Waasisi wa CCM mko wapi?

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,601
338
katika kipindi hiki kigumu ambambo CCM imekuwa na wakati mgumu na hasa kutokana na mwenyekiti wa chama hicho kuwa na uwezo mdogo wa kukiongoza chama hicho lakini nashangaa sana kuona waasisi wa chama hicho kama vile Mzee Malechela, Mzee Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Warioba, cleopa Msuya wapo kimya kabisa pamoja na CCM kuwa na wakati mgumu. Hii inanifanya mimi niamini kwamba ndani ya CCM kwenyewe wazee wengi hawajaridhishwa na utendaji wa JK ambaye sasa amewatenga wazee na kujifanya anawakumbatia vijana. Hii ndo maana wazee wameamua kukaa kimya na kumwachia zigo hili ambalo limemuelemea.

Katika kipindi chote kilichopita hatukuwahi kushuhudia CCM kuboronga kwa kiasi kikubwa namna hii. Hii pia inanipa wasiwasi kwamba mwenyekiti wachama hicho ameshindwa kukiongoza chama na serikali.

hebu tujiulize ndani ya CCM hakuna watu wenye uwezo zaidi ya JK? na kama wapo inamaana hawampi ushauri? na kama wanampa je inamaana anapuuzia? na kama haya yote yanatokea na wazee wenyebusara wako kimya hii inaleta taswira gani? Haya kazi inabaki kwetu sisi wananchi kuamua. Hebu toeni maoni yenu
 
Malecela na Mwinyi ni bora uwatoe hao ni upupu. kama siyo nyerere kuwapinga, muungano ungekuwa chali long time. malecela alimshauri vibaya rais mwinyi kutengeneza serikali tatu na huku mama siti mwinyi akitoa maamuzi ya taifa. hawa wengine uliowataja wameogopa kutoa kauli au misimamo yao kwa hofu ya kuitwa waasi au kunyimwa privilage wanazopata. mkapa angekuwa na la kusema ila bahati mbaya madudu aliyoyafanya na familia yake yamemaliza credibility yake na kuonekana kama walewale. nani zaidi? acha CCM ife in natural death.
 
Utakufa wewe kabla ya CCM....wazee wanakula peshion zao..mambo yanaenda.....we kalia kupayuka.

Timu ya CCM inakuja 2012 kuwafunda nyie chadema
 
Tulieni, bado ticha anageuka kaburini. Soon tutajitambua. Ngoja niagize ki valuuu tena.
 
Back
Top Bottom