Waalimu tugome kama hakieleweki bwana haiwezekani maslahi yetu yanakua vile vile? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waalimu tugome kama hakieleweki bwana haiwezekani maslahi yetu yanakua vile vile?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by harakat, Jun 25, 2012.

 1. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  " HEBU TIZAMA TOFAUTI HII YA KUTISHA YA VIWANGO VYA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMMA WA TZ! ( AJIRA MPYA CHETI)
  MWL 244,400/=
  AFYA 472,000/=
  KILIMO/MIFUGO 959,400/=
  SHERIA 630,000/=
  DIPLOMA MWL 325,700/=
  AFYA 682,000/=
  KLM/MFG 1,133,600/=
  SHERIA 871,500/=
  DEGREE MWL 469,200/=
  AFYA 802,200/=
  KLM/MFG 1,354,000/=
  SHERIA 1,166,000/=

  JE UPO TAYARI KUVUMILIA KUNYANYASWA HIVO KTK UTUMISHI WA UMMAWA TAIFA MOJA LENYE SOKO LA BIDHAA LILILO NA MFUMUKO WA BEI WA KUTISHA?

  UNGANA NA CWT KUDAI NYONGEZA YA MSHAHARA 100%, TEACHING ALLOWANCE, HARDSHIP ALLOWANCE. WAPE SMS HII WALAU WALIMU 20 TU! MSHIKAMANO DAIMA".

  Inadaiwa kuwa mishahara hii ipo kwenye waraka mpya wa mabadiriko ya mishahara itakayoanza kutolewa mwaka mpya wa fedha ( kuanzia Julai mwaka huu). Ongezeko kubwa kwa mishahara ya Kilimo inadaiwa ni kutokana na masharti ya wafadhiri kwenye sekta hii. Walimu wanasadikishwa hili kuwa viongozi wao wa CWT wana waraka huo wa mishara mipya.

  Hapa kwa hili linaloonekana kwa nini waaalimu wasigome ?
  Ni kwa nini watoto wanafeli sana shule za kata na wanafaulu shule za binafsi ?
  nI KWA NINI KUSIWE NA VIONGOZI AMBAO WATALIONA HILI KUWA NI TATIZO
  YAANI TAYARI WAALIMU WAPO KWENYE MGOMO?
  Na je ni kweli kwamba tuna viongozi au watawala ambao hawawezi kutatua matatizo
  ya watu wao mpaka kwa migomo na maandamano kama kwa kesi ya madaktari ?
  Na je kama kweli tunataka kugoma misismamo yetu ni ipi hasa kwani huu wimbo umekua wa
  muda mrefu sana na suala la ngazi za mishahara je nalo libadilishwe ?
  N ahivi vyeo vya Afisa elimu sijui ninini navyo naona havina misingi yoyote iwapo hamna maslahi ya kutosha.

  [​IMG]
  Angalia hii kitu hap ni salary slip ya tgts D3 mtu amekaa kazini miaka minne lakini fedha anayochukua ni dusko
  haieleweki kabisa sasa kwa nini kazi ya ualimu isidharauliwe wakati haiwezi kumfanya mwalimu mwenyewe kuheshimika kiuchumi ?
  Na hapo hapo huyu mtu loan bodi wanakata fedha hiyo dusko kwa nini watoto wasifeli kwani mwalimu ana mawazo ya kodi ya pango ,maji umeme na mambo mengine mengi ?
  Mimi nafikiri serikali aangalie upya mishahara ya kda zote kama ambavyo soko limepandisha bei za bidhaa
  nawasiilisha
   
 2. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Mwalimu ndiye aliyenifundisha kuhesabu vizibo vya soda ili kupata 8+2= , nakukumbuka sana mwl. Damas 1980, kama angekuwa ni wewe uliyeandika uzi huu ningemwambia hivi: mbona umekuwa mjinga siku hizi? Yaani wanakufowadia meseji za ovyo nawe unazituma bila kuzitafuna? Mwl wangu mpendwa siku hizi ni rahisi kupata taarifa, acha kuwa mjinga, unayo haki ya kugoma lakini kugoma bila DATA za ukweli ni utoto!
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nyie hamuwezi kugoma kwa sababu zifuatazo
  Kwanza; Mishahara yenu ni midogo sana
  Pili;udogo wa mishahara yenu unafanya muwe wategemezi wa kazi zenu ili muweze japo kupata milo miwili kwa siku
  Tatu; mmezigeuza shule kuwa sehemu za biashara zenu, hamuwezi kukubali kupoteza kipato cha ziada sababu yamigomo
  Nne; sio wa muhimu kiivyo sababu hata mkigoma hakuna hasara yoyote itakayotokea kwa chama.serikali na taifa zima

  hivyo acheni kutupigia kelele
   
 4. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,648
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Dah! unajibu kama zimefyatuka vile teh! teh! teh!
   
Loading...