The biggest mistake ever ilianzia na sitta kwenye bunge maalum la katiba, maamuzi mabaya ya akina sitta ndio yaliozaa zimwi linaloitwa ukawa. Weekend moja wakati bunge la katiba linaendelea nilipanda ndege kuelekea Zanzibar kutoka dar, mbele yangu walikuwepo aliekuwa mwanasheria wa Zanzibar na waziri wa serikali ya Zanzibar mwanasheria yule alimsimulia waziri madhara watakayopata ccm pindi wakilazimisha katiba wanayotaka wao, naapa kwa jina la Mungu yote aliyoyasema mwanasheria yule ndio yanayotokea sasa, ccm wanalipa gharama kubwa sana kwa kosa la sitta. Kwa uhasama uliokuwepo kati ya chadema na cuf isingekuwa rahisi vyama hivi kuungana na pasingekuwa na ukawa, lakini ona sasa