DOKEZO Waandishi wa Habari na Media Tanzania, tunateseka sana! Kosa moja, hukumu mbili, kupitia Sheria mbili, Mamlaka mbili Tofauti!. Ni Haki? Tufanyeje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yaani nyie machawa mnatakiwa mfanyiziwe hadi akili ziwakae vizuri. Maana nyie watu wanapotaka mabadiliko mnapewa vijisent vya kununulia vijigari mnajitoa ufahamu na kukwamisha mabadiliko. Yaani hata kukiwa na mamlaka kumi za kuwadhibiti nyie machawa, ni sawa tu.
 
"Kwanini Waziri wa Habari kuteua wajumbe wa JAB badala ya kuacha waandishi tuchague wenyewe wawakilishi wetu"

Hapa ni somo kwamba ukimuona nyoka hata kama hayuko kwenye nafasi ya kufanya madhara ni vyema kutoa tahadhari kwa wote wakuzungukao maana haujui nani atakuwa wa kwanza kupata madhara ya nyoka huyo.

Naam, tulisema humu ndani kupigania haki sio mpaka yakufike.

Kama ambavyo wewe umeshangaa waziri wa habari ambaye by default ni:-

1.Kada wa CCM

2.Mbunge wa CCM

3.Mteule wa mwenyekiti wa CCM

Hawezi kwenda kinyume kwa jambo lololte hata 0.00001% linalowaweka CCM njia panda.

Kama jinsi ulivyoshangaa ndio na sisi tulivyoshangaa na kupinga mwenyekiti wa CCM kuteua

1.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ambaye ni kada wa CCM

2.Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi ambaye ni kada wa CCM

Na wale wajumbe wa tume ambao nao ni makada wa CCM.

Dalili niliziona mapema pale waandishi waliotakiwa kuripoti uchaguzi walitakiwa eti kufanya maombi na kupeleka taarifa zao kwenye hiyo bodi ili waruhusiwe kuripoti matukio ya uchaguzi!

Ni jambo la ajabu sasa eti uchaguzi ili uripoti unatuma maombi ila kusimamia shughuli za tume unateuliwa.

Pia , watu tulihoji humu kwenye katiba kule bado tume inasomeka ni NEC ila CCM wamepigiana pasi za kisigino wameunda INEC kinyume na katiba imeenda kusimamia uchaguzi ghushi kwa tume ghushi ambayo haitambuliki kikatiba.

Mwisho siwezi kukupa pole kwa yaliyokukuta ila nasema ni series inaendelea na kuna waliozishabikia sheria mbovu zote nao siku yao inakuja.
 
Taasisi yoyote ni watu wanaohusika, kuanzia zilizo na zisizo za kiserikali, za kitaifa hata binafsi.
Watu wakiwa wa hovyo, vivyo hivyo taasisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…