Waberoya mfano wa kuigwa kwa wakristo wa sasa

Shemasi Jimmy

Member
Apr 23, 2021
93
104
WABEROYA MFANO WA KUIGWA KWA WAKRISTO WA SASA (MATENDO YA MITUME 17:10-12)

Na Shemasi Jimmy 0659 611 252
Hallelujah watu wa Mungu, imempendeza Mungu tujifunze mambo kadha wa kadha kwa lengo la kuelimishana na kuimarishana.

Leo tutajifunza habari za watu wa jamii ya Beroya(Mdo 17:10-12). Waberoya walikuwa wakazi wa mji mmoja uliojulikana kama BEROYA katika MAKEDONIA ya leo, kipindi hicho mji wa beroya ulikua chini ya himaya ya Ugiriki.

Kuna mambo mengi ambayo Mungu anapenda kuzungumza nasi kupitia mfano wa watu wa Beroya, lengo likiwa ni Kuhamasishana na kuonyesha umuhimu wa kupenda kusoma Neno la Mungu peke yako kwa bidii ili uweze kugundua mambo ambayo mengine hujawahi kuyasikia yakihubiriwa. Hasa hapo kwenye kusoma, maana utafiti unaonyesha kuwa kati ya vitu waafrika hawapendi kuvifuatilia na kuvipa maanani ni kupenda kusoma vitabu. “Ndio maana kuna msemo unasema ya kwamba ukitaka kumficha Mwafrika kitu basi kiweke katika Kitabu”.

MSINGI WA SOMO UNATOKA KATIKA KITABU CHA MATENDO 17:10-12
IMEANDIKWA: 10”Mara hao ndugu wakawapeleka Paul na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika Sinagogi la Wahayudi.11” Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.

Tunaendelea kuyaangazia maisha na sifa za watu na wenyeji wa Mji wa Beroya, wakijulikana kama WABEROYA. Lengo letu likiwa ni kutizama sifa walizokuwa nazo ambazo zilipelekea wao kuitwa waungwana.

SIFA YA KWANZA WALIKUAWASTARABU NA WEPESI WA KUJIFUNZA.
watu wa Beroya walikuwa ni waungwana zaidi kwa sababu ya Uradhi na utashi wao kulipokea Neno la Mungu kwa moyo wa kupenda. Watu hawa wa Beroya walikuwa na utayari wa moyo na hawakuonyesha upinzani wowote ule tofauti na sehemu zingine kama vile Watu wa Thesolonike ambao walipinga waziwazi Habari njema za Ufalme wa Mungu zisihubiriwe kwao. Ndio maana Biblia inawataja kuwa wao walilipokea lile neno tofauti na wayahudi wa Thesolonike. MATENDO 17:11a, utaona panasema ya kwamba walilipokea lile neno kwa uelekevu wa Moyo.

SIFA YA PILI – WALIKUWA NA FIKRA ZINAZOTAKA KUKUA (GROWTH MINDSET)
Mindset –Ni akili inayotaka kukua. Hii ni kati ya sifa kubwa ya watu wa Beroya kwamba pamoja na kuwa walikuwa wayahudi ambao walikuwa na msimamo juu ya Torati kama vile ambavyo wayahudi mwengine wa maeneo mengine waliokataa Injili ya Kristo Yesu kupitia Mtume Paulo. Watu hawa walikuwa na fikra zinazotaka kukua. Kuna watu walichojifunza mwaka jana ndicho hicho hicho tu hawakutaka kabisa kujifunza jambo lingine tena katika maisha yao, watu hawa tunawaita kwamba wana FIKRA ZILIZOFUNGWA, ni fikra mgando, ni fikra hazitaki kujifunza upya.

Katika Maisha yetu ni jambo la kiungwana kabisa, kuwa tayari kujifunza mambo mapya na kurekebisha au kufanyia masahihisho mambo kadha wa kadha unayoona yanahitaji marekebisho. Kuwa tayari kukua kifikra na kupenda kujisomea mwenyewe kwanza Biblia na kujiuliza maswali.


SIFA YA TATU –WALICHUNGUZA MAANDIKO KILA SIKU
Watu hawa Biblia inawataja waungwana kuliko wayahudi wa Theselonike kwa sababu waliyachunguza maandiko kila siku ili kupata uelewa zaidi. Hili neno kwamba “WALIYACHUNGUZA” Lina maana kwamba:-
Ni neno la kiupelelezi –kufanya uchunguzi kujua kama ni kweli ya jambo hilo.Lengo la Uchunguzi ni kuelewa pasipo kuamini kwa kusimuliwa na mtu bali wewe unaanza utafiti wako ili uamini maneno ya mtu huyo aliyokusimulia. Kufanya tathimini ya ulichoambiwa au kukisikia
Lengo kuu na mahususi la kufanya Uchunguzi ni kupata

UHAKIKA wa jambo ambalo umesimuliwa au umeambiwa kama ni kweli na ndivyo lilivyo. Watu wa Beroya walihubiriwa na Paulo habari njema za Ufalme wa Mungu wao hawakusema AMINA tu bali waliporudi majumbani mwao waliendelea kuchunguza maandiko katika Vitabu vya AGANO la Kale maana wakati huo Vitabu vya AGANO jipya havikuwepo, kwa hiyo walichunguza maandiko yaliyotabiri kuja kwa Kristo Yesu na ujumbe wake wa Ufalme wa Mungu kurejea katika mioyo ya watu.

Hii ndio iliyokuwa tofauti ya hawa watu wa Beroya na wahayudi wengine katika Israel kwa sababu wao hawakutaka kuchunguza katika Torati ili wawe na hakika kwamba Yesu alitabiriwa kuja ulimwenguni na kuja kuuokoa tena na kuurejeshea Ufalme wake. Ndio maadui wakubwa wa Kristo Yesu walikuwa ni viongozi wa DINI ya Kiyahudi na si wenye dhambi kwa sababu ni watu ambao hawakujisumbua kufanya uchunguzi katika TORATI YA MUSA waliyoiamini ili waone kwamba Yesu Kristo alitabiriwa.

MUNGU wa mbingu na nchi awabariki nyote mliotumia muda wenu wa thamani kusoma chapisho hili. Hakika umejizolea Baraka tele
 
Inapendez sana ukikuta masomo ya namna hii yenye kufunza. Siku hizi watu ni wavivu kusoma vitabu na wamesahau elimu Inapatikana kwenye vitabu. Hata wakiona Uzi mrefu hawawezi kusoma, watu kama Hawa hata katika maisha haya hawapendi kujifunza hususani hata kutokana na makosa Yao wenyewe. .

Pili dunia ya sasa Haina growth mindset, nishakaa na watu Yani akipata Hela anaacha na kazi ikiisha ndio utamuona anatafuta kazi. Watu hawajui hata kuweka akiba, ambayo ingeweza kuwasaidia baadae. Kama binadamu watu husherekea birthday kwa keki na vinywaji wakisahau kuwa birthday ni kipimo Cha personal growth ukitazame kuw je binafsi uko njia sahihi. .

Tatu swala la kuchunguza maandiko Hawana udadisi hivyo wakikutana na andiko lenye ukakasi wanapata shida kuelewa au wanatafsiri kwa urahisi. Mfano tu baada ya adamu kula tunda akajua Yuko uchi, kwa nini hakujua kabla? Kwa nini Mungu alimuadhibu Eva utazaa kwa uchungu baada ya kula tunda. Hapo hapo tunaona Mungu anawafungisha ndoa ya kwanza akiwaambia mtakuwa mwili mmoja, of same mind, ideas etc. Hii inaingiliana na kula tunda Je hili tunda ni nini?

Kama tunda ni chakula Je kauli ya Yesu kuwa chochote kikuingiacho si dhambi Bali kintokacho ndo dhambi. Basi hata ukila mavi si dhambi umeamua kuburudisha nafasi. Ila sasa kitu kibaya kikakutoka rohoni ni dhambi. Hivyo basi kula like tunda pekee ilikuw ni dhambi? Je ukaidi unaweza mpa adhabu ya kuzaa kwa uchungu?

Kuna watu watakuja na mawazo Yao kuwa Adam and Eve walifanya mapenzi, kitu ambacho sijakisema hapa😉😉. Nilichosema ni kwamba huwezi ukala tunda tu Kisha ukahukuniwa adhabu ambazo hazifanani na kosa lenyewe😊

Shukrani sana Shemasi kwa andiko zuri. .
 
Tafsiri, majukumu na maana ya shemasi kwa kanisa Katoliki ni tofauti na hawa wapinzani "protestants"..
Ndio kazi na majukumu Yao hayafanani. Kanisa ndio kinakusimika kuwa wewe ni Shemasi ila Huku kwa wengine mtu anajiita mara askofu, mtume, nabii nk kitu ambacho hujasimikwa Wala hukupakwa mafuta. Hata hapo zamani makuhani walipakwa mafuta na walisimikwa. .
 
Ndio kazi na majukumu Yao hayafanani. Kanisa ndio kinakusimika kuwa wewe ni Shemasi ila Huku kwa wengine mtu anajiita mara askofu, mtume, nabii nk kitu ambacho hujasimikwa Wala hukupakwa mafuta. Hata hapo zamani makuhani walipakwa mafuta na walisimikwa. .
hakika ndugu na unaweza soma 1 tim 3:8-12 utakutana na sifa za mtu anayepaswa kua kuhani ndani ya kanisa la Kristo. barikiwa sana
 
Asante kwa andiko, Kuna Clinic fulani ya tiba asili inaitwa Waberoya,ni ya wasabato,nilikuwa nikidhani ni Jina tu ila kwa sifa hizi nahisi watakuwa walimaanisha hawa jamaa,ngoja nitasoma zaidi nione .
 
Kuna asiye na dhambi? Ajitokeze hapa awe wa kwanza kurusha jiwe
Na kama hakuna mtakatifu kwanini tunasali?
Na Kama hakuna dhambi kubwa wala ndogo kwa mungu,...shemasi anayetamani shape ya mwimba kwaya na mlevi anayekesha anapiga ulabu wote wanatenda dhambi.
Then what's the point ya kwenda kanisani?
Karibuni the cask tupige ulabu wakulungwa
#you only live once
 
Asante kwa andiko, Kuna Clinic fulani ya tiba asili inaitwa Waberoya,ni ya wasabato,nilikuwa nikidhani ni Jina tu ila kwa sifa hizi nahisi watakuwa walimaanisha hawa jamaa,ngoja nitasoma zaidi nione .
barikiwa sana mtoto wa Mungu
 
Back
Top Bottom