Waandishi wa Tanzania na habari mtelezo

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,944
2,029
KIla kukicha habari zinazohusiana na mateso ya watoto zinazidi kuibuliwa,lakini hii inatokana na habari ile ya mtoto walompa jina ''mtoto wa box'',tokea hapo dairy wanaripoti habari za mateso ya watoto.

Je, ni kwa kuwa watanzania waliguswa na habari ile,basi wanajua imekuwa njia ya kuuzia magazeti?

Badilikeni, yapo mambo mbali mbali katika jamii mnayoweza kuibua.
 
Nani aliyekuambia kuwa Tanzania kuna waandishi wa habari wabunifu!!!! waandishi wetu wapo kama bendera kufuata upepo.
 
Wasomaji wa Tanzania ni wa ajabu sana. Ikianza habari, ikaishia njiani, shutuma zitarushwa. Mara oooh, wamehongwa, wameacha kuandika! Habari ikishupaliwa ili kujua hatima yake au kupunguza hilo tatizo, ndiyo utasikia udhaifu kama huu wa "hakuna habari nyingine?" Kwenye uandishi kuna kitu kinaitwa current issues. Wakati JWTZ walivyokuwa wakiwakung'uta M23 hiyo ndiyo iliyokuwa habari! Wakati wa mauaji ya albino yalipopamba moto, hiyo ndiyo iliyokuwa habari. Kuanzia mwezi Agosti habari ni kutoka ndani ya Bunge Maaliumu la Katiba. Mwaka kesho kitakachopamba ni habari za uchaguzi mkuu. Hizo ni current issues. Kuwabeza wanahabari ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu si jambo jema. Hakuwatendei haki.

Pasco, tafadhali jitokeze uwape somo hawa ndugu zetu maana naona madongo yanazidi.
 
Si ili msahau yale maswala nyeti ya wizi wa mabilioni kwenye taasisi za umma watu wanahamisha hela kwa viroba weshatujua mazoba tupo wengi ndio maana wanaandika kutupoteza maboya vichwa vya madafu vipo vingi sana tanzania.
 
tatizo ni ubunifu hatuna kuna mambo mengi yanatendeka kila siku yanapaswa kuandikwa natunajionea wenyewe bali hawatak kujishughulisha
 
Back
Top Bottom