Waasi wa Libya kusafirisha mafuta

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Usafirishaji wa kwanza wa mafuta kutoka eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Libya kwa takriban wiki tatu sasa unatarajiwa kuanza.

Makundi ya upinzani nchini humo yanapanga kujaza tangi la mafuta linaloaminiwa kuwekwa karibu na mji wa Tobruk.

Hatua hiyo inafanyika baada ya mashambulio ya anga kuripotiwa kufanywa na majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato dhidi ya wanaomwuunga mkono Kanali Gaddafi na waasi waliozunguka karibu na mji wa Brega.

Serikali ya Libya imebaki ngangari, huku kukiwa na ujumbe unaoitembelea Ulaya ukisistiza kwamba Kanali Muammar Gaddafi hatoachia madaraka.

Wakati huo huo Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiume wa Kanali Gaddafi ameiambia BBC waziri wa mambo ya nje Moussa Koussa hakuisaliti Libya kwa kwenda Uingereza.

Aliiambia BBC kuwa Bw Koussa alisafiri kwenda Uingereza kwa sababu za kiafya na alikuwa akishinikizwa kutoa madai yasiyo sahihi kuhusu serikali ya Libya katika jitihada ya kupata kinga dhidi ya kushtakiwa.

BBC Swahili - Habari - Waasi wa Libya kusafirisha mafuta
 
Cha muhimu ni kujiuliza hayo mafuta yanaenda nchi gani.
Sasa sababu ya kumbomonda Gadaffi zinaonekana hata kabla jua halijachwa!!!!
 
Back
Top Bottom