Hapa nadhani tunadanganya, tunapenda kukwepa ukweli wa suala hili, hayo maadili ni yepi?Umalaya au kuvaa nguo fupi?
Tuna mifano hai ya wanawake wanaheshimika na kupewa nyadhifa muhimu za serikali ambao wanao vaa kiheshima tena na wengine kujifunika ushungi lakini utakuta ndio wa kwnza kufanya umalaya kisiri, je ni hayo maadili unayo zungumzia yani mambo yafanyike kisiri ?.
Kuto nunua hizo DVD isiwe sababu ya kuwanyima kipato wasanii, kwani hao watoto wako wako kwnye utandawazi , haya mambo watayaona tuu na kuyaiga haswa ya uvaaji, Kikubwa unachotakiwa kufanya ni wewe mzazi kujituma zaidi chapa kazi uwe na kipato kizuri , hakikisha watoto wako wanapata mahitaji yote muhimu na pia hakikisha malezi yako ni bora , kwa kuka na watoto wako kuwa elezea kuhusu maadili mema ni yepi tena kwa upendo,pamoja na kuhakikisha unahishi eneo ambalo ni zuri na haliwezi changia kuharibu watotot wako.
Kumbuka kuharibika kwa watoto kunachangiwa zaidi na wewe mzazi na sio nini wana watch kwnye TV.