Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Wabunge wa CCM kutoka kanda ya ziwa wamefanya siasa za kibaguzi bungeni kwa kutoa michango yao huku wakionyesha kuwa wanabaguliwa kwa kuwa wao ni wasukuma na ndio maana mradi wa ujenzi wa uwanjwa wa ndege wa Mwanza umesimama na si sawa na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sogwe mkoani Mbeya.
Ki mantiki wao (wa kanda ya ziwa) wanaona kuwa wao hawapelekewi maendeleo kwa kuwa waziri ni si mtu kutoka kanda yao (Ziwa) na yeye niwa kanda ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya), Nimemsikia Mh Chenge akisema "...Hatujengewi uwanja wa ndege wa Mwanza kwa kuwa sisi.... kwa kuwa sisi....." Na baadae akapata nafasi mbunge mwingine wa CCM, naye akaja na hoja vilevile za ukanda.
Kwa aina hizi za siasa za kibaguzi, CCM wanazidi kuipeleka nchi yetu pabaya,kama vipaumbele vya maendeleo vinapangwa kwa namna wabunge wa CCM walivyo kuwa wanaotoa hoja za ukabila/ukanda na si kwa nguvu ya hoja basi kazi tunayo kwa siasa za namna hii.
Mwenyezi Mungu atuepushe na hili balaa