Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,919
Juzi na Jana Vyombo vya Habari viliripoti tukio la CAG,DPP na Bulembo, kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM,kumtembelea Raisi Ikulu kwa mazungumzo.Mazungumzo ya CAG na DPP yalikuwa ya kikazi zaidi ila kuhusu mazungumzo ya Bulembo na Raisi nakuachia mwenyewe ung'amue.
Tukiachana na habari ya mazungumzo hayo,kilichonishangaza ni waandishi kushindwa kutumia fursa hiyo kumuhoji CAG na hata Raisi mwenyewe kuhusu safari ya CAG ya nje ya nchi alioifanya hivi karibuni na kuzua mijadala na maswali mengi kama safari hiyo ilikuwa na kibali cha Raisi au laa.
Pamoja na kumuhoji CAG kuhusu mazungumzo yake na Raisi,nilitarajie wangetumia fursa hiyo kuhoji juu ya safari yake hiyo ili aitolee ufafanuzi lakini hawakuthubutu wakaishi kumpiga picha na kumuhoji maswala mengine.
Nina hakika wangekuwepo waandishi wa kimataifa waliokuwa na taarifa juu ya utata wa safari ya CAG, wangetumia fursa hiyo kumuhoji CAG mwenyewe, Katibu Mkuu Kiongozi na pia hata Raisi mwenyewe ili watoe ufafanuzi kwa umma ila hawa wetu hii kwao tena sio habari!!
CC: Pasco , Balile na Manyerere Jackton