mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Picha juu inaonyesha Msaada unaoingia afrika na Jinsi pesa zinavyovunwa afrika ikiwemo.
Kwa Ufupi Msaada kutoka nje kuingia afrika na Tanzania ikiwemo ni Dola Bilioni 30 na Mapesa yanayotoka nje ya afrika kila mwaka ni zaidi ya Trillioni 422 za kitanzania.
PESA ZINAKOPITIA KUTOKA AFRIKA
1: Uvuvi Haramu
2:Mikopo/ Ulipwaji wake
3:Mabilioni ya Pesa kupotea kamatika kupambana na Mabadaliko ya Hali ya hewa.
4:Mishahara inayolipwa kwa watu wanje kutokana na kuwa na Magap ya kiujuzi afrika.
5:Ukwepaji mkubwa wa kodi
6:Uvunaji haramu wa Magogo
7:Kufichwa kwa pesa nje ya afrika mfano Uswizi
8:Faida zinazotengenezwa na Mashirika Makubwa ya kidunia yanayofanya kazi afrika.
9:Kulipa Madeni ambayo ni Matokeo ya Mikopo iliyokuwa Sio ya lazima kukopwa.
Mianya hii tisa ambayo jaha kwetu hapa ipo, ikizibwa vizuri na kutakuwa na haja ndogo sana ya kukopa nje maana tunachokopa ni Kidogo kuliko Tunachovujisha kwenda nje ya nchi na afrika.
Sioni kama huu ni Muda wa kulaumiana. Tunataka akisimama Chadema/UKAWA aseme anatutoa vipi sio CCM imetufikisha hapa, Na maisha yao yaendane na wanachokisema. Tunataka CCM wakisimama waseme kuna makosa Tulifanya huko nyuma sasa Tunapitia njia hii isiyo na makandokando ili Takwimu hizi zigeuzwe.