Waafrika na Window Shopping NewYork! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waafrika na Window Shopping NewYork!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, May 27, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Tujikumbushe simulizi hii: Waafrika wawili walikuwa kwenye Window Shoping ndani ya mitaa ya NY, USA! Katika pitapita yao, wakaingia kwenye duka moja lililokua linauza bidhaa ya ajabu mno-ubongo wa binadamu!! Kulikuwa na ubongo wa Mzungu, Muasia na Mwafrika! Mmoja wa waafrika hawa aliuliza bei ya ubongo wa kila kabila la watu hao. Alifanya hivyo lakini huku akiona aibu kidogo kwa kile alichoamini kwamba, vyovyote iwavyo lazima ubongo wa mwafrika utakuwa unauzwa kwa bei ya kutupwa! Maajabu ya Mussa, alipotajiwa bei akakuta kumbe ubongo wa Mwafrika ndio unaouzwa kwa bei mbaya zaidi, huku ukifuatiwa na wa Muasia na wa mzungu bei yake ulikuwa karibu sawa na bure! Waafrika wale wakapigwa na bonge la mshangao, lakini huku vilevile wakijiskia bonge la ujiko kuona ubongo wa mwafrika ni very expensive ndani ya shopping malls za NY!
  Baada ya kuzinduka toka kwenye mshangao na ma-feelings ya ujiko, mmoja wa Waafrika wale aliuliza vigezo vilivyotumika katika kupanga bei za ubongo ule. Jibu walilopewa ni kwamba ubongo wa mtasha unauzwa bei ya kutupa kv umetumika mno, since the time when a man started to struggle for living!!It’s almost exhausted! Na ule wa Muasia, umetumika angalau, lakini sio sana na ndio maana bei yake ni kubwa kidogo, na ule wa Mwafrika, ndo haujatumika kabisaaaaa, ndo maana ni very expensive!!Ingekuwa ni ardhi, is like a virgin land in area where its pple dies with hunger from time to time!!
  Jamaa (Waafrika) waliondoka kimya kimya huku bila shaka wakitamani utokee muujiza ili watoweke kabisa eneo hilo ndani ya sekunde moja!!! Kwani ingekuwa ndio wewe bado ungeendelea kujihisi bonge la ujiko?!
  Wapo wanaoiona hii ni sawa na joke! Lakini unapoona mikataba ya kipuuzi (sawa na ile ya enzi za akina Chifu Mangungo wa Msovelo) inaendelea kushamiri nchini kwetu na Afrika kwa ujumla, basi ndipo utakapojuwa hiyo sio joke in reality! Ukiona kiongozi wa serikali anajitapa kwamba wawekezaji wanasaidia miradi ya maendeleo ya jamii kwa ku-cite vi-zahanati vyenye paa mbili huku vikiwa havina dawa, bila kuangalia maandaki yanayoachwa na wawekezaji hao, basi hapo napo fahamu kwamba kweli Waafrika hamnazo! Ukiona kiongozi wako anaenda far east na kurudi na ndoto za kutengeneza artificial rainfall wakati kuna water sources za kumwaga basi rejea simulizi hiyo hapo juu! Ukiona kiongozi, au hata raia anatamba kwamba nchi yetu inakubalika kimataifa kwa kigezo kwamba na ndio maana wafadhili wanaendelea kutusaidia, basi hapo unapaswa kuufahamu walakini uliokuwepo ndani ya ubongo wetu! Unapoona hadi leo hii bado kuna watu wanaoamini kwamba umaskini wetu Waafrika ulitokana na wakoloni kupora raslimali zetu wakati wa ukoloni, basi jivike udalali wa ubongo wa mtu kama huyo kv kuna bonge la kamisheni ndani yake!! Ukiona mtu anailaumu serikali kwenye suala zima la vita dhidi ya ufisadi huku mtu huyo akimwacha DPP anakoroma basi hapa bado inadhihirisha ni namna gani ubongo wetu unavyostahili kuuzwa bei ya ghali! Ukiona mtu anaua albino na kuamini kwamba atakuwa bilionea akifanya tambiko kwa kutumia viungo vya albino basi juwa kwamba ni kweli stahiki yetu african brain kuwa the most expensive brain in world markets, coz’ it’s almost virgin brain!
  Aidha, ukiona watu wanapiga kelele na kutembea kifua mbele eti kv rais wao amekuwa ndie rais wa kwanza Afrika kuonana na Obama, basi hapana shaka yoyote kabisa kwamba ubongo wa watu hawa unastahili kabisa kuuzwa kwa bei ya kuruka kwenye larger shopping malls duniani!!
   
Loading...