Waalimu Maswa wasema wapo tayari kugoma, wasema liwalo na liwe!!

Mnyerede

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
210
230
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Maswa, mkoani Simiyu kimesema walimu katika wilaya hiyo wako tayari kugoma endapo viongozi wao kitaifa watatangaza mgomo.

Alisema watafanya hivyo ili kutafuta haki zao kwani wamechoshwa na ahadi za kila mwaka. Hata hivyo, walimu hao walidai kwa sasa hawataogopa kufukuzwa kazi au kufanyiwa jambo lolote na serikali ambalo litakuwa baya kwao.

Kauli ya walimu hao ilitolewa juzi na Mwenyekiti wao, Onesmo Makota,wakati wa kikao cha Kamati Tendaji wilaya, kilichofanyikia mjini hapa. Makota alisema katika wilaya hiyowalimu wanaidai serikali Sh bilioni 1.2, ikiwa ni madai ya mishahara Sh milioni 997 huku madai yasiyo ya mishahara ambayo ni uhamisho, matibabu yakiwa Sh milioni 159.4.

Alisema chama hicho kimekuwa kikishangazwa na hatua zinazochukuliwa na viongozi wa serikali kwa walimu pindi wanafunzi wanaposhindwa kufaulu katika mitihani yao ya kitaifa, kwa kuwashusha vyeo na kuwadhalilisha.

Alisema vitendo hivyo vimekuwa vikifanyika haraka iwezekanavyo huku wakiwataka walimu kufanya kazi,wakati madai yao ya muda mrefu wakishindwa kuyatatua haraka iwezekanavyo kama wanavyofanya wakati wa matokeo mabaya.

“Kwa niaba ya walimu wilaya ya Maswa, napenda kutamka kuwa tunaunga mkono tamko la Baraza Kuu la Taifa lililotolewa na Rais wa CWT kwa kutangaza mgogoro na serikali,tunasubiri kwa hamu hatua zozote zitakazotuhakikishia, walimu kulipwa fedha zetu zote tunazoidai serikali,” alisema Makota.

Alisema licha ya serikali kuendelea kudaiwa na walimu kiasi hicho cha fedha, bado walimu wameendelea kuhamishwa na halmashauri bila ya malipo, na kusababisha deni kuendelea kuongezeka kila mara.

“Tunapenda kuiambia serikali tumechoshwa na hali hii na tunaomba jamii pamoja na serikali watuelewe wakati tutakapogoma, tuko tayari kwa lolote, hata mgomo tuko tayari,ukitangazwa leo tutaanza, lazima ifike mahali tuseme sasa basi, sisi si watoto kama viongozi wameshindwa kutuhudumia iseme,” alisema.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho, Emmanuel Samara, Asha Guya, Devotha Japhety pamoja na Joseph Fundi, walisema kwa nyakati tofauti kuwa wanasubiria kwa hamu kusikia mazungumzo kati ya serikali na viongozi wao kitaifa yataamua nini.
 
Wasimjaribu na alishasema. Haya shauri yao. Maana Mzee yupo serious. Bora waombe kuongea ongea huenda wakaambulia kitu.
 
Kazi ya walimu ni kuitisha serikali kwa maneno pekee bila vitendo. Kizazi cha walimu ndicho kinachoongoza kwa kuburuzwa na serikali za awamu zote, yaani tangu nchi yetu ipate uhuru.
 
Huyo mwalimu anastahili kua mwenyekiti wa UWT taifa, anaongea kwa hoja. Yule mwenyekiti wao Taifa haeleweki hata anasimamia kipi.
 
Back
Top Bottom