Waalimu kuajiriwa moja kwa moja

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
Mwaka jana nilisikia eti baraza la mawaziri waliamua kuwa mwaka huu walimu kama madaktari wataajiriwa wakiwa bado vyuoni.bado mwezi mmoja tu na sijaona dalili ya kitu kama hicho.mbaya zaidi nasikia serikali haina fedha.au mwaka huu pia kama mwaka jana walimu kusota miezi nane mtaani,wakati shule hazina walimu? Mwenye taarifa atujuze.
 
Hizo ni siasa za wazee wa gamba kama wa nia ya dhati tungeona kwa watu waliomaliza diploma wiki iliopita.
 
wakati waliojariwa february bado wanasotea malipo na mishahara wanapata kimagumashi hadi kwa mbinde unasema waajiri, serikal haiwezi labda mwakani
 
Wanafunz wa UD jana ndo kwanza wamejaza form za kuchagua mikoa wanayoipendekeza kufanyia kaz.
 
Wataajiriwa moja kwa moja na muda wizara inawapangia mikoa waliowahi kujaza hizo fomu. Ila priority ni vijijini so mnaotaka Mbeya, Mwanza, Dar, Arusha imekula kwenu
 
Wataajiriwa moja kwa moja na muda wizara inawapangia mikoa waliowahi kujaza hizo fomu. Ila priority ni vijijini so mnaotaka Mbeya, Mwanza, Dar, Arusha imekula kwenu

Hii ndo shida ya vijana wa Ki-TZ wanarundikana mjini sijui kufanya nini? Sasa wote wakijazana Dar, ARU, MZA sijui hizo kazi watagawana vipi!!! Kaaazi kweli kweli!!
 
Back
Top Bottom