Wabongo tunafeli wapi kwenye pricing and location?

Wabongo tunafeli wapi kwenye pricing and location?

Bei za bidhaa za mitandaoni pasua kichwa kwakweli, hazina uhalisia kabisa.
 
Habari:
Nimekuwa nikifuatilia bidhaa nyingi kupitia social medias za wauzaji (kama facebook & Instagram).

Nilichogundua wabongo wengi hawaandiki location walipo na bei ya bidhaa zao wanaficha mpaka uwafate DM..Sasa sijui wanauza mihadarati?

kwamfano Hapa nlikuwa Instagram naangalia duka linalouza swimming costumes,Wengi hawajaweka location wala bei zao na mbaya zaidi unakuta hata DM hawajibu na simu hawapokei.

Nikawa tena naangalia Sehemu gani Dar kuna Swimming pools nzuri na Bei zake lakini wengi unakuta resorts ila hawataji iko wapi au hawataji direction kwenye description unaambiwa ipo kigamboni. hawajui kigamboni ni kubwa?

Hawasemi prices zao za swimming mpaka uanze kuhangaika.(mpaka sasa sijafanikiwa kupata sehemu)

Jamani Tambueni wabongo sisi ni wavivu,,Huo mda wa kukutafta DM au nkupigie bora nitafute muuzaji mwingine aliyeweka wazi price zake.
Matapeli hao.
Walitaka kuniibia milioni 2 wakidai nikishalipa wananiletea tv mpaka mlangoni.
 
Msichojua ni kwamba,
1. Instagram na social media nyingi si wauzaji wenyewe ila ni madalali. Na unajua dalali ni lazima amsome mteja kabla ya kumpa bei.
2. TRA wanachukulia bei uiliyoitaja kikupigia kodi ya kulipa. TRA ni mzigo mzito. Wamefika mahali wanachukua bei kutoka amazon, alibaba ili kukupiga kodi.

3. Mteja wa kweli ataenda DM au whatsap na biashara kufanyika
 
Kuna situation nimekutana nayo kwa madalali wa magari mpaka inastaajabisha.

Gari moja (namba ya usajili ni ileile) ila kila dalali anaitangaza kwa specs tofauti tofauti.

Mmoja 70,000Km mwingine 45,000Km

Mmoja ya mwaka 2009 mwingine 2010 mwingine 2008.

Mwingine 1.5L mwingine 1.8L mwingine 2.0L ila gari moja.

Huyu iko Dar,yule Dodoma na huyu iko Mwanza.

Kuna mpaka Premio na Allion za 1290cc huko au 7 seats na mtu karudia tangazo hilo kwa gari nne tofauti.
 
Changamoto nyingine yakuweka bei watatokea chuki binafsi na kuanza kuiponda bei na hata sio wanunuzi kwahiyo unakuta gafla comment 200 zote ni udaku hili pia ni tatizo jingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom