Waandishi wasidhalilishe taaluma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wasidhalilishe taaluma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, May 5, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  May 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  MWANDISHI wa Habari, ni mtu muhimu kwa taifa na jamii kwa ujumla,
  kutokana na mchango wake mkubwa katika kuelimisha, kuasa, kuonya na
  kuhabarisha matukio mbalimbali, yanayotokea katika dunia, lakini pia
  huweza kuwa mchonganishi na mfitini, iwapo atashindwa kuzingatia
  maadili ya kazi yake.

  Hapa nchini, kumekuwa na habari nyingi zinazoandikiwa kwa lengo la
  uvurugaji na uchochezi, kutoka jamii moja hadi nyingine, au kutokana
  na dini moja hadi nyingine, hata chama kimoja na kingine hali
  inayowafanya wasomaji wa habari hizo kudhani habari zilizoandikwa ni
  kweli na kuanzisha uhasama bila ya sababu za msingi.


  Magazeti mengi, waandishi wao wameshindwa kutumia busara na hekima na
  kuzingatia maadili ya uandikaji wa habari, kwa kuripoti habari ambazo
  kwa muonekano wa jamii, ni zenye kuchochea uhasama, ingawa waandishi
  wenyewe hawalioni hili.


  Vile vile, magazeti nayo kutokana na kujua uuzwaji wa gazeti siku hizi
  ni ushindani, wamekuwa wakikubali kuripoti habari hata ambazo huwa
  hawana uhakika nazo, ili mradi wanajua mapato kutokana na mauzo yake
  kwa siku hiyo yatakuwa makubwa.


  Tumeshuhudia magazeti yakiandika, kwa mfano habari za Mwenyekiti wa
  IPP, katika hali ya kuonyesha chuki dhidi ya watanzania wenye Asili ya
  Asia na kuwasomesha wasomaji, wasiojua chochote kuhusu sakala hilo au
  hata kutokuwa na chochote katika watu hao wawili !
  Mwandishi anatakiwa kuandika habari bila kushinikizwa, wala woga,
  ilimradi habari iwe ya kweli na yenye uhakika, lakini kupotosha kitu
  ambacho wengi wa wananchi walielewa ni nini kilichotokea, ilijenga
  kudhalilisha taaluma hii, ambayo ina mchango mkubwa kwa jamii na taifa
  kwa ujumla.


  Baadhi ya waandishi wamekuwa wakiandika ndani ya habari zao, majina
  kama, uchochezi , papa , Nyangumi , Fisadi na mengineyo ambayo
  'kamusi' za akili zao ziliwatuma kutumia hivyo, lakini bila wao
  wenyewe kujua wanajenga uadui na chuki kati ya wahusika na vyombo
  hivyo, kwa vile mtu yeyote, apewapo sifa mbaya, hujisikia unyonge na
  kujenga chuki.


  Pia, waandishi wengine kwa kutaka kuuza magazeti yao, wamekuwa
  wakitaka tusema sifa kwa kuzikuza habari, kuonekana jambo la ajabu kwa
  kutafutia vichwa vya habari, wanavyohisi kusomeka na kukubalika kwa
  haraka na mnunuzi wa habari, bila kujua wanakwenda kinyume.
  Kwa kutambua waandishi wana wajibu mkubwa kwa jamii katika kutoa
  habari na kuelimisha umma, hawana budi kuzingatia maadili na haki
  zitakiwavyo katika kuandika habari, kwa kuzingatia kuwa, habari hizo
  husomwa na watu mbalimbali, iwapo zitakuwa zenye malengo mabaya, ni
  rahisi kuhamasisha watu wanaoitilafiana katika habari hizo, kuweza
  kudhihiri chuki zao bayana.


  Wengi watakubaliana nami kuwa, hata mgogoro wa Reginald Mengi na
  Rostam pamoja na wengine umekuzwa sana na vyombo vya habari kwa
  kuripoti maelezo toka pande zote zenye malumbano, zenye kejeli na
  tuhuma nzito, jambo linalopelekea wawili wanaogombana kuendeleza chuki
  na mfarakano baina yao.


  Kutokana na kuidhalilisha fani hii, kwa kuandika habari kwa mtindo wa
  bora linunuliwe, ndio maana jamii huwa wanaowagopa waandishi, kiasi
  cha kuwaita 'wambeya' na 'wadaku', kwa nini? Kwa sababu, kwa sikiu za
  hivi karibuni habari nyingi huwa hazina malengo yoyote, zaidi ya
  kupandikiza chuki na kupotosha umma. Turejeshe hadhi ya taaluma kwa
  kuandika habari za kweli, kamilifu na zisizo na upendeleo.
   
Loading...