawa na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sogwe mkoani Mbeya.

Ki mantiki wao (wa kanda ya ziwa) wanaona kuwa wao hawapelekewi maendeleo kwa kuwa waziri ni si mtu kutoka kanda yao (Ziwa) na yeye niwa kanda ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya), Nimemsikia Mh Chenge akisema "...Hatujengewi uwanja wa ndege wa Mwanza kwa kuwa sisi.... kwa kuwa sisi....." Na baadae akapata nafasi mbunge mwingine wa CCM, naye akaja na hoja vilevile za ukanda.

Kwa aina hizi za siasa za kibaguzi, CCM wanazidi kuipeleka nchi yetu pabaya,kama vipaumbele vya maendeleo vinapangwa kwa namna wabunge wa CCM walivyo kuwa wanaotoa hoja za ukabila/ukanda na si kwa nguvu ya hoja basi kazi tunayo kwa siasa za namna hii.

Mwenyezi Mungu atuepushe na hili balaa
Kiukweli uwanja wa Mwanza haujengwi kwa kiwango cha kimataifa, majengo mapya ya abiria ni kama vibanda vya soko la manzese. Daladala zinageuzia kwenye mlango wa abiria hivyo kuleta hofu ya usalama. Kwa kifupi kile kiwanja hakiendani na hadhi ya Mwanza. Kulalamika ni halali ingawa mlalamikaji kakosea kutanguliza mbele usukuma wake, mwanza siyo ya wasukuma pekee.
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,364

Shekh Mtoi mimi naona wewe ndio unaleta siasa za kibaguzi, na ukuiendelea hivi utaiharibu CDM, Mzee Mtei na Bob Makani walipokuwa pamoja alielewa umuhimu wa umoja huo, pili suala hili lilisha ongelewa hapo awali wakati Kingunge alikuwa ni waziri awamu ya kwanza ya Kikwete, sasa kurudiwa leo si jambo la ajabu. Hivyo ukiwa mtu mwenye akili uache kuleta uchchezi usio na maana, kama unataka kusema mapungufu ya serikali wewe, sema na si kuitumia issue hii ya uwanja na mengineyo kuelekea kati ukanda huo, kwani effect yake haipo kwa wasukuma tu, bali BKB, Mara nk. Na Kura Nyingi iwe kwa CDM na CCM ziko huko, na ukila na kipofu usi mshike mkono.
 
ngungwangungwa

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
572
250
Kiukweli uwanja wa Mwanza haujengwi kwa kiwango cha kimataifa, majengo mapya ya abiria ni kama vibanda vya soko la manzese. Daladala zinageuzia kwenye mlango wa abiria hivyo kuleta hofu ya usalama. Kwa kifupi kile kiwanja hakiendani na hadhi ya Mwanza. Kulalamika ni halali ingawa mlalamikaji kakosea kutanguliza mbele usukuma wake, mwanza siyo ya wasukuma pekee.
Ulitaka atangulize nini!? Mwanza ni ya wasukuma,wengine ni wageni. Huo ndo ukweli
 
isotope

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
2,392
0
Ulitaka atangulize nini!? Mwanza ni ya wasukuma,wengine ni wageni. Huo ndo ukweli
Nimekaa mwanza ila sijawahi sikia kuna watu wanaitwa wasukuma wa mwanza. Kuna wasukuma wa ntuzu, wasukuma wa kayenze, n.k Hii inamaana wasukuma pia mwanza ni wakuja tu ndo maana wanatambuana kwa asili zao.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Watu kama wewe kila mara fikra zenu zinasimama katika siasa za mlengo wa vyama. Kama hayo yamesemwa na wabunge, basi hayo ni mawazo ya wabunge wanaowawakilisha wananchi wao.

Wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwa maana kwamba, walichaguliwa na wananchi wengi ambao siyo wanachama wa vyama vya siasa, lakini kikubwa zaidi, ndani ya bunge hakuna wawakilishi/wabunge wa CCM bali kuna wawakilishi/wabunge wa wananchi.

Mawazo kama haya ndiyo yanadumaza hata harakati za maendeleo katika msingi wa umoja. Sitashangaa hata katika mawazo yako, unapenda sana maendeleo yasifanyike ili CCM wasipate hoja katika uwanja wa siasa, kwa maana nyingine, maumivu ya wananchi ndiyo mtaji wako kisiasa.

spinning kama hizi haziwezi kukusaidia katika kuyafikia malengo yako ya siasa za kilaghai.
 
mgenikaribu

Member
Mar 23, 2014
66
70
Tusitafune maneno huu ukanda upo na utaendelea kuwepo, cha kufanya ni kutumia huu ukanda kuleta maendeleo ya haraka kwa kuigawa hii nchi kimajimbo kama zilivyo nchi nyengine zilizoendelea kama Japan, Canada, USA. Jimbo liongozwe na Gavana ataechaguliwa na wananchi wenyewe, tuachane na sijui wakuu wa mikoa na wilaya. Kila jimbo liwe na vyanzo vyake vya uchumi na ikusanye kodi zake kwa maendeleo ya jimbo lake. Kila jimbo lichangie kodi ndogo kwa mfano kama kodi ni asilima 15, 10% ibakie jimboni na 5% kuchangia serikali kuu kwa mambo ya nchi yote kama reli na highway/underground zinazounganisha majimbo, ulinzi wa nchi n.k. Tanzania yote imejaa raslimali lakini hivi sasa zinatafunwa na wajanja wachache ambao ni wahafidhina ambao mabadiliko yeyote kwao ni mwiko.
 
maswitule

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,393
1,225
Ukweli lazima usemwe, uwanja wa Mwanza ni muhimu kiuchumi kuliko songwe. Sisemi songwe usingejengwa lakini priority ingekuwa mwanza

Hapana ki ukweli Uwanja wa ndege wa Songwe ni Mhimu kwa maendeleo ya nchi za SADC na wankusini pia, Kwanza mwanza upo Mbeya kulikuwa hakuna Uwanja kule.
 
Gwalihenzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
5,126
2,000
Tena kawaambia kuwa wana kitundu tu pale Kinondoni
Duh! kitundu kama hiki hapa?
 
Mantissa

JF-Expert Member
Jul 24, 2010
876
225
Nimemsikia KOMBA akiwazodoa CHADEMA kuwa hawana hata ofisi, kwahiyo akamuasa Mwakyembe kuwa asiwasikilize sana hawa wahuni, yeye achape kazi. Maendeleo yanaonekana.

Bora ungetaja mtu mwenye akili, unataja boya?. Nawe kama jina lako tu msalani ambalo ni tofauti sana na jina langu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom