Wa Kulaumiwa ni Saidi mwema na Wenziwe.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Huyu Mkuu wa jeshi la Polisi ,Mkuu wa Usalama na Waziri wa Ulinzi wana hatia ya kuwafuga mafisadi katika nchi hii,hivi hawa watu watatu wanashirikiana vipi katika kuhakikisha wanaotuhumiwa na ufisadi wanashughulikiwa ipasavyo ili kurudishia imani kwa wananchi dhidi ya serikali yao au wanamsubiri Kikwete ,sasa jamani ikiwa kila kitu atafanya Kikwete si atachanika msamba .
Mkuu wa Jeshi la Polisi ,Mkuu wa usalama na askali kanzu mnatakiwa hawa watuhumiwa iwe mnawafuata kinyemela nyemela ile anatoka ofisini kutangaza kujiuzulu tu mnamweka pingu hapo hapo ,maneno na zamana yatafuata baadae ,ndivyo usalama unavyofanya kazi sio mnangoja watu weshapora weshatulia ndio mnaingia na magari ya polisi kuwakurupusha ,halafu mnazuka na matangazo kilichopatikana ni kiasi fulani kingine hakikuonekna na ndio inakuwa ishu imetoka.
Yaani mnasubiri Kikwete awambie haya sasa kamtieni pingu ,haya sasa mpelekeni mahakamani haya sasa mfungeni,hii si kazi ya Raisi inavyotakiwa watu hawa wakishakutuhumiwa na kujiuzulu hapo hawatakikani kuonekana tena na raisi ila awe anapatiwa habari ya kinachoendelea lakini sio wanakutana uso kwa uso nafikiri mmeona logic hapo inayotokea ikiwa watu hawa watakuwa na mazoea ya kukutana .
Usalama wa taifa na jeshi la polisi lilitakiwa kuwaepusha watu hawa na viongozi wengine wa serikali bila ya kusua sua ,hiyo ni kazi yao kwani kuwaachia ni wazi kabisa wataharibu kila kitu ukiwemo ushahidi ,mnampa mtu nafasi ya kupanga na kupangua na kutafuta washauri wa kisasa ili avuruge kila kitu.
hawa ni watu wa kukamatwa mara moja na kupelekwa kwenye jela za mikoani huko ndani ndani kabisa Nyerere anakujua ,mpaka ushahidi utakapomalizika kukusanywa.
Hivi ndivyo tutakavyoweza kuwakaba makoo mafisadi wa taifa hili Tajiri kushinda yote duniani.
Hawa wanaojiuzulu mmoja mmoja ni kuwekwa pingu hakuna cha ubunge wala ukatibu kata au mtungi ,vipi mtu eti anajizuia uwaziri halafu anabaki na Ubunge uliowalaza na njaa sio mawaziri wenzako wala wabunge ni wananchi waliokupa kura ambao wako vijijini huko wala huna habari nao ,unajiuzulu halafu unataka wakupokee kwa zulia jekundu unazidi kuwafanya wajinga.
Nikija kwenye hili jeshi la Polisi na usalama watu hawa wamekaa kama watumwa wa muarabu ,masikini wanalazwa na njaa na kutumwa usiku na mchana kumtumikia bwana ,bwana wenyewe ni CCM ambao ni majangili na wezi wakubwa wanaoiba uchumi wa taifa hili kwa mamilioni ya fedha za kigeni na sio hii shilingi,polisi hawa wanakuwa mstari wa mbele kuwalinda watu ambao hawajali hata maisha ya polisi wanawasaidia kukimbiza masanduku ya kura ,wanawasaidia kuwabamiza na kuwapa kipigo wananchi wanotaka kumchagua mtu ambae wana imani nae ,polisi wanahifanya mateso haya wakiwa na uhakika jambo wanalolifanya ni dhuluma na wanae mlinda hana imani na hao wananchi wanaochezea kisago cha polisi wala hana imani na hao polisi anaowatuma ,labda awanunulie masanduku ya pombe na kuzidi kuwadumaza akili lakini naamini kabisa hali za maisha kwa jeshi la polisi ni duni tena duni sana tena ya kutupwa kabisa .akili zao zimedumazwa na wao wanaona sifa kupita wakipiga raia masikini za Mungu ambao kula yao ya siku inawapa taabu ,lakini polisi huyu akitumwa na mkuu wa sina tu kwa kuwa mkuu yule ni CCM basi polisi hubadilika na kujiona amepewa utajiri mkubwa na utadhani ndio ameshatosheka kwa utajiri wa kuamriwa kuwa na amri ya kupiga kuuwa na kunajisi ,masikini roho za polisi hawa ambao wanapolala ni kipande cha kigodoro kibovu ,ukimtazama mkewe na watoto wake nguo zao ni viraka vitupu na viraka vingine vimebanduka ,chakula ndio hivyo hivyo cha kuokoteza ,watoto wake wachanga makamasi mpaka mashavuni ,maana dawa za kuwatibu hana uwezo nazo ,sasa unategemea nini kwa polisi wa aina hii wanaoishi kwa kutumwa kwenda kuiba kura au kulinda CCM wafanye wizi wa kura.
Matatizo mnayoyasababisha Polisi ndio haya ya kutuweke viongozi wezi walafi wa mali za Taifa ,nini sifa yeni wanawapa watu hawa mafisadi ,mmewalinda huko kwenye mikoa na wilaya zao mpaka wamefikia Uwaziri na kupora mamilioni ya fedha za kigeni za Taifa hili,Polisi mmefaidika na kitu gani na watu hawa ,ni juzi tu wananchi wamejitolea hizo hizo vijindururu na kuwachangia kupata magari na piki piki au vitendea kazi ,hawa mafisadi wamewasaidia kitu gani ,hawa wakimtajirisha Mahita tu kwa kuwa Mahita akiwatuma nyinyi msiojielewa kumtekelezea ulinzi na kumlinda ,leo Mahita anaishi kwenye maraha lakini nyie makoplo na masajenti wa mitaani mnaolala katika nyumba za mbavu za mbwa mna kitu gani mnapata ,mnatumwa kuwapiga viongozi wa upinzani kwa kuwa tu wanaipinga CCM na kuutetea na kuuelimisha umma juu ya ubaya wa CCM ,nakumbuka mlitumwa kumpiga Lipumba ,yule mwengine mkamvua ngua uwanja wa ndege hivi ,mlipata kitu gani au mlitunukiwa vyeo gani ,kwa ninavyofahamu waliotunukiwa vyeo na Nkapa sio nyie mnaolala kwenye mitaa na raia wa kawaida ambao ni wenzenu katika mahangaiko ya kila siku ,inatakiwa mambo haya muyapime na kuyazingatia kama mnatumwa kumpiga au kumzuia raia asitumie haki yake ya kikatiba basi mnayo haki ya kukataa na hizi ni taratibu za kipolisi kukataa jambo ambalo si haki kulitenda au kumtendea raia kwa ufupi ni kosa.
Lakini mnatumwa kama watumwa wa kiarabu Waarabu na mabwanyenye wameondoka na sasa kuna waarabu weusi ambao wanatumia vyombo vya dola kulinda ufisadi wao kuanzia ngazi za mashina hadi Serikali kuu. Kumbukeni tu kuwa mliokuwa mkiwalinda wanajiuzulu na huku ikiwa tayari wanejikusanyia kitita cha fedha sasa nenda ukamwome akugaie vijisent JUST umwambie kama ulishiriki katika kumsaidia kuiba kura na kukimbia na masanduku ya kurandio yeyey akashinda uone ,Nawashangaa sana mnapokamata marungu na risasi kuwaelekezea raia walio au wanaotumia haki yao kikatiba kwa kuwalinda CCM ,chama ambacho kinatoa viongozi wanaofikia ngazi za Uwaziri kumbe ni wezi na ni hatari kwa maisha yenu na ya Watanzania wote kwa Ujumla.
MUngu IBariki Tanzania Mungu Ubariki Muungano wetu.
Mwiba.
 
Serikali yote imeoza, wote vibaraka, ukichunguza hakuna mtu anayehusika na utoaji maamuzi serikalini anayestahili kubaki, uozo mtupu!
 
Mwiba nimesoma sikufika mwisho lakini nikajua point yako .Mkuu wangu hakuna wa kukamatwa kama Mwenyeliti wa CCM , Rais wa jamhuri na Amiri jeshi mkuu hajasema .Ulisikia kabisa hata Mwema anasema wazi kwamba hawa watu ni hatari yaani hata yeye hawezi kufanya lolote .Mkuu wa usalama ama Mwema hawawezi kuwakamata watu kama Chenge , Karamagi na kundi lao maana hao ni marafiki wa bwana mkubwa .Ukiwakamata watakasema mbona mnamwacha JK hapo Nchi inakuwa imeisha .Mzizi wa matatizo ni CCM na JK hakuna zaidi .
 
Mwiba nimesoma sikufika mwisho lakini nikajua point yako .Mkuu wangu hakuna wa kukamatwa kama Mwenyeliti wa CCM , Rais wa jamhuri na Amiri jeshi mkuu hajasema .Ulisikia kabisa hata Mwema anasema wazi kwamba hawa watu ni hatari yaani hata yeye hawezi kufanya lolote .Mkuu wa usalama ama Mwema hawawezi kuwakamata watu kama Chenge , Karamagi na kundi lao maana hao ni marafiki wa bwana mkubwa .Ukiwakamata watakasema mbona mnamwacha JK hapo Nchi inakuwa imeisha .Mzizi wa matatizo ni CCM na JK hakuna zaidi .

Lunyungu hapa umesema ukweli wenyewe, Tatizo liko kwa uongozi wa juu wa ccm na serikali na sio otherwise!
 
..na bado!

..kama mechi za FA vile. mpira unapigwa kila kona!

..watazamaji mwisho wa siku tunasubiri mabao tu!
 
Back
Top Bottom