Wabunge acheni Ushamba wa Madiwani – Momose Cheyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge acheni Ushamba wa Madiwani – Momose Cheyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Aug 7, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wabunge acheni Ushamba wa Madiwani – Momose Cheyo

  Asubuhi leo katika mjadala wa Kipindi cha Tuongee Asubuhi Star TV nimefuatilia kwa ukaribu na tafakuri kubwa mjadala uliokuwa ukiendeshwa na Chilala kuhusu Michango ya Wabunge huko Mjengoni na Studioni alikuwepo Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. John Momose Cheyo na Mwenyekiti wa Chama Kipya cha CHAUMA kijana Paschal Kahangala (nitapenda tumjadili kijana huyu na Chama chake katika Thread tofauti ntakayoipost soon pia)  Nikirejea kwa Mzee Cheyo ambaye alikuwa kitoa mtazamo wake kuhusu mijadala na changamoto zilizopo Bungeni, Cheyo amesema inawezekana kabisa kundi kubwa la hoja na mivutano ya sasa inalenga zaidi katika wabunge kusaka umaarufu na kuwa kuna mchanagnyiko wa akili za ujana, umachachari, uelewa na bangi wote katika kundi moja.


  Nilipolisikia hilo nikavutika kumsikiliza mzee wa Mapesa licha ya Star kukamata kwa tabu kidogo huku Bunju, Mapesa anadai kuna matumizi mabaya ya kanuni namba 68 inayotoa nafasi kwa mbunge kuomba taarifa na muongozo wakati anapohisi mambo haypo sawa.
  Cheyo anadai kuwa katika sintofahamu hili wabunge wamekuwa kakijikuta katika sekeseke la kukwamishana kujadili Hoja za msingi tena za maana kwa masilahi ya Taifa kwa kuitumia kanuni hii vibaya huku upinzani ukiathiriwa zaidi na Chama Tawala.
  Anadai ujanja na ushamba kama huo wamekuwa wakitumia madiwani katika vikao vyao vya halmashauri kuonyeshana ujuzi wa kutumia kanuni na ujuaji wa kishamba ambao hauna tija kwa umma.


  Katika kupigilia msumari katika jeneza Cheyo kasisitiza kuwa ni vema wabunge wakajenga utaratibu wa kutumia vikao vya kamati ambapo ni nafasi nzuri kutoa hoja kwa nafasi bila kipimo na kuwa na uezo mkubwa wa kushawishi mabadiliko ya Hoja au mswaada wowote kwa masilahi ya Taifa kuliko kuendelea kutumia jukwaa la kuuza kinyago katika chupa na kusaka ujiko ambao hauna masilahi kwa Taifa.
  Akibariki utetezi na Hoja yake Cheyo kasema hasiti kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchukuzi ambae kupitia vikao vya kamati walifanikiwa kufanya mageuzi makubwa katika kamati hiyo na kupata nyongeza ya fungu la kuhudumia mipango katika bajeti ya Wizara hiyo na kuwa huu ni uzalendo na Hoja ambazo ni kwa masilahi ya Umma.  Akiuma na kupuliza katika nyakati tofauti hakusita kutupa kombora kwa jirani zake wa upinzani akikejeli kwa mzaha kidogo kuwa hataki ifike pahala kwa wazee kama yeye mwenye upara kulazimika kuingia bungeni wakiwa wamevaa helmet kuhofia akili za wabunge ambao wanataka milango ifungwe ili wapigane.  Baada ya mzaha huo karejea tena kukazia kuwa hapa hoja si kupigana ukitaka kupigana nenda uwanjani katika mieleka ambapo pia yupo refarii mwenye kudhibiti mambo huko uwanjani, lakini kubwa hapa ni wabunge vijana kutumia maarifa, mbinu na ujuzi wao wa kitaaluma kujenga hoja katika kamati kuhakikisha mabadiliko yanapatikana kwa mtanzania mnyonge na sio ushabiki wa kutunishiana misuli kwa kukiuka kanuni za Uendeshaji wa shughuli za Bunge na kuishia kuomba miongozo na Taarifa zisizokuwa na masilahi kwa watanzania.  My TAKE:


  • Sikujua hasa nini lengo la nyuma ya Pazia la Mzee mapesa.
  • Lakini kama ndivyo kuna haja gani ya wapiganaji wetu kutobana hoja katika kamati na kuturahisishia maisha kuliko kuishia kutolewa nje na kukosa muda wa kututetea.
  • Ipo haja tujipange vema kumbe zipo dimension nyingi ambazo tunawez kuzitumia kupaza sauti zetu na kusaka unafuu wa maisha kuliko ilivyo sasa.
  • Nakamailisha Thread kuhusu chama Kipya CHAUMA – Chama cha Ustawi na Maendeleo.A
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mzee mapesa ni gamba hata chama chake kakiua kwa sababu ya tamaa
  ya pesa yeye ccm wanampa vi trip kwenda abroad haoni tatizo kwa sisi kulia njaa
  anyway hata watoto wanamjua huyu mzee ni pungufu
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Cheyo is a morally bankrupt politician who stands for nothing expect his stomach. He is worse kuliko hata wale madiwani wasaliti wa Arusha but the real tragedy ni kwamba yuko kwenye 'one-man' party so there is no one to kick him out. Nadhani CHADEMA wekezeni kwenye jimbo la huyu babu. Ameshakula vya kutosha toka ccm sasa ni muda muafaka kwa wananchi wa jimbo lake kuwa uwakilishi imara na sio huu kulamba miguu ya ccm!
   
 4. F

  FredKavishe Verified User

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jana jioni alikuwa mitaa ya rose garden anachapa pombe'ndo maana anaongea upupu atakuwa na hangover
   
 5. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kajisahau kamwaga sifa nyiingi kwa CCM ili aendelee kupewa shavu kama lile la rada.Aisee hawa watadanganyika tuna tabu. kaulizwa swali kuhusu pamba ati anajibu itafika wakati vyama vitakuwa vinajulikana kwa misimao yao, mfano ukisikia pamba, ufugaji na mambo ya kilimo utawasikia CCM. ukisikia Ushirika utawasikia CCM...kaishia hapo ina maana taifa linaendeshwa na pamba na Ushirika
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu Cheo Njaa ndio inayomsumbua ni bora arudi ccm kuliko kuwa kama mzee wa kiranja Mrema. Cheo yupo Bungeni kwa maslai yake sio wananchi na Taifa jumla
   
 7. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  I wish kama ungepata muda wa kuutazama mjadala huu. Tatizo hawa jamaa nao hawajui kujipromote katika mada kama hizi. Bora Yahya anayepost hapa JF mara moja moja licha ya kuwa nae nowdays ON OFF
   
 8. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  :boom:
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nahisi kama Mremaisim ishamkumba
   
 10. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  well hao ni wengi mkuu
   
 11. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wale wale magamba!
   
 12. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwa mantiki hii sitashangaa kuona ile kasi aliyokuwa nayo wakati wa mjadala wa wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuhusu bei ya Pamba kupunguzwa kutoka sh.1100 hadi tshs 800 inayeyuka kama mshumaa. Ila sina shaka CDM pia wapo watu mahiri katika kusimamia Kilimo acha aendelee kuabudia safari na masilahi binafsi.
   
 13. C

  CBN Member

  #13
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Hii mizee cjui kwanini inang'ang'ania kukaa bungeni.. Anaongea maembe tu..
   
 14. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nasikia kumbe amehai kulipiwa deni na ccm kutokana na kuchukua mkopo aliochukua Benki na baadaye mambo kutokwenda vema katika uwekezaji wake.

  Pengine analipa fadhila
   
 15. m

  mndeme JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Muda mwingi yupo na warembo pale Club 84 Dodoma hata bungeni hashiriki vikao vingi unategemea kuwa atatoa hoja huyu? Huwezi kumfananisha na kijana wa kisukuma J J MNYIKA hata kwa chembe
   
 16. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  :boom:

  Twende kazi, huko DOM napo>>>
   
 17. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko kwenye Kamati wajumbe wengi ni Magamba, watakwamisha tu kwa maslahi yao. Bora waseme tu Bungeni wapiga kura tujue mbivu na mbichi.
   
 18. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Pamba hajaongelea kabisa mkubwa?maana anajiita mtetezi wa wakulima.
   
Loading...