Machungu ya kukosa umeme,watoto wake wanashindwa kujisomea,mara ooh kapeleka mtoto hospitali kaambiwa dawa hakuna huku zingine zikioza MSD,mke alibwagwa na chini na bajaji huku akiwa na uchungu wa uzazi,mara mama yake kule kijijini mahindi yote yamekauka na kijiji chao hawapewi msaada kwa vile walimchagua diwani wa chadema,binamu yake jirani kwao kanyofolewa mkono na fisi akiwahi kuteka maji alfajiri,mtoto wa mjomba wake akababuka ngozi kwa kunywa maji ya sumu nyamongo,mpenzi wake wa zamani kageuka malaya kwenye dangulo moja baada ya kuporwa ardhi na mwekezaji,jirani yake kaziba uchochoro wa kumfikisha nyumbani kwake baada ya kujenga kiosk cha biashara,mdogo wake alikuwa anasoma kati ya chuo kikuu kimoja juzijuzi hapa kafukuzwa na kurudi nyumbani kwake mzigo juu ya mzigo kwa nini asilale macho na kuende kubandika bango wengi tutabandika mabango Kikwete ni Mapepe hasikii na wala hamjali mtu,na sasa hivi ana hasira za kuchukiwa ameamua kumaliza mpaka senti tano ya mwisho hazina kwa kuzurura dunia nzima,