Maamkizi mema, amani na upendo kwa kila mwenye kuisoma mada hii.
Ni imani yangu kubwa kuwa tupo salama na wenye afya njema. Kama kichwa cha habari kinavyosomeka kuna mambo mengi zaidi ya kujadili ili tuweze kufanikisha lengo hili. Kutokana na wimbi kubwa la waafrika kujaribu kukimbia nchi zao na kuhamia nchi nyingine kwa ajili ya hali ya kisiasa, kiuchumi, kimaendeleo na zinginezo, inatupasa tuangaliye wapi tunakosea ili tuweze kuparekebisha na waafrika tuweze kuishi kwa amani, upendo katika bara letu hili tulilopewa na Mungu. Viongozi wetu wa nchi za kiafrika inabidi wafanye mambo ya ziada ili kulinusuru bara hili na machafuko ya vita, ukame, ujinga, maradhi kwani mambo haya ndiyo yanayotufanya tujichukie na tulichukie bara letu, hivyo basi ili tuweze kuishi maisha mazuri tuweke mikakati itakayotuwezesha tufikie malengo yetu tunayoyakusudia, tuweke siasa pembeni na tuangaliye maslahi mapana ya kila mwafrika. Na kwanini ninazungumzia Afrika kwa ujumla, ni kwa kuwa ndiyo tuliyowengi wenye matatizo kwenye nchi zetu na ndiyo wengi wenye kukimbilia Ulaya, wazungu wanakaa mikutanoni kujadili wakimbizi wanaokwenda kwenye nchi zao, kwanini sisi waafrika wenyewe tusijadili kwanini ndugu zetu wanakimbia nchi zao?
Hivyo basi tuchangie mawazo ili tuone tunaanza wapi? na tufanye nini? kwa muda gani?
Ili nasi tuweze kuishi katika maisha ya ndoto zetu na tuwe kimbilio kwa wenye matatizo katika mabara mengine.